Chozi la Jenerali Mabeyo akisimulia siku za mwisho za Hayati Magufuli linaashiria nini?

Chozi la Jenerali Mabeyo akisimulia siku za mwisho za Hayati Magufuli linaashiria nini?

Kuna watu mlikuwa mnaona ni bora katiba ipindishwe ili mama asiwe mrithi wa Jpm!! Watanzania tumelogwa na Nani?

CCM wakati wanafanya vetting ya makamo wa raisi hawakuwahi kufikiri Kuna dharula za vifo ambazo zinampa nafasi makamo wa raisi kuwa raisi kamili?
Katiba iliwatenda vibaya sana..
Na bado, mpaka 2030..
Twafwaaa
 
Tuambie wewe nani alipaswa kuwa Mkuu wa Majeshi? Maana Mabeyo wakati JPM anaingia tayari alikuwa ni moja ya makamanda wa ngazi ya juu kabisa jeshini wala si kwa kubebwa na Magufuli!
Mabeyo kabla hata ya JPM alishakuwa Chief of Intiligency,Kwa hiyo usimchukulie poa kwanza pia jamaa anaonekana ni smart sana angalia hata uongeaji wake na mtu wa msimamo
 
Experience is the best teacher! Now we have it.
Ni Gen Mabeyo kaamua kusema tu kilichojiri vinginevyo tusingekuwa na hiyo experience
Tunahitaji kuwa na record na haya mambo yaongozwe si kutumia busara.
Tutaona huko mbeleni itavyokuwa likija kutokea tukio jingine kama hilo.

NB: umehoji kwa nini makamu wa Rais na waziri mkuu hawakuwepo kusimamia matibabu ya Rais?

Are you serious? Yaani waache kazi za nchi waende wote spitalini kusimamia matibabu ya Rais?

Ulitaka wawepo kwenye chumba cha matibabu wakishuhudia Rais anapodungwa sindano, anapopimwa presha, n.k.?
Yes kwasababu Rais alikuwa mgonjwa Hospiali tena mahututi.

Makamu wa Rais alitakiwa awe karibu ili kuchukua majukumu ingalitokea vinginevyo, ni kwa mujibu wa Katiba ya JMT 1977 Sura ya Pili 37(2)(3)
It's unconscionable kwamba Rais yu mahututi anapewa sakremento na Makamu wa Rais hayupo around.

Kwa maneno mengine maamuzi ya nchi yalifanywa na watu watatu, CDF , IGP na DGIS.
Wakati wanahangaika Makamu wa Rais yupo Tanga katika mkutano wa hadhara ! huo si uendeshaji nchi

Waziri Mkuu ndiye mtendaji wa Serikali, naye pia alitakiwa awe karibu si kwasababu Rais anaumwa, bali Rais yu mahututi na lolote linaweza kutokea! na lilitokea kwa mujibu wa Mabeyo

CDF, DGIS na IGP ni Washauri wa Usalama si waendeshaji wa serikali wakati Makamu na Waziri mkuu wanaendesha mikutano. Mikutano haina tija kwa wakati uliokuwepo.

Hoja si Rais Kuumwa, hoja ni Rais kuwa Mahututi na sote tulijua! ilishangaza viongozi wanahutubia mikutano na wengine kusema ''yupo anachapa kazi''.
 
Hivi kweli unaona ni sahihi mtu kufoji cheti Ili apate ajira na baada ya kubainika na kuthibitishwa kuwa amefoji aachwe aendelee na kazi? Mimi nina mashaka na uwezo wako wa kufikiria
Kama ambavyo na mimi nina mashaka na uwezo wako finyu wa kifikiri na kuiljigeuza kuwa shabiki usie na hoja.
Nani anaajiri, anatumia vigezo gani? Umemuajiri mtu ametumika miaka 20, 25, 30 ndio unabaini kuwa alifoji cheti, tena ni cheti cha kidato cha nne.
Mtu huyo huyo ni daktari bingwa, mhandisi au mwalimu mwandamizi; kwa kuwa tu analifoji cheti cha kidato cha nne unamuondoa kazini? Ni zaidi ya ujinga.
 
Kweli….si umemsikia hata Jenerali Mabeyo kasema kuwa Rais Magufuli alimwambia [CDF] awaamuru madaktari wamrudishe nyumbani lakini akasema hana mamlaka hayo.

Magufuli akashangaa kwa nini CDF hawezi kuwaamuru hao madaktari wamrudishe nyumbani. Jenerali akasema hilo ni suala la madaktari na siyo CDF.

