Uchaguzi 2020 Chato: Yaliyojiri Mapokezi ya mgombea Urais wa JMT kupitia CHADEMA, Tundu Lissu

Uko sahihi kabisa na ninafikiri waTz wote wenye akili timamu hakuna anayeweza kushangilia uhuni huu uliofanywa Chato, na kwa hakika ni aibu kwa Magufuli (kama anayo hulka ya aibu).

Lakini pia ninafikiri CCM ya Magufuli, CCM Mpya imetuletea tafsiri mpya za baadhi ya dhana. Mojawapo ni dhana ya 'tusi'. Kwamba kumkosoa au kutokubaliana na hoja au mradi ambao ameamua kuufanya (binadamu tunaweza kuwa ni mitazamo tofauti juu ya jambo) hilo ni tusi. Ni kumtukana Magufuli. Na wewe unaelekea kuangukia huko.

Lissu hajamtukana Magufuli, bali amekuwa akimkosoa waziwazi. Kijiko anakiita kijiko badala ya kukiita sepetu. Na kama mshindani wa Rais anayetetea kiti chake, mkakati wa kumkosoa ni halali kabisa. Na kwenda kijijini kwake Chato ulikuwa ni uamuzi wa busara na akili kubwa - ili kuondoa fikira za kishamba na ulimbukeni kuwa kijiji au wilaya anayotoka Rais basi washindani wake hawaruhusiwi kwenda kupiga kampenu huko!!!

Pia, sidhani kama wanaChato wote wanashangilia ujenzi wa uwanja wa kimataifa kjijini mwao, kwa mfano, wakati watoto wao bado wanakalia matofali, wamerundikana kama maguni katika vyumba vya madarasa, na hawana vyoo, nk. WaTz wa karne ya 21 wana welewa mkubwa kuliko wa 1947. Si wajinga, na yeye Magufuli analifahamu hilo!!!! Kilichofanyika ni ushamba tu.
 
Lissu ulifikiri CHATO ni pa kispotispot ??Nilikuonya tangu asubuhi kuwa makini unavyoingiw CHATO Umeona sasa yaliyokukuta ???

Yaani umepopolewa na mawe ya kutosha shenzitype yaani ulikuwa unatafuta kick CHATO.
Ipo siku utapigwa mawe pia hauna hati miliki ya nchi kijana unajisifia kuanzisha fujo
 
Hii hesabu feki. Tanzania ni kubwa sana, hakukuwa na sababu ya Lissu kurudi kanda ya ziwa mara ya tatu. Anapoteza muda wake na resources, wasukuma hawezi kuacha kumpa kura mtu wao.

Polee
 
Yeye si alisema anaenda kumdharirisha Magufuli Nyumbani kwake na mimi nikasema akifanya hivyo CHATO hatatoka salama na imekuwa hivyo.
Basi kanywe soup mwanafamilia
 

Nonsense
 
Kwenda zenu mlitaka kupata umaarufu CHATO !!


Nilisema hapa asubuhi akienda huko kuongea shombo atapopolewa na mawe na ndivyo ilivyotokea.
Sawa mwanafamilia wa rais unauchungu kweli na mzee
 
Ingekuwa kujaza watu ndo kushinda ni dhahiri Lowasa angakuwa Rais, Mrema angakuwa Rais, Lipumba enzi za ngunguli angekuwa Rais. Tukutane kwenye ballot box tuna hasira na uchungu wa nchi hii. 5 tena.

We nae, CCM haijawahi kushinda urais isipokua Kikwete. Magu hakushinda 2015 kama ambavyo hata shinda mwaka huu. Tume na Polisi ndio wanaoibeba CCM. Ushindani wa kura za wananchi pekee CCM hawashindiii na hata wewe unaijua hio
 
Hilo ndo swali kuu.Bila kupata majibu ya swali hilo yote yanayofanyika sasa ni kazi bure but let's hope Tume itamtangaza yeyote atakayeshinda.

Tume haitamtangaza Lissu kamwe. Tusipofanya maamuzi magumu ya kukataa rais wa Tume basi tujue CCM itatawala milele. It’s now or never. Katiba lazima ibadilishwe
 

Nonsense [emoji706][emoji706][emoji706]
 
Uko sahihi kabisa na ninafikiri waTz wote wenye akili timamu hakuna anayeweza kushangilia uhuni huu uliofanywa Chato, na kwa hakika ni aibu kwa Magufuli (kama anayo hulka ya aibu)...
Hakuna mtu mwenye support ya 100% aijawahi tokea ata nyumbani kwao.

Pili lazima tuelewa binadamu ‘needs and wants’ zetu azilingani kwa ivyo sio Magufuli wala kiongozi yeyote dunia anaweza mfurahisha kila mtu ndani ya jamii. Magufuli yeye anacholenga ni chenye manufaa ya wengi na kuweka mazingira ya kuchochea uchumi.

If anything mkutano wa Lissu Chato umedhihirisha uongo wa CDM kwamba Chato kunapendelewa.

Tatizo la Lissu yeye akosoi sera za Magufuli bali kila kitu including yeye mwenyewe (personal attacks) mara amwite mshamba, sijui anapendelea kwao au anaponda mbuga ya Burigi and everything kuhusu Chato. Halafu uende na kauli hizo Chato surely you are asking for trouble.

Mwisho tuache kumsingizia Magufuli he has nothing to do na kilichotokea hizo ni hisia za baadhi ya watu tu tena sio wanachato wote but that risk was always present, Lissu is also part to blame ata yeye anajua kutokana na kejeli zake kwa Magufuli majukwaani kwenda Chato was a step too far.

Ingelikuwa anatumia muda mwingi kunadi sera zake asingekutana na kilichotokea leo, tatizo lake ni personal attacks na wana Chato wasingeweza vumilia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…