Binafsi siioni maajabu general Mabeyo kulia. Watu wanaleta stori za uaskari. Hivi ni wapi mwanajeshi alisomea ukakamavu wa kutolia akiumizwa au kukuguswa na jambo la kusikitisha au kufurahisha. Hapa ndo huwa tunaona watu hasa wa tz wanavyokuwa waoga kutetea haki zao mbele ya askari kwa kudhani askari huyo yeye kaumbwa tofauti na yeye au ana moyo wa chuma. Huyu ni mwanadamu km wewe isipokuwa yeye kaongezewa tu somo la ukakamavu na ujasiri kitu ambacho hata raia kibao tu wanacho hasa wakazi wa mkoa wa Mara, Wamasai nk. Nafikiri hivi karibuni tulishuhudia Wamasai Zanzibar wakiwatia bakora askari wa Zanzibar hadi kukimbia.
Askari nao wana hisia, mzuka, nk. Hakuna mbabe wa hivyo vitu. Ni sawa na kusema general hawezi kuhisi njaa, kitu ambacho siyo kweli, maana hakuna baunsa wa njaa.
Mtu hulia hata kwenye msiba usiomhusu, wakati unaomhusu anaweza kujikaza. Kwa hiyo mazingira huamua hisia za mtu atende nini. Hivyo mtu kulia sababu ya huzuni au furaha husababishwa na factors nyingi, wengine hulia kwa kuvuta kumbukumbu ya matukio ya nyuma yaliyomkuta na kumuumiza, ndo maana mwingine anaweza kulia hadharani sababu ya mapenzi na mwingine asilie. Tena mwingine akavalishwa tu pete akalia tena mbele ya umati wa watu.
So, kulia kwa general publicly is not a big deal, a big deal is why is he crying repeatedly. Alilia siku ya mazishi lakini nashangaa hadi kwenye kumbukizi.