Lagrange
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 2,441
- 2,878
Habari ,,
Huu mji wa Dodoma umekuwa na kodi kubwa sana za fremu zisizo endena na uhalisia wa kibiashara , mfano mwaka Huu 2026 nyumba zilizo rekebishwa maeneo ya mjini katikati Kodi ni 4m,3m,2.5m ,2m na 1.5m kwa mwezi . Walio kuwepo hakuna hata mmoja aliye weza kurudi wamekuja wapya
Hizo Kodi ni kubwa mno haziendani na uhalisia wa biashara kwenye huu mji ,Watu wengi wanao kuja Dodoma Kufanya biashara hawarudi kulipa kodi ,wengi wanakimbia Kodi ikiisha , Kodi sio rafiki. Kuna nyumba ilijegwa upya 2023 ,ina fremu sita ,tano wako wapangaji wapya wa awamu ya tatu na hiyo moja anakaa mtoto wa mwenye nyumba yeye halipi Kodi ,ndio Maana yupo. Hii inatupa taswira pana kuwa Kodi sio rafiki kabisa hapa mji wa Dodoma.
Kuna nyumba zimerekebishwa wameingia wafanya biashara wapya kwa Kodi za 4m na 3m kwa kweli nawaonea huruma sana ,najua Kodi ikiisha watakusanya virago au watoe pesa kwingine waje walipe.
Dodoma mjini sio fursa tena Kodi ni kubwa mno Kodi ya 12,000,000,18,000,000 ,24,000,000 ,36,000,000 na 48,000,000 kwa mwaka hapana hailipiki, hizi ni Kodi za kariako kwenye mzunguko Mkubwa Ila kwa hapa Dodoma hazilipiki , watu wengi mitaji yao imeyumba sana kisa Kodi Hizi.
Kama unakuja Dodoma kutakatisha pesa Sawa ,Ila kwa lengo la Kufanya biashara Kodi sio rafiki kabisa. Huu mji ni mdogo hauna mzunguko na wageni wa kila siku uweze kuuza ulipe hayo mamilioni.
Chukua tahadhari sana na mtaji wako hapa ni kichinjio ,
Kuna vigoli vidogo dogo vinakodishwa kwa 12,000,000 na 18,000,000 kwa mwaka , ni vidogo mno mno ,ukiviweka mali Wewe huezi kaa huko ndani , lazima ununue kofia kubwa ya jua Maana unakaa njee .
Kama una mpango wa kuja Kufanya biashara Dodoma , fikiria kwa utulivu sana sana , Kodi Hizi za mamilioni sio rafiki kabisa kwa biashara huu mji ni mdogo sana .
Kodi kwenye huu mji hazina huruma na mtaji wako. Chukua tahadhari Mtanzania mwenzangu, mtaji wa kudunduliza unapatikana kwa tabu sana, uheshimu sana.