Chozi la Jenerali Mabeyo akisimulia siku za mwisho za Hayati Magufuli linaashiria nini?

Chozi la Jenerali Mabeyo akisimulia siku za mwisho za Hayati Magufuli linaashiria nini?

Ya kutambua:

1. Jenerali Mabeyo ni mzalendo kweli kweli asiyekuwa na chembe ya tamaa ya madaraka.

2. Hapo #1 watu kama hawa ni wa kupigiwa mfano.

3. Kuna watu walionekana kuwa walisahau katiba inasema je, ndiyo maana ikachukua siku mbili tatu hadi kuapishwa badala ya masaa 24 kutokea rais kufariki.

4. Kuwa rais alijua atafariki kiasi cha kumhitaji paroko, kadinali na hata kutaka kurudishwa nyumbani akafie kwao.

5. Kumbe ma Profesa wanaotushauri makulaji walikuwa pale. Ama kweli safari ya pagak ikifika (song of lawino) no way back.

6. Aliyepo anashaurika japo kuna wanao mshauri vibaya lakini baadaye wanakaa wanayaweka mambo sawa.

7. Kwamba, hapa mkuu wasemaje? Kuna hawa wamesema hivi ..:

".. kwani waliosema hivyo ni wanajeshi, raia au wanasiasa ...?"

Pamoja na kustaafu, Jenerali Mabeyo bado ni hazina kubwa kwa taifa hili.
Hakika Jenerali Mabeyo ni hazina kwa taifa. Ni mzalendo wa kweli
 
2. Hata kama madaktari wote wangekuwa ni wanajeshi, huwezi tu ukatoa amri ya kibabe ku override ushauri wa kitaalamu.
Sawa kabisa nakubali, lakini kwenye maelezo ya Jenerali (kama nimemsikiliza vizuri), hakuna mahali ameonyesha kujaribu kuwauliza madaktari juu ya kumruhusu mgonjwa arudishiwe nyumbani! Na wao kusema abaki kwa sababu hii ama Ile!!

Ndiyo maana mwanzo timing ya mahojiano imekosewa cha msingi tuendelee kujadili Mema yaliyotendwa na Hayati Dr. Magufuli kwa nchi hii.

Hata hivyo, naweza kuwa nimekosea pia.
 
Yes ilikuwa interview nzuri sana kwa bahati mbaya sana walioendesha interview hawakuwa na weledi.
Laiti wangalikuwa nao tungejua mambo mengi sana

1. Wakati hali ya Mh Rais ikiwa mbaya kwanini Makamu wa Rais na Waziri mkuu hawakuitwa warudi Dar ?
Kwanini Makamu wa Rais na Waziri mkuu hawakuwepo kusimamia matibabu ya Rais. kwanini walikuwa ziarani?
Ilipofikia mahali Kadinali na Paroko wanaitwa, je, hiyo haikutosha kuwaita viongozi wakuu

2. Kwanini wakuu wa vyombo vya usalama walisimamia jambo hili bila kuwa na support ya Serikali

3. Kwanini Jenerali Mabeyo atafute taratibu ndani ya katiba wakati Mwanasheria mkuu wa serikali yupo?

4. Jenerali Mabeyo ametueleza mambo muhimu sana kuhusu Katiba. Kwamba nchi inaendeshwa bila muongo ndiyo maana kila jambo lilionekana kama ''novelty' na kwamba hakuna anayejua
a. Rais akiwa mahututi nani awepo nani aongoze nini
b. Rais akifariki taratibu gani zifuatwe kutangaza kifo, nani afanye hilo
c. Makamu wa Rais anaapishwaje na vitu kama bendera vinakuwaje

Ukimsikiliza Jenerali ni kama vile tuliongozwa na ''busara' na siyo taratibu ndiyo maana kuna wale waliotaka iwe tofauti kwasababu kulikuwa na mwanya huo. Tunatakiwa tukae chini hili halipaswi kuwa jambo la kubahatisha au kusema 'hatukuwa na experience'' hapana.

JokaKuu
Habari za siku nyingi mkuu
 
Imagine Leo akiulizwa katika hali Ile, why wengine waliendelea kama vile nothing urgent was there?

Kwanini VP hakuambiwa kama msaidizi wa kwanza wa Rais kuhusu hali ya mgonjwa?

Kwakweli hii inezua maswali mengi na pengine wanazidi kutuzulia maswali zaidi kuliko majibu.
Waliamini Makamu labda anahusika
 
Chozi la Mabeyo linaungana na machozi ya maelfu ya watanzania waliolia na wanao endelea kulia kutokana na madhira waliyo yapata wakati ule wa mtu yule.
Kwa uchache tu nawakumbuka watumishi 12 Elfu walio ondolewa kazini kwa kuwa eti walifoji vyeti.
Wengine walikuwa wamefanya kazi zaidi ya miaka 20...!
Alafu eti MUNGU anampa ufunuo wa kifo chake tena anaita na watumishi wa Mungu wampake mafuta ni watu wachache sana wanapata hii bahati ya kufunuliwa kifo chako hadi Mungu akuchague
 
Mtazamo wangu baada ya kuona hii video

Kwanza haikuwa ajabu kwa jiwe kutaka kuzungukwa na wanausalam wakati wa ugonjwa wake, naamini hao ndio ambao alikuwa anawaamini sana ukiangalia na uadui mkubwa aliokuwa nao hapa ndani ya inchi na nje ya inchi

Pili,kuhusu kupewa taarifa kwanza Waziri mkuu kabla ya makamu wa raisi nadhani ni hekima imetumika hapa, mwanamke ni mwanamke tu, namna ya upokeaji wa taarifa kama zile lazima itumike busara kubwa,, kwahiyo wakati mwingine si suala la kufuata utaratibu bali ni kutumia hekima na busara.

