Uchaguzi 2020 'Charisma' ya Tundu Lissu itazidi kumpa shida sana Magufuli na CCM kwa ujumla

Uamuzi wa chama tawala kutangaza watakachokifanya wakiwa na ilani mkononi umezingatia matakwa ya siasa za kisasa.
Wameamua kujitambulisha kwa kuweka hadharani wanachokifanya na wanachotarajia kukifanya.

Ni uamuzi wa kisayansi wenye kwenda sambamba na ukweli kwamba Lissu na CDM wakiwa Dodoma basi CCM wanaendelea na kampeni sehemu tofauti..Mam Samia Morogoro, Majaliwa Longido na JPM Shinyanga.

Chama tawala kina ukomavu mkubwa wa kisiasa sio rahisi kuzidiwa maarifa na CDM hii ya sasa.
 

Magufuli amefanikiwa kuwakumbusha wananchi kwamba utajiri wetu tuliopewa na Mungu ni fursa ambayo inaonewa wivu na majirani zetu pamoja na baadhi ya “wazungu”.

Anaposema nchi yetu ni tajiri wale wenye kuijua Tanzania wanamuelewa vyema na wanaelewa maana ya ujenzi mkubwa wa miundo mbinu unaofanywa kwa pesa nyingi.

Wapenda siasa wapo lakini hawana wingi kama ule wa wale wanaoelewa ukubwa wa nchi kiuchumi ambao unatafutwa kwa ujasiri.

Siasa za kimagharibi ni za msimu huu wa kuelekea uchaguzi, lakini ujumbe wa kujenga mazingira wezeshi kiuchumi umeshawaingia watanzania wenye kuitazama nchi yao kwa mtazamo chanya.
 

Wewe una uhakika kuwa Chadema wanakujua?.

Unaufahamu vyema uwezo wa Kaka Freeman wa kuwatumia watu na kuwatupa baada ya kufanikisha malengo yake?.

Waulize wanaoijua vyema Chadema watakueleza mengi usiyoyajua.
 
Magufuli atumie muda huu wa kampeni kuaga. Tarehe 28/10/2020 hatatoboa. Wajumbe watafanya wanayoyajua.
 
Charisma ya kuongea tu haileti maendeleo kwa taifa. Magufuli hata sasa akiukwaa ububu, ameisha prove kwamba ni kiongozi wa aina gani! Vitendo vyake vinatosha kumtangaza! Lissu ni maneno tu ya vijiweni ya Yanga na Simba!

Kwa mfano, Kutiririka maneno kama - mmeona raisi wa awamu ipi amejenga reli? Reli zilijengwa na wajerumani na waingereza - TAZARA na mchina enzi za Nyerere!. Yaani anabeza utawala wa JPM kujenga SGR! Hiyo ndiyo Charisma ya kuongea unayotueleza!?

Kuongea tu hatutaki sisi wananchi - Kuongea tu kumepitwa na wakati tunataka kazi na vitendo na matokeo yaonekane!
 
Kuanzia sasa Lissu amekwishaongeza wapiga kura kutokana na hotuba zake jukwaani. Watu wanataka maendeleo yao na siyo ya vitu.
Huwezi kuwa na maendeleo ya kudumu ya watu pasipo kwanza kuwa na msingi wa maendeleo ya vitu.

Mataifa makubwa yalianza kwa kujenga vitu miaka mingi iliyopita.

Wale black lives matter wanataka minara mingi ya wazungu maarufu ibomolewe kwa sababu ni watu waliofanya biashara ya watumwa waliofanya kazi ngumu ya kuyajenga maendeleo ya vitu, ambayo ndio msingi wa ubepari wenyewe.
 

Inahitajika akili kubwa sana kuweza kuupinga mradi kama ule wa SGR halafu wenye akili timamu waweze kukuelewa.

Anabeza ujenzi wa reli ambazo ni akili za mawakala wa wenye wivu wanapoona kuwa reli ile inakwenda kuimarisha uchumi wa nchi.

Magufuli keshaeleweka anafanya nini na anataka nchi hii ielekee wapi.
 
Ndio Maana wakampiga Risasi
 
Jamaa anauwezo mkubwa sn wa kujieleza, mwenyewe nilitamani kipindi kiwe hata na masaa ma3
 
Mkuu nimekuelewa, nimekupata vizuri sana na Mungu akubariki uendelee kutoa hamasa huko uliko ingawa ID yako mkuu kwetu ni tusi sijui unatuachaje sasa? Shida yangu kwa Lissu itakuwa kujulikana kwake kule vijijini ambako watu wanalishwa matangopori eti wapinzani wataleta vita! Siasa za kipumbavu kabisa, halafu na tume nayo imekaa kimya tu! Nashauri chama kichspishe banners za picha ya Lissu na kila mgombea ubunge na udiwani apewe hiyo picha awe anazunguka nayo kwenye kampeni zake kama alivyofanya mzee Nyerere kwa Mkapa mwaka 1995. Watu vijijini hawamjui Lissu tutapigiwa huko!!
 
Anakinzana balaa. juzi aliwadanganya watu wa ikungi eti anampenda lissu akakinzana na ile kauli ya siku ya ripoti ya makinikia kuhusu kazi za wanajeshi kule kwenye vita.

Atuachie nchi yetu hafai. hana utu. muuaji wa demokrasia. siyo mstaarabu.
Jana tena kajikoroga hapa Shinyanga wakati anamnadi Katambi. Anatuambia eti nileteeni huyu kijana nampenda sana. Akawa amesahau kama alishasema waliokimbia uteuzi wake kwenda kugombea ni watu wenye tamaa ya madaraka!
 
Mimi namwomba Mungu atende maajabu tu huku ,mkoloni mweusi inatosha aisee si kwa maumivu haya.
Mungu atusikie maana tukienda miaka mitano mingine kitakachotupata hakifurahishi.
 
Naam , CHADEMA inatakiwa iweke mikutano mingi sana midogo midogo ngazi za kata na vijiji na wawe focused ni kijiji au kata ipi raia wake hawawajui wapinzani na faida zao iwapo wakipewa madaraka ili raia wafunguke bila hivyo huo ni upenyo wa ccm kuvukia
Huku mijini wanaeleweka hilo lipo wazi maana watu wa mijini ndiyo wanajua siasa na walichotendewa na utawala huu kwa miaka 5 (wanayo elimu ya uraia kwa upana zaidi)
 
Kiufupi tu ni kwamba jamaa hana charisma, na amekuwa anapata shida sana kujinadi kama mnavyojionea wenyewe. Ndiyo maana kampeni zake zimekuwa kutaja madege, meli, SGR na Stiegler's Gorge kana kwamba sisi tunakula hivyo vitu. Na kwa bahati mbaya sana hata wale wabunge 18 waliopita bila kuenguliwa (sio kupoingwa) hawana pia charisma ya kumsaidia boss wao.

Hii ni aibu kwa chama kikongwe kama CCM kukosa watu watu wa aina hiyo wakati iliwahi kuwa nao huko nyuma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…