Chukua hii: 2022 ujio wa Tundu Lissu utaleta Kimbunga

Chukua hii: 2022 ujio wa Tundu Lissu utaleta Kimbunga

Huwa sikubaliani na wewe kwa mambo yote na kwa dharau zako sitarajii kukubaliana na wewe kwa lolote. Lakini...

...tambua Tundu anautaka u Rais wa Tanzania kwa gharama yeyote ile.

...tambua Tundu anarejea na MIKAKATI mahsusi ya namna ya kuiondoa CCM madarakani kutoka kwa wazungu na usifikiri wamewekeza kwa Tundu bure bali muda wote huo wameishi naye wakimuandaa ili aje kuchukua madaraka ili wao walichoki target iwe rahisi kukipata kwalo.

...tambua Tundu hawezi kamwe kuwa na huruma na mwana CCM/mtu yeyote aliyepo CCM kwa namna walivyomfanya.

...2022 ni mwaka mbaya sana kwa CCM kwa sababu kwanza tayari wao kwa wao wamegawanyika na wanatukanana waziwazi!
Mnafeli kwa sababu zifuatazo;
1. TL hafai kuwa Rais wa nchi...ila anafaa kuwa Waziri au Waziri mkuu
2. Wenye Chadema yao hawawezi kukubali eti mgeni wakuja asimame kama rais
 
Mimi ni MBA holder, kama hujui uandishi wa tafsida shauri yako.

Lissu hata kama anataka uRais wa Tz, akijichanganya kumponda Mama tu, itakula kwake big time. Hizi ni principle za maisha tu ndiyo maana nimesema atalaanika.

Halafu uRais wa Tz watu wote waliouvalia njuga, hawajawahi kuupata. Angalia akina Salim Ahmed Salim (akapata Mwinyi), Kolimba na Malecela (akapata Mkapa), Sumaye na Kigoda ( akapata Kikwete), Lowassa na Membe ( akapata Magufuli)

Na sasa ni Samia. Kama CDM kuna siku watapata uongozi wa Nchi hii, Rais atakuwa siyo Lissu au Mbowe. Take it from me wewe Sikuma Gang
CDM ni genge la kifamilia ya kichaga...hawawezi kumuachia mtu wa kabila lingine awe juu yao
 
TL inabidi aachane na tabia ya kutumia lugha isiyofaa wakati wa uwasilishaji wa ujumbe wake pia ajiepushe kujiona mtu anayejua sana kuliko wengine wakati siyo sahihi

Pia ajifunze kuwa na busara na hekima
Mtu pekee mwenye heshima , utu , adabu na hekima. Lissu akiweza kuiga sifa chache tu za Mh Mbowe atakuwa a good leader.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tundu lissu akija atampelekea mama Moto hatari..wananchi wengi hawaipendi hii serikali kutokana na utendajiwa mama ktk tozo,suala la machinga,hali ngumu ya maisha,wizi na ufujaji kushamiri, Mambo ya ajabu ajabu yamerudi...akitoke mpinzani strong lazima mama aondoke..

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Samia atatuma watui kumkamata na yeye kumpa kesi ya uhaini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnafeli kwa sababu zifuatazo;
1. TL hafai kuwa Rais wa nchi...ila anafaa kuwa Waziri au Waziri mkuu
2. Wenye Chadema yao hawawezi kukubali eti mgeni wakuja asimame kama rais

..unasema hivyo kwasababu umezoea Rais mwenye madaraka ya kifalme.

..Lissu alishasema mara kadhaa hataki Uraisi wa Kifalme kama huu wa katiba ya sasa.

..Aliahidi hataki Uraisi ulio juu ya sheria wenye kinga ya kutoshtakiwa.

..Tuandike katiba mpya yenye kipengele vinavyowadhibiti viongozi wa hovyo-hovyo.


Cc Tindo
 
P
Tunakuja ww ni msaka tonge (teuzi)
 
Ujio wa Tundu Lissu utaisumbua sana CCM. kwa sababu siioni tena Ile CCM mpya, iliyokuwa imejaa wababe, watu jeuri na wauaji kwelikweli.