Tatu,naungana na wale wote ambao wamesema kuchelewa kuapishwa kwa raisi ndani ya masaa ya 24 ni kutokana na hii ni experience ya Kwanzaa ktk inchi yetu lazima kuna mambo ya kuyaweka sawa na kujadiliana

Jiwe atabakia kuwa Kiongozi wetu bora wa mda wote pamoja na mapungufu ya kibinadamu aliyokuwa nayo.

Ni hayo tu!
Umesahau alikuwa karibu pia na Viongozi wa Dini
Hadi dakika za mwisho anafariki walikuja kumuombea toba
 
Kwa kuunganisha mambo hamjambo
Sijui ni umasikini au kutokua na fikra nzuri bali mbaya tu
Marehemu alikuwa boss wake na mtu aliemuamini sana kuilinda nchi sasa cha ajabu nini kama akitokwa machozi?
 
Mabeyo anasingizia eti two thoughts ndio zilichelewesha kumuaoisha Rais wakati huo huo anasema kikatiba inatakiwa within 24hrs,hivi anajaribu kumfanya nani ni mtoto hapa wa eti huo ndio ulikuwa mjadala? 🤣🤣🤣🤣

Huyu huyu alitoa Kauli ya utata baada ya Mazishi kule Chato.Aache kujikanganya kama sio mzungumzaji mzuri.

Kwanza sio sawa kabisa kuwafahamisha PM na KMK taarifa za kifo Cha Rais kabla ya VP Kwa kisingizio Cha eti VP Yuko ziarani Tanga.

Hapo Kuna maswali mengi kuliko majibu ya ule uvumi.

Kiufupi Mimi ndio ningekuwa Samia ningewafyeka wote waliopindisha utaratibu.
Ungewafyeka kwa kutumia nini,mimi naona huyo Samia ilitakiwa wamfyeke akiwa hukohuko Tanga
 
Angekuwa mtu mwenye tamaaa ya madaraka tu usingekuwa raisi
Sio kirahisi hivyo, muda ule ule JPM anakata roho tayari allegiance ya TISS ilihamia kwa Samia so worst outcome ingekua vita au mauaji mfululizo. Na jeshi sio kama wote wangekubali tu ingegawanyika na ingekua civil war na power struggle.

So akiangalia madhara akaona mambo yasiwe mengi.... kimanyema ningeita deterrent theory yaani unafanya maamuzi A hata kama huyapendi kwa kupima madhara ya maamuzi B.
 
Itakuwa maokoto effect tu either Jiwe alichukua maokoto yake baada ya kugundua ana utajiri wa kutisha hivyo anawaza MAPENE yake yaliyoporwa or baada ya kifo cha JIwe akawekwa Pembeni hivyo masotojo ,marosoroso,madikodiko ,umete umate unakata.
 
Kama kuna watu waliweza kujipenyeza na kumuua, pamoja na ule ulinzi wote basi hao watu wana akili sana.
Ukiona mtu anakuzibia mianya ya kuiba na wewe maisha yako umezoea wizi lazima utumie akili sana ili kumuua yule anaye kuzuia kuiba na ukumbuke tayali ulishakuwa na watu wako kwenye systems na kumbuka pesa inatoa roho lakini hairudishi roho
 
Naona zitto kabwe ulifurahi sana
Hakuna anayefurahia kifo hata mimi nitakufa muda ukifika ila siwezi singizia sijui nimewindwa sijui maadui.

Sasa JPM alikua anasema chanjo ni mbaya cha ajabu alitumia betri kuendesha moyo kutoka kwa hao hao mabeberu!! Kama sio unafiki ni nini?

Sasa siku betri imepata hitilafu inahusiama nini na kuuwawa? Angekua hana ugonjwa hapo sawa ila mtu anaumwa miaka 15+ akifariki nini cha ajabu?
 
Sio kirahisi hivyo, muda ule ule JPM anakata roho tayari allegiance ya TISS ilihamia kwa Samia so worst outcome ingekua vita au mauaji mfululizo. Na jeshi sio kama wote wangekubali tu ingegawanyika na ingekua civil war na power struggle.

So akiangalia madhara akaona mambo yasiwe mengi.... kimanyema ningeita deterrent theory yaani unafanya maamuzi A hata kama huyapendi kwa kupima madhara ya maamuzi B.
Bora umemkumbusha watu wasahaulifu kweli.

Wamesahau Samia siku anapokea ripoti ya CAG alisema anaomba ripoti ya miamala ya BoT iliyofanyika January hadi March.( behind the scene hii ilikuwa ni decoy) dakika za mwisho mwisho za Jiwe ilionekana kuna pesa ndefu iliidhinishwa BoT kwa shughuli maalum katika ofisi ya Jiwe ila haikujulikana zimeenda wapi ila kwa makusudio ilikua ni "kuhonga" wakuu wa vitengo mbali mbali ili Mama Abdul awekwe kando.

Pili kuna siku huyu huyu ex CDF mwanzoni mwa utawala wa Samia alisema kwenye hadhara " Mh rais nina jambo la kuongea ila naomba nitakuona ofisini"

Ukiunganisha hizo statement 2 utajua nini kilikuwa kinaendelea.
 
Back
Top Bottom