#COVID19 Chanjo za Kupambana na Corona (COVID-19): Nini Maoni na Mtazamo wako?
Ufafanuzi huu unatia moyo kidogo... Kwa hiyo mkuu baada ya kusimamishwa na kuendelea kuna jambo kililorekebishwa ama ni kamari tu,ukiganda damu bahati mbaya kwako?
Miili yetu ina mapokezi tofauti ya chanjo na madawa mengine,ivo kutoa reaction tofauti.kuna watu miili yao haiendani na baadhi ya chemical,mfano mzuri alergy ya karanga au kuwa 'lactose intorelant' unaweza ukawa hata hujaskia lakini watu wana hali hizo ivo chaanjo nazo miili inaweza ikazikataa(hapa sina maana lactose intorelant na karanga alergy zinakufanya ugande damu ukipigwa chanjo ni mifano tu).Waziri wa afya aliliongelea hili vizuri tu,sema ndo watu wapo busy kutafuta video za 'new world order'.

Sent from my SM-G960F using JamiiForums mobile app
 
Maoni ya wataalamu mambo ya chanjo wanasema "hakuna hitaji la kisayansi la kusema chanjo lazima ichukue miaka 5 au 10" .
1.Kulikuwa na uelewa wa hii virus tayari na walijuwa wanaelewa kwa asilimia kubwa
(Researchers were not starting from scratch when they learned about SARS-CoV-2, the virus that causes COVID-19.
SARS-CoV-2 is a member of the coronavirus family.) Corona viruses wapo wengi,ni pamoja wale walosababisha SARS(2002) na MERS(2012) ivo ma doctor walikuwa na data za kutosha,kwa ufupi watu wamekuwa wanawasoma corona viruses kwa miaka ZAIDI ya 50.

(Dr. Eric J. Yager, an associate professor of microbiology at Albany College of Pharmacy and Health Sciences in Albany, NY, told MNT that scientists have been studying coronaviruses for over 50 years. This meant scientists had existing data on the structure, genome, and life cycle of this type of virus)

2.WORLDWIDE COLLABORATION.
-Corona ni pandemic na iliumiza dunia nzima ivo mataifa mengi ambayo huwa kwa kawaida wanafichiana elimu zao ilibidi tu watoe data zao ili washirikiane kupata suluisho.ivo waliweka ubabe pembeni ili kunusurika.
3. FUNDING;Kawaida kunakuwaga na research nyingi zinaendelea ivo kupata pesa inakuwaga tabu na hili ni moja ya sababu research wakati mwengine kusimama au kushindikana, corona ilipokuja pesa zilitolewa kiraisi na kufanya zoezi liende kwa kasi.

4.MATATIZO YA ASTRAZENICA na j&j.
Hili watu wengi wameliongelea lakini naona bado wengi limewapita, zote zilisimamishwa kwa mda na zote baadae zikaruhusiwa na zote bado zinatumika.Matatizo ya kuganda damu ni 'very rare' kuliko faida zake.
Unabidi ikumbukwe wazungu wametengeneza chanjo kwa sababu walidhurika sana na wengi walikufa na uchumi kuporomoka,ivo kwao kupata chanjo ni good news ,hata kama wangekuwa wanakufa 10 kwenye watu elfu chanjo zingeendelea sababu its all about survival!
Corona ipo,inaua na haina dawa kama hutaki kuchanja ni haki yako ila tafuta njia mbadala ya kujikinga sababu corona haijaondoka tutakuwa nayo sana tu,na kuna uwezekano mkubwa kuja kwa vatiant nyingine ambayo inaweza kuwa deadly kuliko delta.


Sent from my SM-G960F using JamiiForums mobile app
Mambo haya hapa:
 
Watu wanajifanya hawajasikia!! Ukichomwa chanjo og inakuwa hivi:
.
 
Watu msiojatambua mmekazana wataalam wataalam.

Hivi unajua kama madaktari wote wa Tanzania ni wachuuzi wa madawa ya kigeni tu?

Ni brainwashed people ambao ukimwambia habari ya dawa from scratch haelewi kitu.

Ukitaka kujua kuwa wataalam hakuna ona ambavyo wanashindwa kujibu maswali kuhusu chanjo, na kuhusu kipimo cha korona. Wanatangaza korona kwa kipimo gani?

