Tetesi: Chukueni hii ya Moto Moto kabisa. Inonga, Kapombe, Chama, Manula na Baleke miamala yao ilisoma mapema sana

Wewe ni mharibifu wa soka la TZ. Unastahili ban ya maisha kwa tabia yako hii ya umbea.
 
Zamani Simba na Yanga ilikuwa ni lazima kisomwe kisomo kizito kwa ajili ya wasaliti.
Na wasaliti waliogopa Sana kisomo.
Msaliti anaweza kuwa mchezaji au kiongozi.


Kwa sababu ya kupuuzwa wazee wa Simba tutaendelea kuumizwa na Yanga kila siku,
Sababu zile desturi zetu za timu kupewa wazee wa Simba kuicheza mechi ya Yanga kupuuzwa..

Yanga hadi Leo timu hukabidhiwa wazee wa Yanga,,
Na lazima kisomo kisomwe kwa wasaliti..
 
Nakubaliana sana na wewe mkuu maana hata kwenye changing room jersey ya Ally Salim ilikuwepo ila nimeshangaa imekuwaje.

Kwa hiyo jamaa waliuza mechi siyo?
Changing room unaweka na jezi za reserve
 
Mimi ni rafiki yako lakini Simba hii ingemfunga Yanga basi neno KUDRA lingekuwa limepata mahali pa kukaa. Tusidanganyane sajilini nafasi zinazopwaya bila hivyo mtamtuhumu hata mfua jezi.
 
Mbona kichwa cha habari umeki edit ?
Tofauti na kichwa cha habari cha mwanzo baada ya hii habari ya wachezaji kufungiwa kutoka. huku ni kupotosha watu.
 
Je yanga ilisajili kiufundi??


Je simba ilisajili kwa mihemko??


Je simba alistahili kupigwa 5G na yanga??

Na Gentamycine 😂😂😂😂😂
 

Attachments

  • Screenshot_20231107-180957.png
    16.3 KB · Views: 2
Kwa kuangalia body language, Baleke angependa kucheza Yanga.
Easily Yanga wanaweza kupata saini ya Baleke.
Hakujali Simba kupoteza Jana, na pia hakutaka kuifunga Yanga Ile mechi ya mbili bila.
Inaomywsha pia yupo karibu sana na Maxi.
 
hawana lolote kaka wanabwabwaja tu. wamepigwa katika mchezo wa kawaida kabisa, kama ni kuhongwa kwanini wasiseme kwenye mechi ya alhaly ambapo kocha anamtoa chama bila sababu za msingi
 
Je simba imesajili hovyo hovyo ??

Na Gentamycine

 
Yanga ipo katika fomu na inacheza kiushindani??


Na Gentamycine

 

Attachments

  • Screenshot_20231107-181856.png
    24.6 KB · Views: 1
Wanawaonewa tu mpira Simba ilizidwa hasa baada ya kutoka Kibu Denis.
Unamtoa Kibu anaye kaba unamwingiza Miquisson ambaye hakabi kabisa.

Kocha alitakiwa japo kumwingiza Moses Phili au Chillunda.

Wachezaji wa Simba wengi hawakabi Kama Chama, Miquisson, Baleke, Ntibayonkiza.

Timu inabakia na wakabaji Sita tu lazima wachoke na matokeo ndio hayo tena.

Lakini Simba ilitakiwa wamfukuze Kocha tu kwa kushindwa kuusoma mchezo na kuruhusu kufungwa kila mechi.

Lakini Mbona Tanga Yanga tuliwafunga 5-2 lakini wenzetu walivumilia.

Kama magoli ya penati mbona nao Yanga walifunga kwa Penati Goli la 5.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Badala ya kujifukuza wao viongozi eti wanawafukuza wachezaji ili wanachama wao wasione uzembe wa viongozi wao kwa kusajili hovyo .

Chama alitaka kusawazisha kwa free kick Diarra akafanya save ya maana ikawa kona iliyoleta goli !

Manula amefanya save nyingi za hatari , yale magoli Hata Andre onana asingeweza kufuta !

Dakika 20 za mwisho wachezaji wa simba walikuwa hoi poor fitness maanake maandalizi yalikuwa duni uwezo wa mwili ulikuwa umefika Kikomo zingeongezwa dakika 30 wangepigwa 5 nyingine jumla ikawa 10!, lakini hapo sio kosa la mchezaji ni kosa la Mwalimu wa viungo.

Kwahiyo mwalimu wa viungo sawa ni halali kufukuzwa.
 
Kosa lipo na kwa Kocha Mkuu.
Tunafungwa kila mechi na timu ndogo yeye halifanyii kazi hilo tatizo.

Phili anafunga kila mechi lakini anawekwa Benchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…