#COVID19 Chanjo za Kupambana na Corona (COVID-19): Nini Maoni na Mtazamo wako?
kama unafikiri watapigwa kihalisi uko wrong side...
watapigwa kwa hiari yao, na hiyo ndiyo itakayo justify wao kuadhibiwa na Mungu. Mungu ni Mungu wa hiari, anakupa uchague uovu au utakatifu, umkane au usimkane. wakati huo utakuwa ni wa dhiki kuu ambayo bado haijaja, na mpinga kristo atakuwa ndio mtawala wa dunia hii atakayekuwa ana comand kile kitu na uchumi atashikilia yeye. maana ya dhiki kuu ni mateso ya aina hizo, ndio maana wanasema watu watatamani laiti kama wasingezaliwa kwasababu utakuwa wakati wa mateso. Yesu alisema ole wao wamama wajawazito, na akasema ombeni ili nyakati hizo zisiwe nyakazi za baridi (winter ile ya ulaya inayodondosha barafu, israel kuna winter pia), kwasababu zitakuwa ni nyakati ngumu mno.

kwa hiyo tuseme nyakati hizo ndio hizi tulizo nazo ambazo watu wana uhiari wa kutenda dhambu au wasitende, wamwabudu Mungu au wasimwabudu, waende church au la, wafanye lolote, na mpinga kristo hajaibuka (ila ameshazaliwa tayari anakua umri ukifika ndio ataanza kukinukisha, usiseme nimejuaje, jueni kuwa tayari ameshazaliwa, nusu mtu nusu jini)

ili kuikimbia 666, acheni dhambi ili Yesu akija awanyakue aende na ninyi hewani kwa miaka 7 ambayo hapa duniani mpinga kristo ndio atayatoa makucha yake yote na kufanya mateso hayo. baada ya miaka hiyo 7 Yesu m wenyewe ataashuka toka juu kuja kutawala dunia kwa miaka 1000, na atampiga mpinga kristo na mateso ndiyo yatakoma.

hapo ndipo atakapokusanya watu wote duniani na wale walokufa watafufuta, na sote tutaenda kwenye kiti cha hukumu, kila mtu atahukumiwa kulingana na matendo yake, wengine watapata uzima na kutawala ya Yesu milele, wengine watapata mateso milele na milele. kwa hiyo, wewe kama ni mtu wa Mungu wala usiogope dhiki kuu, haitakukuta, utakuwa umenyakuliwa, ila kama ni mtenda dhambi, utakimbia hadi unyasi kama mnavyokimbia vaccine ya corona.
 
16 Pia mnyama wa pili aliwaamuru watu wote, wakubwa na wadogo, matajiri na maskini, walio huru au watumwa, wawekewe alama kwenye mikono yao ya kulia au kwenye vipaji vya nyuso zao. 17 Hakuna ambaye angeweza kununua au kuuza bila ya kuwa na alama hii.

Alama hii ni jina la mnyama au namba ya jina lake.

18 Kila mwenye uelewa anaweza kujua maana ya namba ya mnyama.

Hili linahitaji hekima.

Namba hii ni namba ya mtu.

Nayo ni 666.

16. Kwahiyo hii chanjo tunachoma kwenye mikono ya kulia au paji la uso??
17. Ni bora hata ungeongea bar code, maana bidhaa za supermarket ndio huwezi kuuza wala kununua bila kuwa na bar code!

18. Afadhali ungeniambia namba za simu ndio mnyama mwenyewe ningekuelewa maana kila mtu ana namba zake za simu [emoji2377]
 
16. Kwahiyo hii chanjo tunachoma kwenye mikono ya kulia au paji la uso??
17. Ni bora hata ungeongea bar code, maana bidhaa za supermarket ndio huwezi kuuza wala kununua bila kuwa na bar code!