Kama hoja yako ni ya kuimba ngonjera za "Sikilizeni wataalam" tusipotezeane muda. Bora uwaite hao wataalam wako waje hapa kuongea.
Wewe ni Juha kabisa. Vipanga wa Muhimbili na wale wa Pharmacy wamesoma mpaka ulaya na Marekani. Huko kote wametuheshimisha kwa ufaulu wa hali ya juu sana.. Wengine wamebaki huko wanategemewa sana.. Kuna ambao wamesoma mpaka Havard na wako pale.. Halafu wewe failure wa Form 4 unakuja hapa kuongea pumba? Hivi unajua ili usome ufikie ubingwa unatakiwa uwe kipanga haswa? Kama kuna daktari kasoma Muhimbili halafu alifeli form 4 kama wewe mtaje.. Uachage ufala
 
Wewe ni Juha kabisa. Vipanga wa Muhimbili na wale wa Pharmacy wamesoma mpaka ulaya na Marekani. Huko kote wametuheshimisha kwa ufaulu wa hali ya juu sana.. Wengine wamebaki huko wanategemewa sana.. Kuna ambao wamesoma mpaka Havard na wako pale.. Halafu wewe failure wa Form 4 unakuja hapa kuongea pumba? Hivi unajua ili usome ufikie ubingwa unatakiwa uwe kipanga haswa? Kama kuna daktari kasoma Muhimbili halafu alifeli form 4 kama wewe mtaje.. Uachage ufala

Watu ambao hamjui elimu ni nini mna shida sana. Mkisikia kwamba huyu ni mtaalam basi mnashindwa kuhoji.

Halafu kuonesha ushamba wako eti Harvard, Marekani na ufaulu wa juu. Utafikiri unaongea na wanakijiji bwana!

Hahahahaaaa yaani ni full burudani.

Yaani unajenga hoja kwa kutumia "appeal to authority" badala ya kuonesha uwezo wako wa kama unaweza kuchambua merit ya hoja.

Mfano mdogo:

Umeshawahi kujiuliza kwanini daktari mahakamani anahojiwa na watu ambao hawajawahi kushika hata themomita?

Na kwa nini ushahidi wake unachukuliwa kama ushauri tu, sio neno la mwisho?

Tumia akili yako vizuri.

Kama huna sema nikuazime.
 
Tusubiri hao milioni waliochanjwa na watakaochanjwa wakifa tunakataa mazimaaaaa
Tatizo effects zake siyo lazima uzione leo! Inaweza ikawa baada ya miaka 10, 15 au kizazi kijacho, hasa kama effects hizo ni intentional.
 
Bila ya kujali kuwa Rais Samia na kundi lake wamechomwa Janssen au hapana; haituondolei uhalali wa sisi kuhoji na kujadili kwa mapana bila ya kupotosha ufanisi na ubora wa Janssen Vaccine. Aidha, hii ni ukweli kwamba kati yetu sisi hakuna anaeweza thibitisha au kutothibitisha kuwa ni kweli Rais na kundi lake wamechomwa Janssen Vaccine au hapana .
Hili libaki kuwa lao na MUNGU wao.

Kama independent entity;
a. Tulitegemea kuona baada ya kuwasili kwa chanjo, Wizara ya Afya ifanye random trials kwa namna ambayo inafaa kabla ya kuwapa watanzania kutokana na record ya Janssen Vaccine. Hili halijafanyika, je wizara imeamua kutufanya sisi Lab testing rats [emoji232] ?

b. Kamati iliyoundwa juu ya UVIKO-19!ilikuwa ni theoretical based yaani ni ku google na google, na mapendekezo yake yalikuwa ni theoretical based dhidi ya existing research za wengine; kamati kama kamati Ilifanya testing gani katika kuishauri serikali juu ya chanjo za aina mbalimbali? kamati ilipendekeza chanjo ya aina gani? na kwa vigezo gani ambavyo ni experimental ?

c. Short na long term effects za Janssen zimebainishwa kwa mantikia gani? au ndiyo sisi tunatakiwa kuzitolea taarifa hizo long term na short term effects post vaccination?

d. Science kwa sasa ni weapon hatari sana, iweje sisi tunaendea haya mambo bila ya kuweka practical base? Integrity's na authenticity ya wizara ya afya ipo wapi? Dhamana dhidi ya watanzania ni kutusomea documents za wazungu au kututhibitishia by testing and trialing scientifically as independent entity?

