Chato: Yaliyojiri katika Maadhimisho ya mwaka 1 wa kifo cha Hayati Magufuli. Kasala, tusimamie ukweli na haki. Samia kuendeleza Mema

Sherehe ya Leo ni kubwa sana hasa tukikumbuka wapendwa wetu waliouwawa na huyu mtu.

Bora alikufa Tena kifo kibaya
 
Kesho unakufa
 
Pengo lake halina spea, serikali yake ilisifika kwa utekelezaji serikali ya sasa hivi inasifika kwa maneno na malalamiko mengi bila utekelezaji.

Wale wenye mimba zako za chuki kwenye vichwa na mawazo yao, waliodai "hamna uhuru wa kujieleza ",baada ya kuingia Mama wakadai sasa hivi kuna uhuru wa kujieleza, cha ajabu.

Pamoja na uhuru wakujieleza.
1.Mgao wa umeme kimya
2.Mgao wa maji kimya.
3.Tozo kimya.
4.Bei ya mafuta imepanda tokea mwaka jana mwishoni, amabayo imegusa bidhaa nyingine kimya.
5.Watu wanajipigia hela plus utendaji na uwajibikaji wa watumishi umepungua kimya.

Unajiuliza sasa uhuru wa kuongea walikuwa wanaudai katika mambo gani, ikiwa mambo yanayo yagusa wananchi hawaongei labda may be aliwabana sana kwenye issues zao za Magendo.

Bahati kwa nature ya kazi yangu nimezunguka sana baadhi ya mikoa,nimeshudia hospitali ulizojenga kila wilaya, mahakama kila wilaya barabara za kisasa,nimeshuhudia majengo mapya ya ofisi za wakuu wa wilaya na wakurugenzi na zaidi nilishuhudia barabara ya km 50 ya zege kuelekea Ludewa.

Pumzika tu ila pengo lako halina spea, vitu ulivyo vifanya vinaonekana huitaji kutumia nguvu.

RIP Chuma John Pombe Magufuli.
 
Nipe tathimini ya kiuchumi ya ilo daraja refu la busisi , au huko linako elekea Kuna resources gani ambayo itainua uchumi wetu, otherwise ni zawadi kwa mkwe wake kama wanavyosema wengi
Kweli unaumri mdogo sana tokea umezaliwa na kuijua hii nchi.... nakumbuka mwaka 1985 ndio niliingia Mwanza mjini nikitokea Dar wakati huo wakazi wake hawakuzidi 200k kifupi tulikuwa tunafahamiana mpaka kwa majina ya utotoni. Mwanza ni mji unaokuwa haraka sana miaka 35 baadae ni jiji lenye wakazi wasiopungua 1.5m (kwa wilaya za Ilemela na Nyamagana).

Mwanza ni jiji lenye viwanda vingi zaidi kwa eneo lote la kanda ya ziwa, jiji lenye soko kubwa la bidhaa za samaki, jiji lenye soko kubwa la bidhaa za kilimo, jiji lenye njia nyingi za usafirishaji kuanzia reli, barabara, anga na maji. Mwanza pia ni jiji lenye biashara kubwa ya madini, ngozi na utalii. Kuhoji faida za daraja la Busisi inanipa mashaka na uwelewa wako wa njia za kukuza uchumi kwenye maeneo.

Ikiwa unazungumzia viwanda lazima kuwe na njia bora na rahisi za kuingiza malighafi na kutoa bidhaa kwenda kwa wateja wa mwisho kwa haraka. Ukumbuke idadi kubwa ya wacongo wananunua bidhaa za samaki toka Soko la mwaloni ambalo ni moja ya vyanzo vikubwa sana vya mapato mkoa wa Mwanza.

Wavuvi wanafanya shughuli zao ziwa Victoria wanategemea soko lao kuu ni Mwanza kuanzia samaki wanaoingia viwandani mpaka wanaoelekea kwa wateja bila kuchakatwa kupia viwanda vikubwa... (Dagaa, Sato na Sangara), wavuvi wa Mkoa wa Geita na maeneo ya Sengerema wanasafirisha samaki kwa boat na Barabara kutegemea Jiografia ya eneo na wengi watatumia Daraja la Busisi ambalo kwanza ni nafuu na haraka kuliko vivuko vya Busisi na Kamanga.

Wafanyabiashara wa Congo, Burundi na Rwanda watalitumia kama wanavyotumia sasa kivuko cha Busisi ambacho utalazimika kusubili saa nzima kuvuka upande wa pili wakati daraja utatumia dk 3 tu.

Faida ni nyingi mno kwa wakazi wa Bukoba Sengerema Geita Kigoma na maeneo mengine. Fanya homework yako ndio uje kuhoji umuhimu wa kiuchumi aliuona JPM na kuamua kuweka bilions of money kwenye hilo Daraja
R.I.P jemedali.
 
Mkuu pole kwa msiba wa JPM

Naomba kuuliza kutoa hukumu kwa kiswahili kuna tija gani wakati kiswahili hakijitoshelezi chenyewe

Tungefanya kwanza tafiti ndipo tuanze kukitumia
 
Kama hakuacha mifumo ya kuibua, kusimamia na kuendeleza hivyo ulivyovitaja basi hakuwa na nia njema!!

Alafu fikiria kwa undani mna over spend kwenye kumbikizi wakati wapo vijana mitaani wenye mahitaji na hawajui hatma yao! Kama alikuwa bora mnavotaka tuamini mngetafuta namna bora ya kumkumbuka!

Mfano mdogo... watu wote muhimu ukumbukwa siku za kuzaliwa kwao na si za kufa!

JPM alale anakostahiki! Mmethibitisha hana umuhimu wowote!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…