Chato: Yaliyojiri katika Maadhimisho ya mwaka 1 wa kifo cha Hayati Magufuli. Kasala, tusimamie ukweli na haki. Samia kuendeleza Mema

Chato: Yaliyojiri katika Maadhimisho ya mwaka 1 wa kifo cha Hayati Magufuli. Kasala, tusimamie ukweli na haki. Samia kuendeleza Mema

Mungu ni mwema kwa wote waliompenda na wasiompenda .ila Mungu alimpenda zaidi na alisikia maombi ya wengi ndio maana hayupo.Nchi imekuwa shwari,tuna amani mioyoni mwetu ,watu waliishi kama wako Ukraine why,watanzani walio wengi hawakujua wafanyeje wale waliokua na roho ya "nacist "walishangilia wenzao kufungiwa account, kunyanganywa hela kwa nguvu ,kupotea kwenye mazingira ya kutatanusha na pia kubambikiwa kesi za uhujumu uchumi.Tuanatoa pole kwa familia Mama Janet na Watoto Mungu awape nguvu ila mmepumua sasa hata umenenepa mama yetu ingawa kuondokewa na Mume sio jambo jepesi
Sherehe ya Leo ni kubwa sana hasa tukikumbuka wapendwa wetu waliouwawa na huyu mtu.

Bora alikufa Tena kifo kibaya
 
Mungu ni mwema kwa wote waliompenda na wasiompenda .ila Mungu alimpenda zaidi na alisikia maombi ya wengi ndio maana hayupo.Nchi imekuwa shwari,tuna amani mioyoni mwetu ,watu waliishi kama wako Ukraine why,watanzani walio wengi hawakujua wafanyeje wale waliokua na roho ya "nacist "walishangilia wenzao kufungiwa account, kunyanganywa hela kwa nguvu ,kupotea kwenye mazingira ya kutatanusha na pia kubambikiwa kesi za uhujumu uchumi.Tuanatoa pole kwa familia Mama Janet na Watoto Mungu awape nguvu ila mmepumua sasa hata umenenepa mama yetu ingawa kuondokewa na Mume sio jambo jepesi
Kesho unakufa
 
Leo ni Maadhimisho ya Mwaka mmoja Tangu Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli atukote. Maadhimisho hayo yanafanyika mkoani Geita katika wilaya ya Chato.

Maadhimisho hayo yatahudhuriwa na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia suluhu, Makamu wa Rais Dkt. Isdori Mpango, Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi na viongozi mbalimbali wa serikali ya Jamuhuri.

Pia soma Taarifa ya Msiba

Kusoma Historia yake soma zaidi hapa

===
LIVE UPDATES yanayo jili viwanja vya Chato
Pengo lake halina spea, serikali yake ilisifika kwa utekelezaji serikali ya sasa hivi inasifika kwa maneno na malalamiko mengi bila utekelezaji.

Wale wenye mimba zako za chuki kwenye vichwa na mawazo yao, waliodai "hamna uhuru wa kujieleza ",baada ya kuingia Mama wakadai sasa hivi kuna uhuru wa kujieleza, cha ajabu.

Pamoja na uhuru wakujieleza.
1.Mgao wa umeme kimya
2.Mgao wa maji kimya.
3.Tozo kimya.
4.Bei ya mafuta imepanda tokea mwaka jana mwishoni, amabayo imegusa bidhaa nyingine kimya.
5.Watu wanajipigia hela plus utendaji na uwajibikaji wa watumishi umepungua kimya.

Unajiuliza sasa uhuru wa kuongea walikuwa wanaudai katika mambo gani, ikiwa mambo yanayo yagusa wananchi hawaongei labda may be aliwabana sana kwenye issues zao za Magendo.

Bahati kwa nature ya kazi yangu nimezunguka sana baadhi ya mikoa,nimeshudia hospitali ulizojenga kila wilaya, mahakama kila wilaya barabara za kisasa,nimeshuhudia majengo mapya ya ofisi za wakuu wa wilaya na wakurugenzi na zaidi nilishuhudia barabara ya km 50 ya zege kuelekea Ludewa.

Pumzika tu ila pengo lako halina spea, vitu ulivyo vifanya vinaonekana huitaji kutumia nguvu.

RIP Chuma John Pombe Magufuli.
 
