Kweli unaumri mdogo sana tokea umezaliwa na kuijua hii nchi.... nakumbuka mwaka 1985 ndio niliingia Mwanza mjini nikitokea Dar wakati huo wakazi wake hawakuzidi 200k kifupi tulikuwa tunafahamiana mpaka kwa majina ya utotoni. Mwanza ni mji unaokuwa haraka sana miaka 35 baadae ni jiji lenye wakazi wasiopungua 1.5m (kwa wilaya za Ilemela na Nyamagana).
Mwanza ni jiji lenye viwanda vingi zaidi kwa eneo lote la kanda ya ziwa, jiji lenye soko kubwa la bidhaa za samaki, jiji lenye soko kubwa la bidhaa za kilimo, jiji lenye njia nyingi za usafirishaji kuanzia reli, barabara, anga na maji. Mwanza pia ni jiji lenye biashara kubwa ya madini, ngozi na utalii. Kuhoji faida za daraja la Busisi inanipa mashaka na uwelewa wako wa njia za kukuza uchumi kwenye maeneo.
Ikiwa unazungumzia viwanda lazima kuwe na njia bora na rahisi za kuingiza malighafi na kutoa bidhaa kwenda kwa wateja wa mwisho kwa haraka. Ukumbuke idadi kubwa ya wacongo wananunua bidhaa za samaki toka Soko la mwaloni ambalo ni moja ya vyanzo vikubwa sana vya mapato mkoa wa Mwanza. Wavuvi wanafanya shughuli zao ziwa Victoria wanategemea soko lao kuu ni Mwanza kuanzia samaki wanaoingia viwandani mpaka wanaoelekea kwa wateja bila kuchakatwa kupia viwanda vikubwa... (Dagaa, Sato na Sangara), wavuvi wa Mkoa wa Geita na maeneo ya Sengerema wanasafirisha samaki kwa boat na Barabara kutegemea Jiografia ya eneo na wengi watatumia Daraja la Busisi ambalo kwanza ni nafuu na haraka kuliko vivuko vya Busisi na Kamanga. Wafanyabiashara wa Congo, Burundi na Rwanda watalitumia kama wanavyotumia sasa kivuko cha Busisi ambacho utalazimika kusubili saa nzima kuvuka upande wa pili wakati daraja utatumia dk 3 tu.
Faida ni nyingi mno kwa wakazi wa Bukoba Sengerema Geita Kigoma na maeneo mengine. Fanya homework yako ndio uje kuhoji umuhimu wa kiuchumi aliuona JPM na kuamua kuweka bilions of money kwenye hilo Daraja
R.I.P jemedali.