La mwisho, lakini ambalo si la mwisho kabisa; nashauri kwamba kama Wizara ya Afya, inataka kufanikiwa katika hii vita, iwe PROACTIVE badala ya kuwa REACTIVE. Ni wakati wa kusikiliza zaidi kwasababu Wizara kama Wizara haijafanya experiment yoyote kwenye Janssen, kilichofanyika ni paper based na kupokea maagizo kutoka juu.

Hata hivyo, nashauri kwamba tusishawishi watu kutokwenda kuchanjwa; Wanasiasa na maigizo yao wasiwe ni sehemu ya kukukataza au kukushawishi kwenda au kutokwenda.
Maisha ni yako na MAAMUZI ya kwenda au kutokwenda yatoke kwako.
Wanajua mapungufu yao, sasa wafanye nini zaidi ya kuimba chanjo ni bora?
Arguments za wanaosita ziko wazi lakini hazijibiwi sababu hawawezi, hivyo wanakimbilia kwenye kubeza nakudharau.
 
Panya ni hao wanaochanywa!
Mpaka panya original wanashangaa!
 
Tunasema chanjo hupimwa effectiveness na safety.

Hivi vyote vinataka muda wa kutosha kuvihakiki in short and long term basis.

Chanjo ya corona imetengenezwa under pressure kwa uharaka wa kudhibiti ugonjwa usiendeleee kusambaa zaidi duniani,na haswa ikizingatia ugonjwa wenyewe husambaa kwa njia ya hewa(njia hatari sana).

Mpaka sasa tunaweza kuzungumzia athari chanya au hasi za chanjo hii in short term basis sababu bado ugonjwa wenyewe na chanjo hatujakaa navyo muda mrefu.

Katika short term basis tayari kumeibuka variants ambazo upo ushahidi there is a need for additional booster apart from vaccine itself ili kuweza kupambana na variants watakaokuwa wanajitokeza.

Hatujui how many variants we are going to encounter.

Hapa tayari kwa upande wangu effectiveness ya vaccine ishaingia mashaka.

Na kama effectiveness iko mashakani in long term basis hata safety nayo inaingia doubts,tutakuwa watu wa aina gani tukiwa kila wakati tunadungwa kemikali zinazotemper na dna zetu?!hizi dawa za kawaida tu matumizi ya mara kwa mara zinatuathiri what about chanjo?(tena ya respiratory disease ambayo kila mwaka yana msimu wake lazima yatokee).

Chanjo za magonjwa yaliyopita zilichanjwa huku kukiwa na idadi kubwa tu ya watu ambao hawakuchanjwa na idadi hiyo ya wasiochanjwa haijawahi kuleta new deadly variants kama hii corona.Whats so special about corona variants?!(ambazo ni always deadly hakuna variant inayokuwa less).

Kuna jamii duniani ambazo bado ugonjwa huu sio tishio sana to the extent of taking risk measures kama kuwaintoxicate na a lot of chemicals in the name of vaccine.
Mfano ni sisi waafrika.

Ukitazama speed ya maambukizi Tanzania na kiwango cha athari kilichojitokeza,je,possibility ya kuathirika na deadly variants inaendana na uzito wa kudunga watu wetu haya machanjo ambayo hatujayapa muda wa kutosha wa kuyajua effectiveness na safety in long term basis?

kwanini hatutumii hii resistance ya kinga zetu za asili kuweka other strict measures kuhakikisha tunazuga kidogo muda wa kutosha ili kuona nini kinachoendelea kwingineko?Is it neccessary na sisi kuichukulia corona kama national emergency of level one response?!

Tusisahau kuwa response tunayoipata toka kwa wananchi wa kawaida juu ya chanjo ya corona inatueleza jinsi gani jamii yetu haina habari kabisa na tishio la corona.Kwa hiyo naamini wakati wenzetu kwingineko wanachanja jamii zao kama hatua ya KUDHIBITI(unadhibiti athari ambayo ipo na imeshaleta madhara makubwa) maambukizi,sisi tunachanja jamii yetu ili KUIKINGA(unakinga athari isiyokuwepo au iliyopo kwa kiwango kisicho na madhara lakini yenye uwezekano mkubwa wa kuongezeka baadae).

