Akili za kimasikini siku zote hazipendi kusikia kuna gharama za ziada za kufidia, ama kulipa ili kukabiliana na janga ama tatizo lolole lile. Siku zote akili kama hizi hupenda sana kusaidiwa, kupata vitu kwa njia za mkato ama kupewa vitu vya bure,
Gonjwa aina ya UVIKO 19 lenye sura ya "biological weapon" pamoja kuripotiwa kila siku kuwa linaisumbua dunia yote hivi sasa bado kweli kuna watu hawaamini kuwa lipo! Je! Tahadhari zote hizi zinazotolewa na wataalamu wa afya kuna watu wanathubutu kuzibeza?
Kwani kuna yeyote yule kati ya Magufuli ama Mama Samia ambaye amewahi kukanusha kuhusu uwepo wa visa vpya, maambukizi mapya ya virusi na hata vifo vitokanavyo na UVIKO 19? Je! Ama kuna yeyote kati yao kama Rais wa nchi yetu ambaye amewahi kuthubu kuwasihi wananchi kuacha kuchukua hatua stahiki katika kutaka kukabiliana na janga la gonjwa hili tishio kwa maisha ya mwanadamu?
Maandiko matakatifu yanatuambia, "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa". Naam! Tuache siasa, tuache ushabiki, tuache mzaha juu ya wimbi hili jipya. Ni lazima tuchukue tahadhari, kama wewe binafsi huoni ulazima wa kuvaa barakoa ama kuchukua hatua nyingine zinazo shauriwa basi huo ubaki kuwa ni msimamo wako binafsi wala usishawishi watu wengine kufanya hivyo.
Lakini la mwisho ijapokuwa si kwa umuhimu, ni suala la chanjo, bado nakubaliana na wote wale wenye kushauri kuwa liwe jambo la hiari kwa mtu mwenye kutaka kuchanjwa. Wale wenye kusitasita bado wanahitaji kujiridhisha zaidi juu ya usalama wa chanjo hizi mara zitakapoanza kutumika rasmi hapa nchini.