Mwamba 777
JF-Expert Member
- Nov 23, 2020
- 2,780
- 4,504
na ndio maana Lisu kapoa kama maji ya mtungi kuonesha yuko pamoja na mama. Huyu suzy mleta mada hapa atasubiri sana na sukuma gang wenzake.TL atakuwa anajichimbia kaburi lake na kupotea kwenye ramani kama atamdhihaki Rais SSH.
Ikumbukwe Lissu aliposhambuliwa na risasi za kikundi cha akina Makonda, kisha kufanyiwa emergency treatment pale Dodoma Regional Hospital, alisadirishwa hadi Nairobi kwa matibabu.
Akiwa pale Agakhan hospital hakuna mwana CCM hata mmoja aliyethubutu kumtembelea pale hospitalini zaidi ya Makamu wa Rais wa wakati huo Samia Suluhu. Waliogopa kwa kuwa Magufuli hakutaka Lissu awe hai na hakutaka afarijiwe Wala kulipiwa matibabu.
Kama Lissu atamnanga Rais SSH kwa mdomo wake mchafu basi LAANA kubwa itampata kwa kukosa SHUKRANI