Kwa kuzingatia njia inayotumika kudhibiti si njia salama sana(kuingiza kemikali mwilini kama ilivyo kwa kunywa madawa mengine na chanjo)then upo umuhimu wa kuzingatia pia kile kinachosababisha hadi sasa ugonjwa huu hausumbui sana jamii ya watanzania.Nacho kizingatiwe na kitumike kutufanya always tuwe ahead of time na advantage.Ikibidi twende mdogo mdogo,tusikimbizane sana na dunia ila tuilinde sana jamii yetu kwa njia za kawaida kwanza.

Waafrika tungeungana kuhakikisha dunia inaheshimu na kukubali uhalisia wa ugonjwa wa corona na njia tunazotumia huku Afrika.
 
Manabii wa chanjo nawaambia hatudanganyiki!! Hata huko Marekani zzidj ya asilimia 50 ya raia wa Marekani wamekataa kuchanjwa! Mpaka rais Biden ameamua kuwabembeleza kwa kuwaahidi hongo ya dola 100 kwa kila atakayekubali kuchanjwa!! Pamoja na kuahidiwa dola 100 kwa kuchanjwa bado Biden amegonga mwamba.
Kitendo cha kutoa hongo kwa raia wake ili kuwachanja ni USHAHIDI tosha kuwa hata duniani kote wanatumia HONGO kushawishi watu wachanjwe!! NI AIBU ILIYOJE?
Huwezi kushawishika kuchanjwa wakati wataalam waliobobea kama huyu wakimwaga nondo za uhakika za kuelimisha watu kuhusu uongo uliopo nyuma ya chanjo!
 
Manabii wa chanjo nawaambia hatudanganyiki!! Hata huko Marekani zzidj ya asilimia 50 ya raia wa Marekani wamekataa kuchanjwa! Mpaka rais Biden ameamua kuwabembeleza kwa kuwaahidi hongo ya dola 100 kwa kila atakayekubali kuchanjwa!! Pamoja na kuahidiwa dola 100 kwa kuchanjwa bado Biden amegonga mwamba.
Kitendo cha kutoa hongo kwa raia wake ili kuwachanja ni USHAHIDI tosha kuwa hata duniani kote wanatumia HONGO kushawishi watu wachanjwe!! NI AIBU ILIYOJE?
Huwezi kushawishika kuchanjwa wakati wataalam waliobobea kama huyu wakimwaga nondo za uhakika za kuelimisha watu kuhusu uongo uliopo nyuma ya chanjo!
View attachment 1874742
Ukitaka kumpinga mtaalam huyu na wewe anza kwa kutupa CV yako kwanza kama alivyoanza yeye kabla.
 
[emoji1787]pole mkuu,hivi hiyo ni ya wap?
Saudia Arabia mkuu,,tumeshaambiwa mabaharia wote kama hutaki kuchanja,,ticket ya nyumbani tayari.

Huku kwanza bila tawakalna huingii duka lolote na ukikamatwa na police huna hiyo tawakalna ni penalty au ndani,,

Unapewa kesi ya kueneza corona kwa maksudi.
Tawakalna ni system wameweka kwenye mitandao kupitia simu,,ukishapimwa corona wana kuweka ktk system kama upo garanteen itaonyesha red sign na kama upo OK itaonyesha kijani..

Na unakuwa nayo kwa muda wote,,ukitaka kuingià lolote iwe sokoni,dukani,ofisi yeyote kama una tawakalna huingii ..na wanakaa mbali na wewe.

Sasa wamekuja na chanjo,,hadi mwisho wa mwezi huu ujao kama huna kadi ya chanjo zao wanazotaka .

Huingii ofisi yeyote ,hotel wala Saudi Arabia huingii...
 
Kituo kituo kikubwa kabisa kinachoshughulika na magonjwa ya kuambukiza cha marekani (CDC) kimelazimika kutoa matokeo yanayoonesha kuwa chanjo haimkingi kabisa aliyechanjwa kuambukizwa corona!! ROBO TATU ya maambukizi mapya yanawapata waliochanjwa chanjo ya corona. Asilimia 80 ya wanaoelemewa na
corona na kulazwa ni wale waliopata chanjo kamili, yaani chanjo mbili!! Hatimaye watu wataelewa tu! Wanapendekeza angalau barakoa zinasaidia. Hawa hapa soma mwenyewe! Ikibidi tafuta mkaliman kama lugha ya malkia ni tatizo!

The CDC released that evidence on Friday. In a study of 469 cases of Covid-19 that broke out in the resort town of Cape Cod, Massachusetts, earlier this month, 74% occurred in “fully vaccinated persons.” Four out of five patients hospitalized were fully vaccinated, and on average the inoculated had completed their two rounds of doses only 86 days before infection.