CCM mpya ilitetewa na wakuu WA mikoa, sasahiv sion na sisikii wakuu wa wilaya na mikoa wakifoka kama zamani. Siwasikii katibu Mkuu wa CCM na katibu WA itikadi na uenezi WA CCM wakiwafokea wapinzani.

Kule bungeni Ndugai amebanwa na Wana CCM wenzake. Hana pa kupumulia.

Wimbo WA katiba mpya na tume huru ya uchaguzi unazidi kuimbwa kila Kona ya nchi, unaimbwa na waliowahi kuwa viongozi ndani ya serikali ya CCM.
 
Hakika ujinga wa uzeen lazma utakufa tu
Tundu Lissu atakuja TZ mwaka 2025 kwenye mradi wake wa kugombea urais wa JMT. Na ujue japokuwa viongozi wa CHADEMA wanadai hawatashiriki uchaguzi bila tume huru yeye Lissu atahakikisha anagombea japo ana uhakika wa kushindwa ila kwake ni mradi unaolipanvizuri. Kuna dhana kuwa Lissu anaomba Mbowe afungwe jela ili iwe rahisi kwake kugombea kwa sababu atakuwa kaimu mwenyekiti. Kwenye uchaguzi Lissu anawadanganya mabeberu kuwa atashinda na wanampa pesa nyingi wakiamini kuwa akishinda atabadilisha zile sheria za madini zilizoboreshwa wakati wa Magufuli. Na hata pesa inayochangishwa kwenye kampeni zake hazikusanywi na CHADEMA bali ndugu zake ili ionekane michango inafadhilikampeni kuwa ni pesa za mabeberu. Na picha nyingi lazima zitumwe ku-retire imprest yapesa alozopokea. Kwa nini Lissu adanganye kuwa anakuja 2022 wakati anasubiri kipindi cha uchaguzi 2025?
 
Mnafeli kwa sababu zifuatazo;
1. TL hafai kuwa Rais wa nchi...ila anafaa kuwa Waziri au Waziri mkuu
2. Wenye Chadema yao hawawezi kukubali eti mgeni wakuja asimame kama rais

Huna ujualo, umezama kwenye propaganda za kizee mpaka umekuwa mjinga. Hao wenye chama chao mbona walimruhusu kugombea uraisi uchaguzi uliopita?
 
Tukimjibu kwa hoja huyu atatusumbua,tutamzomee,tutamkashfu tutamtukana.Tunao vijana maalum kwa kazi hiyo tuliowapa mafunzo kwenye makambi.
🤣🤣🤣🤣🤣
 
Tatizo hamjiulizi kama ana watu wa kuongoza naye nchi....hivi TL akiwa rais halafu Mbowe atamuachaje?ataweza kumzuia Mbowe asiuze nchi kweli?akijaribu kumzuia nini kitatokea?

..katiba inapaswa kuzuia viongozi kuuza nchi.

..kwa katiba hii ya sasa hivi hata " Mr.Clean " Ben Mkapa aliuza nchi.

..nchi yetu ina mali nyingi, wananchi wasiofuatilia, na katiba inayolinda viongozi, hayo ndio mazingira yanayowezesha viongozi kuuza nchi.

..Lissu aliahidi kwamba akichaguliwa ataanzisha mchakato kuleta KATIBA INAYOWAJIBISHA VIONGOZI.
 
..katiba inapaswa kuzuia viongozi kuuza nchi.

..kwa katiba hii ya sasa hivi hata " Mr.Clean " Ben Mkapa aliuza nchi.

..nchi yetu ina mali nyingi, wananchi wasiofuatilia, na katiba inayolinda viongozi, hayo ndio mazingira yanayowezesha viongozi kuuza nchi.

..Lissu aliahidi kwamba akichaguliwa ataanzisha mchakato kuleta KATIBA INAYOWAJIBISHA VIONGOZI.
TL hawezi kuchaguliwa na wenye akili timamu. Aendelee kujifurahisha.
 
Back
Top Bottom