Magufuli alikuwa anadhani kwa vile Mabeyo ni CDF, basi anaweza kutoa amri kwa yeyote yule na ikatekelezwa.

Kwa kuangalia tu juu juu, Mabeyo anaonekana kama ni mtu mwenye sense.

At least that’s how he came across in the interview.
Angerudishwa kwao angepona..
 
Wewe nawe Kumbe hamna kitu, wenyeviti na wajumbe wa Bodi hawana mishahara. Hupata pesa kama kiinua mgongo Fulani kila baada ya miaka mitatu ambao ndiyo muda wa Bodi kuwapo madarakani. Na wengine huigawa Kwa tatu Ili kila mwaka wapate chochote. zaidi ya hapo ni posho ya vikao.
Hakuna sehemu ‘non executive directors’ (NED) hawana mshahara na marupurupu kwa hizo part time job.

Tafuta financial report ya NCAA uone fixed remuneration wanazopokea NED kila mwaka.
 
Sio kirahisi hivyo, muda ule ule JPM anakata roho tayari allegiance ya TISS ilihamia kwa Samia so worst outcome ingekua vita au mauaji mfululizo. Na jeshi sio kama wote wangekubali tu ingegawanyika na ingekua civil war na power struggle.

So akiangalia madhara akaona mambo yasiwe mengi.... kimanyema ningeita deterrent theory yaani unafanya maamuzi A hata kama huyapendi kwa kupima madhara ya maamuzi B.
Usalama wa taifa unafananisha na jeshi
 
Binafsi nimeshangazwa na timing ya interview ya Jenerali, why now?? Na si wakati ule ama wakati ujao?
Kwa nini hasa.
Jenerali Mabeyo amepita katika mtihani mgumu, yaani anastahili heshima zetu
Mabeyo anatahadharisha matatizo katika mifumo na ikiwa watatokea 'wahuni' na walikuwepo nchi itakuwa katika matatizo.

Ni kwavile tu walioendesha mahojiano hawakuwa na weledi, Jenerali alikuwa tayari kufunguka sana.
Ametuonyesha kwamba AG (Mwanasheria Mkuu) hana kazi, VP na PM wanavyo kuwa 'sidelined' na Wahuni

Nikija kwenye hoja "busara" ilitumika badala ya taratibu za kikatiba kama kumuapisha baada ya 24 hours... Maswali yanaongezeka.
Mambo mengi yalitumia busara badala ya taratibu na miongozo.
Kuna tatizo la kutotengeneza mifumo yetu halafu tukaifanyia 'test' kabla ya madhara.

Tulitakiwa tuwe na 'structure' kivitendo. Namshukuru Gen Mabeyo! Wahuni wangetuvuruga sana!
Ndiyo maana nikashauri tujikite kwenye mema tu aliofanya Hayati Magufuli (R I.P) kwenye mjadala. Pia tujikite kumshauri Mama Dr. Samia katika kutimiza wajibu wake kwa kuwa ni Rais wetu sasa, Maana tumeambiwa na Jenerali kuwa Rais anapenda sana kushirikisha watu kwenye kazi zake.

Al marhumu Mzee Mwinyi alisema '' baada ya kifo ni hadithi, hivyo tujitahidi hadhithi ziwe nzuri''

Kwa Magufuli huwezi kuandika legacy yake kwa kuchagua!
Kwa bahati mbaya kama hutaandika mabaya na maouvu yake hutamtendea haki.

Jenerali Mabeyo anatueleza PM alivyokuwa hajui taratibu na kudhani CDF ana amri kwa Daktari.
Hili si geni ndivyo alivyokuwa. JPM hakuwa mtu wa kuheshimu taratibu achilia mbali kuzifuata

Matatizo aliyoeleza Jen Mabeyo ni zao la kuvunja taratibu .
JPM alikuwa na genge lililotaka kutumia njia za mkato kama alivyoliingiza madarakani.

Kundi hilo ndilo lililokuwa linampiga vita SSH na linajulikana
Kundi lina Prof na Wasomi. Ukimsikiliza Mabeyo anasema '' tulirudi kwenye katiba''

Si kwamba Mabeyo hakujua Katiba inasema nini, alichokisema kwa fasihi ni kwamba '' Tulitumia Katiba' kudhibiti matakwa ya genge alilounda JPM.