The cases studied occurred in people vaccinated primarily with Pfizer and Moderna shots, with a smaller number having received Johnson & Johnson’s one-dose jab. No one vaccine was singled out as providing better or worse protection, and none appeared to prevent symptoms from developing. Some 79% of vaccinated patients were symptomatic, the study noted.

Lab testing revealed that 90% of all the Cape Cod infections involved the Delta variant of the coronavirus.

The report lends weight to the argument that the current crop of vaccines aren’t as effective against the Delta variant, although the CDC and World Health Organization (WHO) both insist that vaccination is effective against “severe disease and death” from the virus, to quote WHO technical lead Maria Van Kerkhove in a briefing earlier on Friday.

ALSO ON RT.COM
Governor Abbott threatens to fine local govts that order Texans to mask up as CDC U-turn triggers wave of new mandates
However, the CDC study noted that similarly high viral loads were found in vaccinated and unvaccinated people. Walensky stated on Friday that “high viral loads suggest an increased risk of transmission” and raised concern that “vaccinated people infected with Delta can transmit the virus.” The study itself is less alarmist, stating that “microbiological studies are required to confirm these findings.”

Walensky said that the Cape Cod study was “pivotal” in informing the CDC’s decision to recommend indoor masking. Previously, the agency drew flak from Republicans for using an extremely limited Indian study on viral loads and potential transmission to back up the mask guidance, as was revealed by documents leaked to the Washington Post on Thursday.

The study appears to negate the argument by top health officials that unvaccinated Americans are responsible for the fourfold rise in Covid-19 cases in the US since June. “This is an issue predominantly among the unvaccinated, which is the reason why we’re out there, practically pleading with the unvaccinated people to go out and get vaccinated,” White House coronavirus adviser Dr. Anthony Fauci told CNN on Sunday, adding that the US is currently moving “in the wrong direction” with regard to stamping out Covid-19.
We are all equal
Quote ReplyReport Edit
Messages have been posted since you loaded this page. View them?

Inasikitisha kuona kuwa mataifa mengi kwa ujinga tu na kukosa uzalendo wa kweli, yamejiingiza kwenye mtego mkubwa wa gharama kubwa kwa ajili ya chanjo ambayo mwisho wa siku haisaidii chochote!! Miradi ya maendeleo itasimama na mataifa kutwikwa deni kubwa la muda mrefu!
Hivi haujiulizi: wanakupa chanjo kiasi kidogo kisichotosheleza manitaji ili kukuingiza mtegoni yaani wanakupa "msaada" wa chanjo asilimia 20 ya watu wako halafu wewe ununue au ukopeshwe chanjo kutosheleza asilimia 80 ya watu wako waliobaki!! Lakini mbaya zaidi hata chanjo yenyewe haisaidii, sana sana inakufanya uishi kwa hofu ya madhara ya muda mrefu ambayo hayajulikani, ukiacha madhara ya muda mfupi yanayojulikana kama damu kuganda na kufa, sehemu iliyochanjwa kuwa kama sumaku nk. KINACHOSHANGAZA viongozi wanayajua yote haya na walikuwa wanayazungumza vizuri tu miezi michache iliyopita, lakini sasa wamegeuka kuwa mitume na manabii wa kuipigia debe chanjo ya corona, na kuanza kuwatisha watu na data za corona ambazo awali walisema ni ujinga kutangaza data maana hazijakusudiwa kwa matumizi ya wote isipokuwa kwa matumizi ya madaktari tu. Kulikoni? Kwa nini tusiamini lile dau alilotangaza Biden na wao linawahusu?
 
Mungu akubariki sana kwa ujumbe huu, kila anayemwamini Mungu asikilize na kuchukua hatua.
 
Ingetosha kusema kijana tu bila kuweka msabato, maana ukisema msabato unataka kuaminisha hadhira kwamba'kijana msabato' anawakilisha mawazo ya kanisa, wakati hayo ni mawazo yake tu kama mtu mwingine yeyote.

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
Mungu akubariki sana kwa ujumbe huu, kila anayemwamini Mungu asikilize na kuchukua hatua.


kama mnawapenda watu acheni kuchukuwa sadaka za walalahoji. Biashara yenu kubwa ni kujaza uongo na ujinga masikini.
 
Back
Top Bottom