Chozi la Jenerali Mabeyo akisimulia siku za mwisho za Hayati Magufuli linaashiria nini?

Chozi la Jenerali Mabeyo akisimulia siku za mwisho za Hayati Magufuli linaashiria nini?

Hujui sheria za jeshi kaa kimya

Kwa kawaida, sheria za jeshi huwa na masharti maalum kuhusu umri wa kustaafu. Hata hivyo, kuna hali ambapo jeshi linaweza kuongeza muda wa utumishi kwa wanajeshi baada ya kufika umri wa kustaafu kutegemea na mahitaji ya kimkakati au sera za kijeshi za nchi. Hii mara nyingi hufanyika kwa kuzingatia uwezo na uzoefu wa wanajeshi walio katika huduma.

..wakati mwingine " masharti maalum " ni upenyo waliopewa watawala kukiuka sheria.

..masharti / mazingira maalum yaliyopelekea Jiwe kuteua mstaafu ni yapi? Unaweza kutudokeza?
 
Kwa hiyo kama ilivyosemekana akina Bashiru na yule jamaa wa Tiss walitaka kusigina Katiba waweke wamtakaye.
 
Hakika suala la kifo ni fumbo sana sana sana sana

Ukibahatika kufa mbele za watu Mwombe Mungu

Leo hii tumepata simulizi nzuri ya EX CDF kumbe magufuli wakati anakufa hakuwa mikononi mwa mtoto wake,Mkewe wala ndugu yoyote ili ni kwa sababu ya cheo chake lakini hata mke hakurusiwa kuwa pale kumuuguzia mumewe?

Wewe ulie na ndoa kumbe usiringe yawezekana siku unakufa hata mkeo hatokuwa karibu na wewe wala watoto ulio wazaa

Aise
Bora maisha ya upadri[emoji3][emoji1787][emoji16][emoji23] fundisho kubwa

Simulizi ya CDF ipo wazi

Magufuli alipata nafasi ya kutubu dhambi zake zake kupitia Baba paroko na Kadinari pengo ili ni daraja la pekee sana sio wote ulipata

Magufuli alitaka akafie nyumbani kwake bira shaka hakupendezwa kuuguzwa paspo mkewe kuwa pale au watoto wake

Magufuli alitaka kujiua kwa kutaka kutolewa hosptali akafie kwake hii ni roho ya mauti uwa inamsumbua kila mmoja anae karbia kufariki uwa anachaguo lake.

Mwisho kwa uhakika

Magufuli kwa simulizi ya ex cdf yupo mbinguni

Je mlio kuwa karibu na Nyerere,Mkapa na Mwinyi Nini kilijili ili sisi tujipange kukutana nao either mbinguni hama motoni?
Mkuu umeandika kwa hisia sana.
 
Hivi kweli unaona ni sahihi mtu kufoji cheti Ili apate ajira na baada ya kubainika na kuthibitishwa kuwa amefoji aachwe aendelee na kazi? Mimi nina mashaka na uwezo wako wa kufikiria
Alikuwa bias. Mbona alimuacha makonda aendelee licha ya kufoji vyeti na majina makonda aliua, hakuwa analipa kodi na ushuru alikuwa anatumia madaraka yake vibaya. Licha ya kuwafukuza wenye vyeti feki ilileta tija gani? Kupitia yeye Jiwe kulikuwa na upotevu wa matrillion.
 
Ukimsikiliza Jenerali ni kama vile tuliongozwa na ''busara' na siyo taratibu ndiyo maana kuna wale waliotaka iwe tofauti kwasababu kulikuwa na mwanya huo.
Binafsi nimeshangazwa na timing ya interview ya Jenerali, why now?? Na si wakati ule ama wakati ujao?

Kwa nini hasa.

Nikija kwenye hoja "busara" ilitumika badala ya taratibu za kikatiba kama kumuapisha baada ya 24 hours... Maswali yanaongezeka.

Ndiyo maana nikashauri tujikite kwenye mema tu aliofanya Hayati Magufuli (R I.P) kwenye mjadala. Pia tujikite kumshauri Mama Dr. Samia katika kutimiza wajibu wake kwa kuwa ni Rais wetu sasa, Maana tumeambiwa na Jenerali kuwa Rais anapenda sana kushirikisha watu kwenye kazi zake.
 
Kwa kauli yake ‘anadhani kuna wakati washauri wake wanampa ushauri mmbaya’ (hiyo ni cue tosha), juu ya mtazamo wake wa siasa za sasa. Sema kamalizia na diplomatic language tu anashirikisha watu wengi kwenye maamuzi yake na anafanya kazi nzuri.

Tukumbuke kwa sasa general ni mstaafu na wala awezi kuwa na open opinion kuhusu siasa ata angekuwa bado CDF leo; na akuwa na upande kwenye interview yake.

Lile chozi akielezea siku za mwisho za marehemu ndio limenishangaza kuna kitu emotionally kinamsumbua na kile kifo.

Ni swali tu sijahitimisha sababu itakuwa nini ukizingatia ni ngumu sana watu wa level yake kuonyesha public emotions.
Wasije wakamuona liability tu wakamuwahisha na yeye ohoooo
 
Sasa cha kushangaza Mabeyo pamoja na kujitahidi kutabasamu ila chozi lilimshinda nguvu kwa sekundę kadhaa ameonekana akibubijikwa machozi ya hudhuni mbele ya camera. Kumbuka ata alipofiwa na mtoto wake rubani, general akutoa chozi alipofika eneo la tukio.

