Mgombea wa Urais anayetarajiwa kupata ushindi mkubwa Tundu Lissu leo ataitetemesha Chato na viunga vyake katika kampeni zake zilizoivuta Dunia.
Taarifa kutoka ndani ya Team yake ya Kampeni kabla ya kuhutubia mkutano wa Hadhara atautembelea Uwanja wa ndege wa Chato uliozua gumzo nchini kote kutokana na Ujenzi wake.
Tundu Lissu amepata uungwaji mkono mkubwa kutoka Makundi yote ya Jamii hususan Wafanyakazi ambao wanalaani kupitishwa kwa sheria Haramu ya kupora Mafao yao. CCM na serikali yake walipitisha sheria ya kuzuia Mafao ya Wafanyakazi hata Kama ameacha kazi akiwa na miaka 30 haruhusiwi kupewa haki yake ya mafao mpaka afikishe miaka 60.Sheria hii Haramu imelaaniwa na kila mfanyakazi na Tundu Lissu ameapa kuifutilia mbali Mara tu baada ya kuapishwa.
Ingawa Chato ni nyumbani kwa mgombea Urais wa CCM Lakini kwa muda mrefu Chadema imekuwa na uungwaji mkono mkubwa na inao wafuasi wa kutosha.Mmoja wa makamanda mashuhuri wanaotokea Chato ni mwanamama Husna Amri ambaye anajulikana nchi nzima kwa ujasiri wake.
Tunatarajia kuwaletea kila kitakachojiri katika mapokezi na Mkutano wa Kampeni hapa Chato.