JPM ametuachia nyufa kubwa ikiwa ni pamoja na kutoheshimu ubinadamu, kujenga ukanda na ukabila n.k.
Aliposimama kuagiza mtu atwange risasi alikuwa katika rekodi leo unataka watu wasiseme!!

JPM pamoja na ukatili na mbaya mengi alitusaidia kujua hii Katiba inategemea heshima, madili na utu wa mtu .
Katiba ina matundu na alituonyesha ilivyo mbaya, isivyoweza kujitetea au kutetewa chini ya mikono miovu
 
Nadharia na uhalisia ni vitu tofauti sana.

Kujifunza toka kwa wengine ni nadharia tu. Tukio likikutokea wewe, huo ni uhalisia.

Na dynamics za wengine, haziwezi kufanana na za kwako.

Safari ijayo likitokea tena, unataka tuige Wamarekani wanafanyaje au tufanye vile itufaavyo kutokana na uzoefu wetu kwa kutumia taratibu zetu?
MV Bukoba ilipozama, tukadhani tumejifunza.

Ila kila ajali na janga linapotutokea, tunakuwa kama wageni wa tukio husika.

Au labda ni hadi majanga na misiba mingapi ndipo tunakuwa na umahiri wa kuikabili kwa weledi?

Unajitahidi sana bila mafanikio kuutetea ujinga.
 
Ni Gen Mabeyo kaamua kusema tu kilichojiri vinginevyo tusingekuwa na hiyo experience
Tunahitaji kuwa na record na haya mambo yaongozwe si kutumia busara.
Na ndo maana nampa pongezi zake.

Ila yeye ni mtu mmoja tu na kafunguka kupitia kile alichokiona yeye.

Usishangae wengine waliokuwepo nao kuwa na version tofauti ya tukio lilivyojiri.

Licha ya hivyo, kudos kwake.
Yes kwasababu Rais alikuwa mgonjwa Hospiali tena mahututi.

Makamu wa Rais alitakiwa awe karibu ili kuchukua majukumu ingalitokea vinginevyo, ni kwa mujibu wa Katiba ya JMT 1977 Sura ya Pili 37(2)(3)
It's unconscionable kwamba Rais yu mahututi anapewa sakremento na Makamu wa Rais hayupo around.

Kwa maneno mengine maamuzi ya nchi yalifanywa na watu watatu, CDF , IGP na DGIS.
Wakati wanahangaika Makamu wa Rais yupo Tanga katika mkutano wa hadhara ! huo si uendeshaji nchi

Waziri Mkuu ndiye mtendaji wa Serikali, naye pia alitakiwa awe karibu si kwasababu Rais anaumwa, bali Rais yu mahututi na lolote linaweza kutokea! na lilitokea kwa mujibu wa Mabeyo

CDF, DGIS na IGP ni Washauri wa Usalama si waendeshaji wa serikali wakati Makamu na Waziri mkuu wanaendesha mikutano. Mikutano haina tija kwa wakati uliokuwepo.

Hoja si Rais Kuumwa, hoja ni Rais kuwa Mahututi na sote tulijua! ilishangaza viongozi wanahutubia mikutano na wengine kusema ''yupo anachapa kazi''.
Tatizo letu, au kwa usahihi niseme tatizo la CCM ni kuongoza/ kutawala kwa kutumia mazoea zaidi na si kwa taratibu kwa mujibu wa sheria.

Laiti katiba iliyopo [hata kama ni mbaya] ingefuatwa kwa jinsi inavyotoa mwongozo, wala kusingekuwepo na sintofahamu iliyokuwepo.

It’s not that complicated.

CCM wamejenga utamaduni mbaya wa kutokufuata katiba na kutokuiheshimu katiba.

Hili ni suala la kiutamaduni wa CCM. Ni utamaduni mbaya sana unaoruhusu mtu hata kuvunja katiba waziwazi kabisa na hakuna mtu hata mmoja kutoka kwenye chama chao au serikali yao anayesema hapana.

Kama kuna lawama au kuna aliyekosea, mlaumiwa au mkosaji huyo ni CCM na viongozi wake wote maana hakuna hata mmoja wao aliyejaribu kuondokana na huo utamaduni.
 
MV Bukoba ilipozama, tukadhani tumejifunza.

Ila kila ajali na janga linapotutokea, tunakuwa kama wageni wa tukio husika.

Au labda ni hadi majanga na misiba mingapi ndipo tunakuwa na umahiri wa kuikabili kwa weledi?

Unajitahidi sana bila mafanikio kuutetea ujinga.
Haya, sawa. Uko sahihi.

