ki2c
JF-Expert Member
- Jan 17, 2016
- 7,719
- 14,506
Mama alilia sana kipindi cha msiba.Umewahi ona mama akitoa lengelenge? Au hakuwa mtu wake wa karibu?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mama alilia sana kipindi cha msiba.Umewahi ona mama akitoa lengelenge? Au hakuwa mtu wake wa karibu?
Katiba iliwatenda vibaya sana..Kuna watu mlikuwa mnaona ni bora katiba ipindishwe ili mama asiwe mrithi wa Jpm!! Watanzania tumelogwa na Nani?
CCM wakati wanafanya vetting ya makamo wa raisi hawakuwahi kufikiri Kuna dharula za vifo ambazo zinampa nafasi makamo wa raisi kuwa raisi kamili?
Mabeyo kabla hata ya JPM alishakuwa Chief of Intiligency,Kwa hiyo usimchukulie poa kwanza pia jamaa anaonekana ni smart sana angalia hata uongeaji wake na mtu wa msimamoTuambie wewe nani alipaswa kuwa Mkuu wa Majeshi? Maana Mabeyo wakati JPM anaingia tayari alikuwa ni moja ya makamanda wa ngazi ya juu kabisa jeshini wala si kwa kubebwa na Magufuli!
Ni Gen Mabeyo kaamua kusema tu kilichojiri vinginevyo tusingekuwa na hiyo experienceExperience is the best teacher! Now we have it.
Yes kwasababu Rais alikuwa mgonjwa Hospiali tena mahututi.Tutaona huko mbeleni itavyokuwa likija kutokea tukio jingine kama hilo.
NB: umehoji kwa nini makamu wa Rais na waziri mkuu hawakuwepo kusimamia matibabu ya Rais?
Are you serious? Yaani waache kazi za nchi waende wote spitalini kusimamia matibabu ya Rais?
Ulitaka wawepo kwenye chumba cha matibabu wakishuhudia Rais anapodungwa sindano, anapopimwa presha, n.k.?
Kama ambavyo na mimi nina mashaka na uwezo wako finyu wa kifikiri na kuiljigeuza kuwa shabiki usie na hoja.Hivi kweli unaona ni sahihi mtu kufoji cheti Ili apate ajira na baada ya kubainika na kuthibitishwa kuwa amefoji aachwe aendelee na kazi? Mimi nina mashaka na uwezo wako wa kufikiria
Angerudishwa kwao angepona..Kweli….si umemsikia hata Jenerali Mabeyo kasema kuwa Rais Magufuli alimwambia [CDF] awaamuru madaktari wamrudishe nyumbani lakini akasema hana mamlaka hayo.
Magufuli akashangaa kwa nini CDF hawezi kuwaamuru hao madaktari wamrudishe nyumbani. Jenerali akasema hilo ni suala la madaktari na siyo CDF.
Magufuli alikuwa anadhani kwa vile Mabeyo ni CDF, basi anaweza kutoa amri kwa yeyote yule na ikatekelezwa.
Kwa kuangalia tu juu juu, Mabeyo anaonekana kama ni mtu mwenye sense.
At least that’s how he came across in the interview.
Kabla ya Mzena sijui alikuwa anatibiwa hospitali gani!Angerudishwa kwao angepona..
Hakuna sehemu ‘non executive directors’ (NED) hawana mshahara na marupurupu kwa hizo part time job.Wewe nawe Kumbe hamna kitu, wenyeviti na wajumbe wa Bodi hawana mishahara. Hupata pesa kama kiinua mgongo Fulani kila baada ya miaka mitatu ambao ndiyo muda wa Bodi kuwapo madarakani. Na wengine huigawa Kwa tatu Ili kila mwaka wapate chochote. zaidi ya hapo ni posho ya vikao.
Usalama wa taifa unafananisha na jeshiSio kirahisi hivyo, muda ule ule JPM anakata roho tayari allegiance ya TISS ilihamia kwa Samia so worst outcome ingekua vita au mauaji mfululizo. Na jeshi sio kama wote wangekubali tu ingegawanyika na ingekua civil war na power struggle.
So akiangalia madhara akaona mambo yasiwe mengi.... kimanyema ningeita deterrent theory yaani unafanya maamuzi A hata kama huyapendi kwa kupima madhara ya maamuzi B.
Jenerali Mabeyo amepita katika mtihani mgumu, yaani anastahili heshima zetuBinafsi nimeshangazwa na timing ya interview ya Jenerali, why now?? Na si wakati ule ama wakati ujao?
Kwa nini hasa.
Mambo mengi yalitumia busara badala ya taratibu na miongozo.Nikija kwenye hoja "busara" ilitumika badala ya taratibu za kikatiba kama kumuapisha baada ya 24 hours... Maswali yanaongezeka.
