Yesu Anakuja
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 12,675
- 25,924
watapigwa kwa hiari yao, na hiyo ndiyo itakayo justify wao kuadhibiwa na Mungu. Mungu ni Mungu wa hiari, anakupa uchague uovu au utakatifu, umkane au usimkane. wakati huo utakuwa ni wa dhiki kuu ambayo bado haijaja, na mpinga kristo atakuwa ndio mtawala wa dunia hii atakayekuwa ana comand kile kitu na uchumi atashikilia yeye. maana ya dhiki kuu ni mateso ya aina hizo, ndio maana wanasema watu watatamani laiti kama wasingezaliwa kwasababu utakuwa wakati wa mateso. Yesu alisema ole wao wamama wajawazito, na akasema ombeni ili nyakati hizo zisiwe nyakazi za baridi (winter ile ya ulaya inayodondosha barafu, israel kuna winter pia), kwasababu zitakuwa ni nyakati ngumu mno.kama unafikiri watapigwa kihalisi uko wrong side...
kwa hiyo tuseme nyakati hizo ndio hizi tulizo nazo ambazo watu wana uhiari wa kutenda dhambu au wasitende, wamwabudu Mungu au wasimwabudu, waende church au la, wafanye lolote, na mpinga kristo hajaibuka (ila ameshazaliwa tayari anakua umri ukifika ndio ataanza kukinukisha, usiseme nimejuaje, jueni kuwa tayari ameshazaliwa, nusu mtu nusu jini)
ili kuikimbia 666, acheni dhambi ili Yesu akija awanyakue aende na ninyi hewani kwa miaka 7 ambayo hapa duniani mpinga kristo ndio atayatoa makucha yake yote na kufanya mateso hayo. baada ya miaka hiyo 7 Yesu m wenyewe ataashuka toka juu kuja kutawala dunia kwa miaka 1000, na atampiga mpinga kristo na mateso ndiyo yatakoma.
hapo ndipo atakapokusanya watu wote duniani na wale walokufa watafufuta, na sote tutaenda kwenye kiti cha hukumu, kila mtu atahukumiwa kulingana na matendo yake, wengine watapata uzima na kutawala ya Yesu milele, wengine watapata mateso milele na milele. kwa hiyo, wewe kama ni mtu wa Mungu wala usiogope dhiki kuu, haitakukuta, utakuwa umenyakuliwa, ila kama ni mtenda dhambi, utakimbia hadi unyasi kama mnavyokimbia vaccine ya corona.