18. Afadhali ungeniambia namba za simu ndio mnyama mwenyewe ningekuelewa maana kila mtu ana namba zake za simu [emoji2377]
ukisikia neno "mnyama kutoka nchi kavu- mpinga kristo" jua kuwa ni binadamu ambaye hatakuwa wa kawaida kwasababu atakuwa na nguvu sana. atafanya miujiza sana, na ndiye atakuwa mtawala wa dunia hii. maandalizi yake mengine ni new world order aina ya dini ambayo wamarekani wengi wanayo na dini hiyo inaruhusu everything na kuvumiliana, mashoga wanaruhusiwa, free mason wanaruhusiwa, yaani ni order mpya ya naman ya kuishi hapa duniani.

ni binadamu atakayetawala dunia nzima na pia atakuwa karibu sana na taifa ya israel (mnyama wa baharini).
 
Yale yale ya wapinzani wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kutaka kuoneshwa mkataba as if hapo kabla walishawahi kuoneshwa mikataba ya mambo mengine!!!

Je, wewe unaweza kuonesha namba za usajiri ya chanjo zingine zinazotumika Tanzania kutoka kwa hao hao mnaoaminishana wanawaonea wivu?!

Halafu mambo mengine ni ya kutumia tu common sense!! Hivi kama Rais wa nchi ameidhinisha matumizi ya chanjo, hivi unatarajia hao TMDA watashindwa kutoa namba ya usajiri hata wasiporidhika nayo?!

FYI, kwenye hili la COVID-19 siwezi ku-rely kwenye sources za vyombo vya serikali ambavyo vipo politically corrupted!!
🤣 😎🙁
 
Leo ni siku rasmi ya kuzindua uchanjaji wa chanjo ya CORONA kitaifa maarufu kama covid-19 ..! Kidunia kwenye ulimwengu wa siasa biashara na mahusiano ya kimataifa hakuna shida kabisa.. Kwanza chanjo yenyewe tumepewa bure kama msaada! Hatuwezi kuipinga wala hatuna ubavu wa kuikataa. Utaanzaje kuikataa kwa mfano wakati vingine vyote umevikubali?

Kuna unabii wa ajabu kwenye CORONA na kiuhalisia ni hii ni lugha kificho ya NEW WORLD ORDER ...Alama ya yule mnyama anayetawala dunia mwenye number 666 maarufu kama mpinga Kristo..Ant Christ!
Hebu twende kwa ufafanuzi wa namba na herufi
Naweka herufi na mpangilio wake kwa namba kisha jumlisha utapata jibu la kushangaza

CORONA

C 3
O 15
R 18
O 15
N 14
A 1
--- ---
6 66
Hapo ukijumlisha idadi ya herufi unapata 6 na ukijumlisha idadi ya namba za herufi unapata 66 ... Ukiweka pamoja ile 6 ambayo ni idadi ya herufi na ile 66 ambayo ni idadi ya namba za herufi unapata 666.

Hawa ni Illuminant wanaotawala dunia na leo hii rasmi tumezindua madhabahu yao Tanzania kwenye kitengo cha ugonjwa wa corona
Hawa ni watu wanaowaza mbele kabla yetu na hawajawahi kushindwa kitu. Tayari tuna namba ya siri ambayo ni mojawapo ya kutawala dunia. Ni nani leo hii hatumii namba ya siri? Kuanzia kwenye barcode mpaka kwenye msg za kawaida?

Swali muhimu kwanini wametuletea corona kabla ya microchips? Wao tayari wako kwenye microchips.. Kwanini hii imebaki kuwa yao lakini hili la corona ni la wote? Unabii utatimia miaka si mingi..!

Pamoja na haya yote lakini hatuna haja ya kuIkataa chanjo maana tutakufa hata kabla ya misheni ya siri kutimia. Kitakachoumia ni kizazi kijacho miaka 20 ijayo.. Corona ni hatua muhimu ya kuandaliwa kutawaliwa kisasa na kuwa watumwa wao kupitia namba za siri... Madhara yake sio haya ya kiafya.. Madhara halisi yatakuja kwenye kizalia chako...!!!

Ukiweza ukasome Kitabu cha ufunuo sura ya 13 mstari wa 18 ..!
Mheshimiwa Mshana Jr, bado hujachanjwa?
 