Ndiyo maana nikashauri tujikite kwenye mema tu aliofanya Hayati Magufuli (R I.P) kwenye mjadala. Pia tujikite kumshauri Mama Dr. Samia katika kutimiza wajibu wake kwa kuwa ni Rais wetu sasa, Maana tumeambiwa na Jenerali kuwa Rais anapenda sana kushirikisha watu kwenye kazi zake.
Nyuzi za hivi unatakiwa kuwa makini sana kuchangia, hutakiwi kuwa too emotional vinginevyo unaweza jikuta matataniHa ha haaaaaaaa uko na akili mingi
MV Bukoba ilipozama, tukadhani tumejifunza.Nadharia na uhalisia ni vitu tofauti sana.
Kujifunza toka kwa wengine ni nadharia tu. Tukio likikutokea wewe, huo ni uhalisia.
Na dynamics za wengine, haziwezi kufanana na za kwako.
Safari ijayo likitokea tena, unataka tuige Wamarekani wanafanyaje au tufanye vile itufaavyo kutokana na uzoefu wetu kwa kutumia taratibu zetu?
Na ndo maana nampa pongezi zake.Ni Gen Mabeyo kaamua kusema tu kilichojiri vinginevyo tusingekuwa na hiyo experience
Tunahitaji kuwa na record na haya mambo yaongozwe si kutumia busara.
Tatizo letu, au kwa usahihi niseme tatizo la CCM ni kuongoza/ kutawala kwa kutumia mazoea zaidi na si kwa taratibu kwa mujibu wa sheria.Yes kwasababu Rais alikuwa mgonjwa Hospiali tena mahututi.
Makamu wa Rais alitakiwa awe karibu ili kuchukua majukumu ingalitokea vinginevyo, ni kwa mujibu wa Katiba ya JMT 1977 Sura ya Pili 37(2)(3)
It's unconscionable kwamba Rais yu mahututi anapewa sakremento na Makamu wa Rais hayupo around.
Kwa maneno mengine maamuzi ya nchi yalifanywa na watu watatu, CDF , IGP na DGIS.
Wakati wanahangaika Makamu wa Rais yupo Tanga katika mkutano wa hadhara ! huo si uendeshaji nchi
Waziri Mkuu ndiye mtendaji wa Serikali, naye pia alitakiwa awe karibu si kwasababu Rais anaumwa, bali Rais yu mahututi na lolote linaweza kutokea! na lilitokea kwa mujibu wa Mabeyo
CDF, DGIS na IGP ni Washauri wa Usalama si waendeshaji wa serikali wakati Makamu na Waziri mkuu wanaendesha mikutano. Mikutano haina tija kwa wakati uliokuwepo.
Hoja si Rais Kuumwa, hoja ni Rais kuwa Mahututi na sote tulijua! ilishangaza viongozi wanahutubia mikutano na wengine kusema ''yupo anachapa kazi''.
Haya, sawa. Uko sahihi.MV Bukoba ilipozama, tukadhani tumejifunza.
Ila kila ajali na janga linapotutokea, tunakuwa kama wageni wa tukio husika.
Au labda ni hadi majanga na misiba mingapi ndipo tunakuwa na umahiri wa kuikabili kwa weledi?
Unajitahidi sana bila mafanikio kuutetea ujinga.
Bahati ni kufunuliwa kuhusu kifo, au kujua kwamba Mungu amekupa rehema?Ukipata bahati ya MUNGU Kukufunulia kifo chako jua wewe MUNGU amekuchagua hiyo nafasi wanapata wachache sana 😢
Huyu Mabeyo siyo tu kwamba ni Jenerali wa Jeshi vitani lakini ni Jenerali aliyevusha Taifa wakati mgumu.Na ndo maana nampa pongezi zake.Ila yeye ni mtu mmoja tu na kafunguka kupitia kile alichokiona yeye.
Usishangae wengine waliokuwepo nao kuwa na version tofauti ya tukio lilivyojiri.
Licha ya hivyo, kudos kwake.
Exactly!!!Tatizo letu, au kwa usahihi niseme tatizo la CCM ni kuongoza/ kutawala kwa kutumia mazoea zaidi na si kwa taratibu kwa mujibu wa sheria.
Laiti katiba iliyopo [hata kama ni mbaya] ingefuatwa kwa jinsi inavyotoa mwongozo, wala kusingekuwepo na sintofahamu iliyokuwepo.
It’s not that complicated.
CCM wamejenga utamaduni mbaya wa kutokufuata katiba na kutokuiheshimu katiba.
Hili ni suala la kiutamaduni wa CCM. Ni utamaduni mbaya sana unaoruhusu mtu hata kuvunja katiba waziwazi kabisa na hakuna mtu hata mmoja kutoka kwenye chama chao au serikali yao anayesema hapana.
Kama kuna lawama au kuna aliyekosea, mlaumiwa au mkosaji huyo ni CCM na viongozi wake wote maana hakuna hata mmoja wao aliyejaribu kuondokana na huo utamaduni.