Chapati ya Kichina, mmea unaoishi kwenye maji, Kombucha/tea mushroom

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Daah...umenikumbusha mbali sana kipindi hiko Bi Mkubwa anafanya kazi Bank NBC alikuja nayo hiyo chapati ya ajabu,na tulikuwa tunaihifadhi kwnye chungu halafu juu tunaifunika kwa kitambaa,jioni mama akitoka job wote tunakunywa yale maji yake kuna kipindi tunavizia wakiacha ufunguo wa ndani kwao tunaingia na kuiimimina ile juice na kuinywa ilikuwa na ladha nzuri na tamu sana,mama alisema walipeana huko ofisini kwao na wafanya kazi wenzao wa Banki halafu sikumbuki ilipoteaje maana ilikuwa ni miaka ya 90 kipindi hiko..
Umenikumbusha mbali sana na hiyo Chapati ya ajabu
 

Mkuu, ilikuwa nzuri sana kwakweli,

sijui nani bado anayo atusaidie hapa!

Atakuwa ametufaa sana!
 
Ulikuwa unauweka kwenye maji kiasi Gani?

Inategemea na chombo na chapati yako!

Mara nyingi ilikuwa kama kwenye sufuri la ukubwa wa chapati hiyo basi maji unaweka nusu au nusu na robo!
 
Ulitamba sana kwenye miaka ya mwishoni ya 90'.
Kila mtu akikatia kipande cha ' Fungus' mwenzani ili akaoteshe kwenye maji? Sijui ulipotelea wapi...
Ulikuwa ukilishwa chai ya rangi. Juice yake ilikuwa tamu sana. Nami niliupoteza kwa kutoongeza hiyo chai, kwenye hiyo miaka ya 90s.
 
Nakumbuka tulikuwa kunaweza chai ya rangu sio maji
Sadakta. Uliwekwa chai ya rangi. Unauweka na baada ya siku kadhaa unamimina kwenye chombo na kunywa. Ikilala asubuhi una kuta utando juu, ndio inaanza hivyo, si lazima ukate kipande.
 
Mkuu; Jaribu University of Dar es salaam
 
Zile ni fungus. Hivyo ukimega kakipande kadogo ukaweka ktk chombo kingine ina- multiply.
 
Duh!

Kweli ni mmea mzuri sana, kuupata ni adimu sana, nimejitahidi sana kuutafuta humu mtaani bila mafanikio! Nikaona bora nije humu kwa waungwana najua sitakosa hata mawazo ya wapi pa kuupata!

Maana penye wengi hapaharibiki neno!
Ukiupata rudi hapa utugawie. Mimi niliutumia miaka ya 80
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…