🤣 😎🙁
Usicheke Kiongozi, mambo mengine ni kutafuta kukomoana tu!!! Sitasahau siku nadaiwa mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo wakati hata mikataba ya ujenzi wa vyumba vya choo hatujawahi kuoneshwa 🤣 !!
 
Kwani watu wamelazimishwa chanjo?

Wewe toka umezaliwa umepata chanjo ngapi mpaka leo?

Ngoja ujione unavyoruka hilo swali.
 
Ufunuo 13:16-18

Agano Jipya: Tafsiri ya kusoma kwa urahisi

16 Pia mnyama wa pili aliwaamuru watu wote, wakubwa na wadogo, matajiri na maskini, walio huru au watumwa, wawekewe alama kwenye mikono yao ya kulia au kwenye vipaji vya nyuso zao. 17 Hakuna ambaye angeweza kununua au kuuza bila ya kuwa na alama hii.

Alama hii ni jina la mnyama au namba ya jina lake.

18 Kila mwenye uelewa anaweza kujua maana ya namba ya mnyama.

Hili linahitaji hekima.

Namba hii ni namba ya mtu.

Nayo ni 666.
Kwani watu wamelazimishwa chanjo?

Wewe toka umezaliwa umepata chanjo ngapi mpaka leo?

Ngoja ujione unavyoruka hilo swali.
 
"Mimi ni Mama wa Watoto 4, Bibi wa wajukuu, mke lakini pia Rais na Amir Jeshi Mkuu nisingejitoa mwenyewe kujipeleka kwenye kifo nikijua nina majukumu yote haya, hii chanjo ni ya wataalamu na wataalamu wetu wamejiridhisha, NIKO TAYARI Kuchanjwa" Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
 
"Mimi ni Mama wa Watoto 4, Bibi wa wajukuu, mke lakini pia Rais na Amir Jeshi Mkuu nisingejitoa mwenyewe kujipeleka kwenye kifo nikijua nina majukumu yote haya, hii chanjo ni ya wataalamu na wataalamu wetu wamejiridhisha, NIKO TAYARI Kuchanjwa" Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
mshana, kuchanjwa tunatakiwa kuchanjwa tu kwa hiari, ila uhakika hatuwezii kuwa nao kwasababu sio sisi tulioitengeneza. tunaamini kilichosemwa na third party na kuomba tu Mungu, ndio maana hata wao wanasema usaini kuonyesha kwamba ukipata athari serikali haitawajibika, na ni hiari.
 
Chanjeni haraka,mkichelewa mtachomwa sindano kwenye mbususu au kwenye dushe kwa lazima.
 
Kama kuna kipindi niliwadharau wasomi wetu jumla, ni kipindi cha Magufuli. Cha ajabu msomi kama huyu ukimwambia adai katiba mpya Ili haya ya kudhalilisha taaluma yasitokee tena atasema tuache chokochoko!
Angalau alichokisema kipindi hicho kilikuwa cha kitaaluma kuliko hiki cha sasa!
 
Biblia imesema namba hiyo watu watapigwa kwenye paji la uso, na mpinga kristo anaoperate openly na kufanya miujiza yake openly, sio kwa kificho. msikimbie kivuli.
hivi akitokea mchungaji na kuipinga hii chanjo halafu akasema yeye ana upako wa kuwatibu(kinga) watu na watu kweli wakapona,kwa mazingira haya si inawezekana kabisa akatumika na huyo mpinga kristo?
 
hivi akitokea mchungaji na kuipinga hii chanjo halafu akasema yeye ana upako wa kuwatibu(kinga) watu na watu kweli wakapona,kwa mazingira haya si inawezekana kabisa akatumika na huyo mpinga kristo?
nadhani, kuna mchungaji kuongea mambo ya kimungu, na mchungaji kuongea mambo ya akili yake ya kawaida, na sio kosa kufanya yote hayo mawili kama kuna sababu ya msingi hasa kwa hiyo later.
 
Back
Top Bottom