Uchaguzi 2020 Chato: Yaliyojiri Mapokezi ya mgombea Urais wa JMT kupitia CHADEMA, Tundu Lissu

Uchaguzi 2020 Chato: Yaliyojiri Mapokezi ya mgombea Urais wa JMT kupitia CHADEMA, Tundu Lissu

Serengeti mbuga kubwa yenye maajabu haina uwanja wa kimataifa licha ya kupokea watalii duniani kote. Serengeti ina ka-airstrip kavumbi iweje chattle pawe na uwanja wa kimataifa wakati hakuna watalii kabisa? Huu ni ufisadi mkubwa!
SERENGETI haukujengwa wa Lami sababu sheria za kimataifa haziruhusu kujenga uwanja wa ndege wa lami ndani ya mbuga

Wa chato uko nje ya mbuga .Mbuga ndio zimeanzishwa uwanja upo sasa ni part two ni kampeni ya kuzitangaza dunia nzima watu waanze kuzitembelea na flight zianze baada ya kupata vibali vya shirika la usafiri wa anga duniani yaani ICAO
 
Hilo ndo swali kuu.Bila kupata majibu ya swali hilo yote yanayofanyika sasa ni kazi bure but let's hope Tume itamtangaza yeyote atakayeshinda.
Siyo ya Mahela na Kaijage, all are hopeless!
 
Hii hesabu feki. Tanzania ni kubwa sana, hakukuwa na sababu ya Lissu kurudi kanda ya ziwa mara ya tatu. Anapoteza muda wake na resources, wasukuma hawezi kuacha kumpa kura mtu wao.
Unajidanganya, Mimi mwenyewe msukuma wa Geita lakini kura atapata za kishindo.

Utawala huu umeumiza wengi wakulima, wafanyabiashara, wavuvi, wafanyakazi na wote hao kura kwa Lisu tu.
Tukutane leo chato
 
Hii hesabu feki. Tanzania ni kubwa sana, hakukuwa na sababu ya Lissu kurudi kanda ya ziwa mara ya tatu. Anapoteza muda wake na resources, wasukuma hawezi kuacha kumpa kura mtu wao.
Nani kakuambia Magufuli ni msukuma au kwa kuwa anaongea Broken Kisukuma ndio unafikiri ni msukuma. Unajua kwa nini hata kabila lake hataki lijulikane.
 
Siyo ya Mahela na Kaijage, all are hopeless!
Tutapiga kura tuone wanaziibaje na tutajua cha kufanya muda ukifika.

Maccm hamtofanikiwa na hizi njama za kukatisha tamaa watz wanaotaka mabadiliko.

Awamu hii ng' ombe atachinjiwa alipoangukia
 
This is a very dangerous move. Tundu Lissu and his followers should be vigilant.
 
Bado haujajibu swali langu je mwananchi wa chato ujenzi wa uwanja wa ndege chato ndio kipaumbele chake? Utamsaidia nini mwananchi wa chato?
Kuna vipaumbele vya nchi na vya mtu binafsi sio vyote lazima viwe vipaumbele vya Chato vingine ni vya kitaifa

Mfano Serengeti kuna uwanja wa ndege lakini si kipau mbele cha wana Serengeti ni cha kitaifa

Mfano kipaumbele cha wana Chato ni Lissu? au CHADEMA?
 
Sijaelewa KAMANDA!! anachomewa nyumba? KAMANDA huwa ni mtu hatari si rahisi hivyo
Lakini kama kawaida yenu Chadema kutengeneza matukio kutafuta kick za kisiasa kila mkiona haziendi mnatumia mioto utasikia ohh ofisi ya Chadema YACHOMWA moto ohh moto moto !!!

Hizo picha zenyewe za moto na kubomelewa mmmmm zinatia shaka
Kwani nyumba basi pagale limeezuliwa na upepo
 
kuna vipaumbele vya nchi na vya mtu binafsi sio vyote lazima viwe vipaumbele vya chato vingine ni vya kitaifa

mfano serengeti kuna uwanja wa ndege lakini si kipau mbele cha wana serengeti ni cha kitaifa

Mfano kipaumbele cha wana Chato ni Lisu? au Chadema?
Kipaumbele gani cha nchi kilielekeza Chato ujengwe uwanja wa ndege? uwe ni mpango wa maendeleo wa miaka 5 au ilani ya CCM 2015-2020?
 
Na labda kukuibia Siri ili ukasirike zaidi Lissu atafungia kampeni Kanda ya Ziwa kwa siku 3 za mwisho
Serengeti mbuga kubwa yenye maajabu haina uwanja wa kimataifa licha ya kupokea watalii duniani kote. Serengeti ina ka-airstrip kavumbi iweje chattle pawe na uwanja wa kimataifa wakati hakuna watalii kabisa? Huu ni ufisadi mkubwa!
Leo unakuja na approach ya kuzungumzia Serengeti ningejua unatoka Kanda gani na mtazamo wako ningeishia kusema tu Uwanja wa Serengeti umepitia Changamoto nyingi Sana zikiwemo mitizamo ya Monopolism basis kwa maana pale Arusha na Kilimanjaro kuwa watalii wa Nchi hii lazima lango kuu lao la kuingia na kutoka ni Mikoa hiyo Miwili.

Siasa za kushambulia Uwanja wa Chato kwa sisi ambao tuko muda mrefu kwenye soko la Utalii tunajua kwani hata Uwanja wa Mwanza kwa Sera za CHADEMA hautakiwi kuwepo watakwambia umezungukwa na Milima ni hatari kwenye usafiri wa anga yapo mengi tu nafiri niwambie tu Jumatano nitakuwa Live Star Tv kuelezea haya mambo kwann Chama cha Mbowe kinapinga maeneo Mengine kuendelezwa na hasa maeneo ya Kanda ya Ziwa na maeneo Mengine, usikose kuwa nami ktk kukufumbua macho Mtanzania mwenzangu kwa haya yanayoendelea ndani ya Chadema.
 
Nahisi watamzuia kutembelea huo uwanja.Na kwakuwa huko ni nyumbani kwa mgombea yule,nina wasiwasi pia anaweza fanyiwa hujuma katika kampeni zake huko lengo kuhakikisha hapati watu au ashindwe kuhutubia.

Ni imani yangu Lissu haendi kufurahia uwanja,bali anaenda kufanya tathimini physically ya huo uwanja kwa kuingilia kilichojengwa (kupata picha ya kilichojengwa) na ulazima wake pamoja na umuhimu wa kujenga uwanja katika eneo hilo.

Ushauri:Tundu Lissu vaa helmet muda wote ukiwa huko Chato na kuwaambia wananchi kila mtu awe mlinzi kwa kumtupia macho alie jirani yake katika mikutano na misafari atayofanya huko Chato.

Lolote linaweza kutokea leo hii, hivyo ni bora kuchukua tahadhari zote zinazowezekana kuchukuliwa.
Sasa mbona kuna. Uzi.humu.Husna.kachomwa moto usiku wa leo
 
Back
Top Bottom