Uchaguzi 2020 Chato: Yaliyojiri Mapokezi ya mgombea Urais wa JMT kupitia CHADEMA, Tundu Lissu

Uchaguzi 2020 Chato: Yaliyojiri Mapokezi ya mgombea Urais wa JMT kupitia CHADEMA, Tundu Lissu

Binafsi si support physical attacks kwa raia wala kiongozi yoyote kwa sababu za siasa.

Baada ya kusema hayo lazima tuelewe Tanzania ni kubwa sana na watu wake wana viji culture vinavyopishana in terms of what they can tolerate kutokana na maeneo yao...
Uko sahihi kabisa na ninafikiri waTz wote wenye akili timamu hakuna anayeweza kushangilia uhuni huu uliofanywa Chato, na kwa hakika ni aibu kwa Magufuli (kama anayo hulka ya aibu).

Lakini pia ninafikiri CCM ya Magufuli, CCM Mpya imetuletea tafsiri mpya za baadhi ya dhana. Mojawapo ni dhana ya 'tusi'. Kwamba kumkosoa au kutokubaliana na hoja au mradi ambao ameamua kuufanya (binadamu tunaweza kuwa ni mitazamo tofauti juu ya jambo) hilo ni tusi. Ni kumtukana Magufuli. Na wewe unaelekea kuangukia huko.

Lissu hajamtukana Magufuli, bali amekuwa akimkosoa waziwazi. Kijiko anakiita kijiko badala ya kukiita sepetu. Na kama mshindani wa Rais anayetetea kiti chake, mkakati wa kumkosoa ni halali kabisa. Na kwenda kijijini kwake Chato ulikuwa ni uamuzi wa busara na akili kubwa - ili kuondoa fikira za kishamba na ulimbukeni kuwa kijiji au wilaya anayotoka Rais basi washindani wake hawaruhusiwi kwenda kupiga kampenu huko!!!

Pia, sidhani kama wanaChato wote wanashangilia ujenzi wa uwanja wa kimataifa kjijini mwao, kwa mfano, wakati watoto wao bado wanakalia matofali, wamerundikana kama maguni katika vyumba vya madarasa, na hawana vyoo, nk. WaTz wa karne ya 21 wana welewa mkubwa kuliko wa 1947. Si wajinga, na yeye Magufuli analifahamu hilo!!!! Kilichofanyika ni ushamba tu.
 
Lissu ulifikiri CHATO ni pa kispotispot ??Nilikuonya tangu asubuhi kuwa makini unavyoingiw CHATO Umeona sasa yaliyokukuta ???

Yaani umepopolewa na mawe ya kutosha shenzitype yaani ulikuwa unatafuta kick CHATO.
Ipo siku utapigwa mawe pia hauna hati miliki ya nchi kijana unajisifia kuanzisha fujo
 
Hairusiwi kimataifa toka mashamba I ya kigaidi Marekani viwanja vyote vya ndege duniani unaenda ukiwa unasafiri au unadindikiza msafiri Huwezi kwenda kutalii sio mbuga ile ndio maana zamani uwanja wa Ndege wa Dar es salaam tulikuwa tukienda kutalii unapanda juu hata harusi tukienda nazo lakini vyote vilipigwa marufuku .Hivyo Huwezi kwenda eti nakuja kutalii sisafiri Wala Nini nakuja tu kutalii

Nonsense
 
Kwenda zenu mlitaka kupata umaarufu CHATO !!


Nilisema hapa asubuhi akienda huko kuongea shombo atapopolewa na mawe na ndivyo ilivyotokea.
Sawa mwanafamilia wa rais unauchungu kweli na mzee
 
Ingekuwa kujaza watu ndo kushinda ni dhahiri Lowasa angakuwa Rais, Mrema angakuwa Rais, Lipumba enzi za ngunguli angekuwa Rais. Tukutane kwenye ballot box tuna hasira na uchungu wa nchi hii. 5 tena.

We nae, CCM haijawahi kushinda urais isipokua Kikwete. Magu hakushinda 2015 kama ambavyo hata shinda mwaka huu. Tume na Polisi ndio wanaoibeba CCM. Ushindani wa kura za wananchi pekee CCM hawashindiii na hata wewe unaijua hio
 
Hilo ndo swali kuu.Bila kupata majibu ya swali hilo yote yanayofanyika sasa ni kazi bure but let's hope Tume itamtangaza yeyote atakayeshinda.

Tume haitamtangaza Lissu kamwe. Tusipofanya maamuzi magumu ya kukataa rais wa Tume basi tujue CCM itatawala milele. It’s now or never. Katiba lazima ibadilishwe
 
Sijaelewa KAMANDA!! anachomewa nyumba? KAMANDA huwa ni mtu hatari si rahisi hivyo.

Lakini kama kawaida yenu Chadema kutengeneza matukio kutafuta kick za kisiasa kila mkiona haziendi mnatumia mioto utasikia ohh ofisi ya Chadema YACHOMWA moto ohh moto moto.

Hizo picha zenyewe za moto na kubomelewa mmmmm zinatia shaka

Nonsense [emoji706][emoji706][emoji706]
 
aende na Butiama amwite walimu muovu aone kama atatoka salama
Walimuita mwitongo kabisa kina madaraka
Ei6HV_VWsAEWjpj.jpeg
 
Uko sahihi kabisa na ninafikiri waTz wote wenye akili timamu hakuna anayeweza kushangilia uhuni huu uliofanywa Chato, na kwa hakika ni aibu kwa Magufuli (kama anayo hulka ya aibu)...
Hakuna mtu mwenye support ya 100% aijawahi tokea ata nyumbani kwao.

Pili lazima tuelewa binadamu ‘needs and wants’ zetu azilingani kwa ivyo sio Magufuli wala kiongozi yeyote dunia anaweza mfurahisha kila mtu ndani ya jamii. Magufuli yeye anacholenga ni chenye manufaa ya wengi na kuweka mazingira ya kuchochea uchumi.

If anything mkutano wa Lissu Chato umedhihirisha uongo wa CDM kwamba Chato kunapendelewa.

Tatizo la Lissu yeye akosoi sera za Magufuli bali kila kitu including yeye mwenyewe (personal attacks) mara amwite mshamba, sijui anapendelea kwao au anaponda mbuga ya Burigi and everything kuhusu Chato. Halafu uende na kauli hizo Chato surely you are asking for trouble.

Mwisho tuache kumsingizia Magufuli he has nothing to do na kilichotokea hizo ni hisia za baadhi ya watu tu tena sio wanachato wote but that risk was always present, Lissu is also part to blame ata yeye anajua kutokana na kejeli zake kwa Magufuli majukwaani kwenda Chato was a step too far.

Ingelikuwa anatumia muda mwingi kunadi sera zake asingekutana na kilichotokea leo, tatizo lake ni personal attacks na wana Chato wasingeweza vumilia.
 
Back
Top Bottom