Nipe tathimini ya kiuchumi ya ilo daraja refu la busisi , au huko linako elekea Kuna resources gani ambayo itainua uchumi wetu, otherwise ni zawadi kwa mkwe wake kama wanavyosema wengi
Kweli unaumri mdogo sana tokea umezaliwa na kuijua hii nchi.... nakumbuka mwaka 1985 ndio niliingia Mwanza mjini nikitokea Dar wakati huo wakazi wake hawakuzidi 200k kifupi tulikuwa tunafahamiana mpaka kwa majina ya utotoni. Mwanza ni mji unaokuwa haraka sana miaka 35 baadae ni jiji lenye wakazi wasiopungua 1.5m (kwa wilaya za Ilemela na Nyamagana).

Mwanza ni jiji lenye viwanda vingi zaidi kwa eneo lote la kanda ya ziwa, jiji lenye soko kubwa la bidhaa za samaki, jiji lenye soko kubwa la bidhaa za kilimo, jiji lenye njia nyingi za usafirishaji kuanzia reli, barabara, anga na maji. Mwanza pia ni jiji lenye biashara kubwa ya madini, ngozi na utalii. Kuhoji faida za daraja la Busisi inanipa mashaka na uwelewa wako wa njia za kukuza uchumi kwenye maeneo.

Ikiwa unazungumzia viwanda lazima kuwe na njia bora na rahisi za kuingiza malighafi na kutoa bidhaa kwenda kwa wateja wa mwisho kwa haraka. Ukumbuke idadi kubwa ya wacongo wananunua bidhaa za samaki toka Soko la mwaloni ambalo ni moja ya vyanzo vikubwa sana vya mapato mkoa wa Mwanza.

Wavuvi wanafanya shughuli zao ziwa Victoria wanategemea soko lao kuu ni Mwanza kuanzia samaki wanaoingia viwandani mpaka wanaoelekea kwa wateja bila kuchakatwa kupia viwanda vikubwa... (Dagaa, Sato na Sangara), wavuvi wa Mkoa wa Geita na maeneo ya Sengerema wanasafirisha samaki kwa boat na Barabara kutegemea Jiografia ya eneo na wengi watatumia Daraja la Busisi ambalo kwanza ni nafuu na haraka kuliko vivuko vya Busisi na Kamanga.

Wafanyabiashara wa Congo, Burundi na Rwanda watalitumia kama wanavyotumia sasa kivuko cha Busisi ambacho utalazimika kusubili saa nzima kuvuka upande wa pili wakati daraja utatumia dk 3 tu.

Faida ni nyingi mno kwa wakazi wa Bukoba Sengerema Geita Kigoma na maeneo mengine. Fanya homework yako ndio uje kuhoji umuhimu wa kiuchumi aliuona JPM na kuamua kuweka bilions of money kwenye hilo Daraja
R.I.P jemedali.
 
1. Daraja la Tanzanite Dar
2. Mikataba ya madini
3. Ukuta wa mererani
4. Utumbuaji
5. Uzinduzi wa malipo ya serikali kupitia control number
5. Umeme wa Tsh 27,000/=
6. Elimu bure darasa la kwanza hadi form four
7. Ukarabati wa. Viwanja vya ndege na meli
8. Bomba la mafuta Hoima kwenda Tanga
9. Kuanzisha Tarura, Latra,
10. Kununua radar kwenye viwanja vya ndege vyote.
11. Kuivunja bodi ya ununuzibwa madini
12. Kuanzisha tume ya madini na madoko ya kuuzia madini
13. Kuvunja Jiji la Dar es salaam
14. Kumfukuza kazi Nape mnauye, mchechu wa NHC,
15. Kwa miaka mitano kutokwenda ulaya
16. Kuzirudisha halmashauri zote ofisi ya Rais.
17. Kuondoa watu wenye vyeti feki kwenye mfumo wa mishahara ya serikali.
18. Kukarabati shule za serikali za zamani
19. Kununua ndege mpya 11
20. Kufufua reli ya Dar to arushaTanzania
21. Kukarabati bandari ya mtwara, tanga na Dar
22. Kukusanya na kuzitambua mali za CCM
23. Kuanzishwa wizara mpya ya Madini
24. Miaka mitano umeme haujawahi kukatika
25.ujenzi wa hospitali za kanda, mikoa na wilaya
26. Ujenzi wa mshakama za wilaya
27. Kuongeza idadi ya hifadhi za tsifa na jeshi usu.
28. Kufuta mishahara ya 45,000,000
29. Kuongeza viwanda nchini
30. Kuwaeleza ukweli watanzania kuhusu covid 19
31. Kupunguza urasimu kwa watumishi wa umma
32. Kuanxisha ofisi za msajili wa hati za ardhi kila mkoa na kufuta ofisi za kanda
33. Kukamata wakwepa ushuru
34. Kampuni ya Halotel ya JK , wabia wake kwenda segerea kwa kutokulipa kodi
35. Serikali kununua magari yake kwa mfumo maalumu kupunguza madalali
36. Kiswahili kuanza kutumika mahakamani kutolea hukumu
37. …..,, Samia haya niliyoyataja anayaweza kuyasimamia?kuyaendeleza?kubuni vingine ? CCM tujiuliza maswali kabla hatujamwambia Samia achukue fomu 2025
Mkuu pole kwa msiba wa JPM