Igeni kutoka Marekani.
 
Ukipata bahati ya MUNGU Kukufunulia kifo chako jua wewe MUNGU amekuchagua hiyo nafasi wanapata wachache sana 😢
Bahati ni kufunuliwa kuhusu kifo, au kujua kwamba Mungu amekupa rehema?

Ukijua kifo chako, ndiyo nini sasa? Kwani wee hujui utakufa?

Unachezea rehema ya Mungu sasa, halafu???
 
Na ndo maana nampa pongezi zake.Ila yeye ni mtu mmoja tu na kafunguka kupitia kile alichokiona yeye.
Usishangae wengine waliokuwepo nao kuwa na version tofauti ya tukio lilivyojiri.
Licha ya hivyo, kudos kwake.
Huyu Mabeyo siyo tu kwamba ni Jenerali wa Jeshi vitani lakini ni Jenerali aliyevusha Taifa wakati mgumu.
Naamini version yake kwasababu
1. Ana uthubutu wa kutueleza habari ambazo angeweza kukaa nazo moyoni. Mwenyekiti wa baraza la usalama hawajibiki kwetu.
2. Hii si mara ya kwanza, kuna siku alimwambia Rais SSH, ''...mengine tutaongea Ofisini''
3. Busara zake zilishinda ''Wahuni' waliotaka kupindua meza. Yeye alisimama na Katiba hii mbovu kama ilivyo.
4. Aliposema kuna ''school of thoughts' kuhusu bendera alimaanisha Wahuni walitaka Rais asiwe na mamlaka kamili. Yeye (tena ukiangalia uso wake) anaonyesha msisitizo, '' bila bendera Jeshi halitamtambua''

Kuna za kimbea 'chini chini kwamba Wahuni walitaka hata kifo kisitangazwe mapema. Uzushi huo unasema baraza la akina 'Mabeyo' likawaweleza Wahuni, kama hamtamtangaza hadi saa 6 tutamtangaza Rais wetu, Wahuni wakanywea ndiyo sababu ya kutangazwa 5 Usiku.
Tatizo letu, au kwa usahihi niseme tatizo la CCM ni kuongoza/ kutawala kwa kutumia mazoea zaidi na si kwa taratibu kwa mujibu wa sheria.

Laiti katiba iliyopo [hata kama ni mbaya] ingefuatwa kwa jinsi inavyotoa mwongozo, wala kusingekuwepo na sintofahamu iliyokuwepo.

It’s not that complicated.

CCM wamejenga utamaduni mbaya wa kutokufuata katiba na kutokuiheshimu katiba.

Hili ni suala la kiutamaduni wa CCM. Ni utamaduni mbaya sana unaoruhusu mtu hata kuvunja katiba waziwazi kabisa na hakuna mtu hata mmoja kutoka kwenye chama chao au serikali yao anayesema hapana.

Kama kuna lawama au kuna aliyekosea, mlaumiwa au mkosaji huyo ni CCM na viongozi wake wote maana hakuna hata mmoja wao aliyejaribu kuondokana na huo utamaduni.
Exactly!!!
 
Habari za mda huu wapwa, kwa mliobahatika kuangalia video ya cdf mabeyo anaelezea dakika za mwisho za magufuli kuna sehem alisema kwamba "Magufuli alimwita na kumwambia mm siwezi kupona niitieni kadinali pengo"

swali langu ni, Mtu anakua anapitia hali gan mpaka anasema maneno kama haya, kwa hadhi ya magufuli bila shaka alikua na madaktari bingwa wengi, ni nini kinamfanya achukue kusmama upande wa kwamba hatapona ilihali anapatikwa huduma standard kabisa, nlitegemea labda awe upande wa imani kwamba ipo sku ntapona ata kama itachukua mda
 
Nadhani hali ya kufa kufa ilikua imeshamjaa..namuonea tu huruma Mamake mzazi.jamani😭..sijui anaendeleaje!
 
Haya mambo yako kimkakati Sana unaweza kukuta CDF bado ni Mabeyo, na IGP bado bado ni Siro, na DGISS bado ni Diwani Athumani walitoka kimkakati kwenye Macho ya nje lkn kiutendaji bado ni wao, 2025 utashangaa nahodha msaidizi anawekwa pembeni kupisha nahodha mwenye ujuzi baada ya nahodha msaidizi kuifikisha meli ng'ambo kwa mawimbi makali kabisa
 
Back
Top Bottom