Je anajutia kutosikiliza maamuzi ya watu waliomshauri wapindue męża ya katiba huyo mama hiyo nafasi sio size yake na kinachoendelea leo Tanzania.
Daily news!!

Hawajampangia cha kusema hawa!!
 
Kwa kauli yake ‘anadhani kuna wakati washauri wake wanampa ushauri mmbaya’ (hiyo ni cue tosha), juu ya mtazamo wake wa siasa za sasa. Sema kamalizia na diplomatic language tu anashirikisha watu wengi kwenye maamuzi yake na anafanya kazi nzuri.

Tukumbuke kwa sasa general ni mstaafu na wala awezi kuwa na open opinion kuhusu siasa ata angekuwa bado CDF leo; na akuwa na upande kwenye interview yake.

Lile chozi akielezea siku za mwisho za marehemu ndio limenishangaza kuna kitu emotionally kinamsumbua na kile kifo.

Ni swali tu sijahitimisha sababu itakuwa nini ukizingatia ni ngumu sana watu wa level yake kuonyesha public emotions.
Mkuu kama umewahi kushuhudia hatua za mwisho za mtu unaemfahamu huwa sometimes huwa kanakuja ka-feeling flani hivi kakiambatana na machozi kulengalenga. Mgonjwa umemwacha umemwacha muda flani na ukapiga nae story alafu baadae unakuja kumwangalia hajitambui na ana struggle kitandani acha kabisa
 
Watanzania gani, maana Mimi ni mtanzania na Wala sitaki kujua Nini kilitokea maana naona amani imerejea nchini.

In the whole world, hakuna anayekubaliana na mambo yote. Hata JPM, kuna waliompinga na waliomkataa.
Wamekataliwa mitume na manabii...
Naposema watanzania namaanisha mimi na wengine waliomkubali.
Sio lazima na wewe uwemo kwenye kundi na haijalishi. Kipendacho roho....
 
Basi tatizo siyo kukosa uzoefu, bali kukosa weledi.

Nakuhakikishia hata tungekuwa na uzoefu kuliko Marekani, hali ingekuwa ileile.

Angalia mfano wa majanga: kuzama kwa meli, ndege kuanguka, ukame, njaa na majanga mengine ya asili kama mafuriko na matetemeko.

Tumejifunza kitu chochote kama taifa au kila tukio linatushtukiza sie ni kama wageni?

Nimesema kama mpaka wale walio juu wanaganga njaa, hawaheshimu hata viapo walivyoapa. Hawana ethics za kazi....what else has remained?

Tusijifananishe na Marekani. Hii njaa yetu ni ya next level 🤣🤣🤣🤣
 
Unaujinga ulichoandika ni kwamba Mabeyo amedanganya
Nimekuuliza na swala la Magufuli kuita viongozi wa dini nalo kadanganya
Jibu swali acha kuzunguka zunguka kama chizi anaetafuta mkate jalalani

Wengine wanapeana hadithi wakiwa na supu ya pweza, gahawa na kadhalika.
Wakimaliza hapo ni kula ubwawa rundo kubwa
 
Yes ilikuwa interview nzuri sana kwa bahati mbaya sana walioendesha interview hawakuwa na weledi.
Laiti wangalikuwa nao tungejua mambo mengi sana

1. Wakati hali ya Mh Rais ikiwa mbaya kwanini Makamu wa Rais na Waziri mkuu hawakuitwa warudi Dar ?
Kwanini Makamu wa Rais na Waziri mkuu hawakuwepo kusimamia matibabu ya Rais. kwanini walikuwa ziarani?
Ilipofikia mahali Kadinali na Paroko wanaitwa, je, hiyo haikutosha kuwaita viongozi wakuu

2. Kwanini wakuu wa vyombo vya usalama walisimamia jambo hili bila kuwa na support ya Serikali

3. Kwanini Jenerali Mabeyo atafute taratibu ndani ya katiba wakati Mwanasheria mkuu wa serikali yupo?

4. Jenerali Mabeyo ametueleza mambo muhimu sana kuhusu Katiba. Kwamba nchi inaendeshwa bila muongo ndiyo maana kila jambo lilionekana kama ''novelty' na kwamba hakuna anayejua
a. Rais akiwa mahututi nani awepo nani aongoze nini
b. Rais akifariki taratibu gani zifuatwe kutangaza kifo, nani afanye hilo
c. Makamu wa Rais anaapishwaje na vitu kama bendera vinakuwaje

Ukimsikiliza Jenerali ni kama vile tuliongozwa na ''busara' na siyo taratibu ndiyo maana kuna wale waliotaka iwe tofauti kwasababu kulikuwa na mwanya huo. Tunatakiwa tukae chini hili halipaswi kuwa jambo la kubahatisha au kusema 'hatukuwa na experience'' hapana.

JokaKuu
Experience is the best teacher! Now we have it.

Tutaona huko mbeleni itavyokuwa likija kutokea tukio jingine kama hilo.

NB: umehoji kwa nini makamu wa Rais na waziri mkuu hawakuwepo kusimamia matibabu ya Rais?

Are you serious? Yaani waache kazi za nchi waende wote spitalini kusimamia matibabu ya Rais?

Ulitaka wawepo kwenye chumba cha matibabu wakishuhudia Rais anapodungwa sindano, anapopimwa presha, n.k.?
 
Back
Top Bottom