Naomba kuuliza kutoa hukumu kwa kiswahili kuna tija gani wakati kiswahili hakijitoshelezi chenyewe

Tungefanya kwanza tafiti ndipo tuanze kukitumia
 
1. Daraja la Tanzanite Dar
2. Mikataba ya madini
3. Ukuta wa mererani
4. Utumbuaji
5. Uzinduzi wa malipo ya serikali kupitia control number
5. Umeme wa Tsh 27,000/=
6. Elimu bure darasa la kwanza hadi form four
7. Ukarabati wa. Viwanja vya ndege na meli
8. Bomba la mafuta Hoima kwenda Tanga
9. Kuanzisha Tarura, Latra,
10. Kununua radar kwenye viwanja vya ndege vyote.
11. Kuivunja bodi ya ununuzibwa madini
12. Kuanzisha tume ya madini na madoko ya kuuzia madini
13. Kuvunja Jiji la Dar es salaam
14. Kumfukuza kazi Nape mnauye, mchechu wa NHC,
15. Kwa miaka mitano kutokwenda ulaya
16. Kuzirudisha halmashauri zote ofisi ya Rais.
17. Kuondoa watu wenye vyeti feki kwenye mfumo wa mishahara ya serikali.
18. Kukarabati shule za serikali za zamani
19. Kununua ndege mpya 11
20. Kufufua reli ya Dar to arushaTanzania
21. Kukarabati bandari ya mtwara, tanga na Dar
22. Kukusanya na kuzitambua mali za CCM
23. Kuanzishwa wizara mpya ya Madini
24. Miaka mitano umeme haujawahi kukatika
25.ujenzi wa hospitali za kanda, mikoa na wilaya
26. Ujenzi wa mshakama za wilaya
27. Kuongeza idadi ya hifadhi za tsifa na jeshi usu.
28. Kufuta mishahara ya 45,000,000
29. Kuongeza viwanda nchini
30. Kuwaeleza ukweli watanzania kuhusu covid 19
31. Kupunguza urasimu kwa watumishi wa umma
32. Kuanxisha ofisi za msajili wa hati za ardhi kila mkoa na kufuta ofisi za kanda
33. Kukamata wakwepa ushuru
34. Kampuni ya Halotel ya JK , wabia wake kwenda segerea kwa kutokulipa kodi
35. Serikali kununua magari yake kwa mfumo maalumu kupunguza madalali
36. Kiswahili kuanza kutumika mahakamani kutolea hukumu
37. …..,, Samia haya niliyoyataja anayaweza kuyasimamia?kuyaendeleza?kubuni vingine ? CCM tujiuliza maswali kabla hatujamwambia Samia achukue fomu 2025
Kama hakuacha mifumo ya kuibua, kusimamia na kuendeleza hivyo ulivyovitaja basi hakuwa na nia njema!!

Alafu fikiria kwa undani mna over spend kwenye kumbikizi wakati wapo vijana mitaani wenye mahitaji na hawajui hatma yao! Kama alikuwa bora mnavotaka tuamini mngetafuta namna bora ya kumkumbuka!

Mfano mdogo... watu wote muhimu ukumbukwa siku za kuzaliwa kwao na si za kufa!

JPM alale anakostahiki! Mmethibitisha hana umuhimu wowote!!
 
Back
Top Bottom