Kwa miaka 9 mfululizo kampuni ya Yutong ya China imekuwa kinara kwa kuuza mabasi mengi zaidi duniani.
Utengenezaji na uuzaji wa mabasi ya abiria imekuwa biashara kubwa yenye ushindani hasa mabasi ya umeme. Mabasi yamekuwa yakitengenezwa kwa kazi na makusudi tofauti tofauti.
Kinachoangaliwa katika ushindani wa biashara hii ni idadi (units) za mabasi ambazo makampuni katika nchi husika yameuza.
Ifuatayo ni 10 bora ya majina ya makampuni yaliyouza mabasi mengi zaidi duniani mwaka 2022 na idadi ya mabasi yaliyouzwa;
(1)YUTONG (China) – 58,688
View attachment 2679250
(2)DIAMLER (Ujerumani) – 32,612
View attachment 2679307
(3)KING LONG (China) – 26,450
View attachment 2679303
(4)GOLDEN DRAGON (China) – 19,392
View attachment 2679306
(5)MARCOPOLO S.A (Brazil) – 15,831
View attachment 2679298
(6)ZHONGTONG (China) – 15,054
View attachment 2679295
(7)MAN (Ujerumani) – 13,972
View attachment 2679308
(8)HIGER (China) – 11,412
View attachment 2679302
(9)VOLVO (Sweden) – 9,731
View attachment 2679309
(10)SCANIA (Sweden) – 7,777
View attachment 2679310
Katika tatu (3) bora duniani, makampuni matano ya China yameongoza kwa pamoja yaliuza mabasi 130,996, ikifuatiwa na makampuni mawili ya Ujerumani yaliuza jumla ya mabasi 46,584 na Sweden mabasi 17,148
REKODI YA CHINA KATIKA BIASHARA YA MABASI
●Kwa miaka 9 mfululizo kampuni ya Yutong ya China imekuwa kinara kwa kuuza mabasi mengi zaidi duniani.
●China ndilo taifa linalouza karibu asilimia 50 ya mabasi katika soko la dunia.
●China inaongoza kwa kutengeneza mabasi yasiyotumia mafuta (new energy vehicle) Asilimia 90 ya mabasi ya umeme duniani ni yaliyotengenezwa na makampuni ya China.
●Youngman ndilo basi kubwa zaidi lililovunja rekodi duniani lenye urefu wa mita 25 lenye uwezo wa kupakia abiria 300. Lilipewa jina la utani triple bus. Lilitengenezwa na kampuni ya China Youngman Automobile Group Co., Ltd.
View attachment 2679287
●China ndilo taifa pekee duniani lenye viwanda 16 vikubwa vya kutengeneza mabasi; Yutong, Higer, Zhongtong, Kinglong, JMC, Foton, BYD, Golden Dragon, Asia Star, Ankai, Changan, Dongfeng, Nanjing Iveco, Briliance Renault, Sunwin na Sunlong.