Chuo Kikuu Mzumbe chamtunukia Rais Samia Shahada ya Udaktari wa Heshima katika Uongozi
DKT. SAMIA ATUNUKIWA SHAHADA YA UDAKTARI WA HESHIMA YA UONGOZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Shahada ya Udaktari ya Heshima (PhD) katika uongozi, leo tarehe 24 Novemba 2024, kwenye mahafali ya 23 ya Chuo Kikuu cha Mzumbe, yaliyifanyika Kampasi Kuu ya Morogoro.

Shahada hiyo aliyotunukiwa Mhe. Rais Dkt. Samia, imetokana na umahiri na uwezo aliouonesha kwenye uongozi katika nafasi mbalimbali alizotumikia taifa, kupitia Chama na Serikali na nje ya hapo. Pia Dkt. Samia leo ni mgeni maalum kwenye mahafali hayo yanayofanyika katika Viwanja vya Maekani.
Jf mnanifurahisha. Mimi nimeandika haya maelezo kweli?????
 
Screenshot_20241124-191935.png
 
Achana na mambo ya Open university,huko wanasoma wazee hakuna fresher anaenda kusomea bachela hapo.

Nasisitiza Mikoa 15 haikuwa na Vyuo na nimeitaja apart from yenye Vyuo ambako kote Kuna miradi ya Upanuzi wa miundombinu inaendelea.

Hutaki andika mada Yako kunipinga
Wapo freshers kibao wanasoma first degree acha upotoshaji. Dunia ya Sasa watu hawataki

kupoteza muda wanatumia online and distance learning.
 
Form 4 Failures 😆😆
Wewe uwezo wako wa kufikiri ni mdogo sana na ndio maana unaweza kuwa chawa

Unatoa hoja za uongo kwa sababu ya kujipendekeza. Uchawa umekuwa dhambi ya
jamii. Mtu kama wewe unajivunjia utu na heshima yako kisa uchawa.

Kama unawezo wa kufukiri kweli nimezungumzia form six freshers wewe unaongelea
form four failures, uoni wewe ni mropokaji usiye na data.
 
Hadi leo Ripoti ya mauaji ya Ali Kibao bado, Soka na wenzake bado hawajasema walipo na mafisadi kwa mujibu wa CAG hawajachukuliwa hatua. Hizo zote ni sifa kwa Kiongozi?
 


Chuo Kikuu Mzumbe kinatarajia Kumtunuku Rais Samia Shahada ya Udakatri wa Heshima katika Uongozi wa Chuo kama ishara ya kutambua jitihada zake katika kuboresha Elimu ya Juu Nchini hasa miundombinu,Utafiti na kuongeza idadi ya udahili.

Hiyo itakuwa ni Shahada ya 5 Kwa Rais Samia na Shahada ya 1 kutolewa na Chuo Kikuu Mzumbe.

Ikumbukwe Rais Samia ni alumni wa Mzumbe Hongera Rais Samia, jitihada zako zitambuliwe Sasa Ukiwa hai na Kila mtu anaona.👇👇

Leo Jumapili, Novemba 24, 2024 ni mahafali ya 23 ya Chuo Kikuu cha Mzumbe, Mkoa wa Morogoro.

Katika mahafali hayo yatakayofanyikia chuoni hapo,
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan atatunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima katika Uongozi ya Chuo Kikuu Mzumbe.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa William Mwegoha amesema hiyo itakuwa shahada ya kwanza ya heshima kutolewa na chuo hicho tangu kuanzishwa kwake.

Shahada hiyo ya udaktari wa heshima itakuwa ya tano Rais Samia kuoewa tangu alipoingia madarakani Machi 19, 2021 akichukua kijiti cha mtangulizi wake, hayati John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021.

Shahada nyingine nne ametunukiwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Tanzania), Chuo Kikuu cha Zanzibar, Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru (India) na Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki.

Aidha, Profesa Mwegoha amesema suala la usawa wa kijinsia limepiga hatua chuoni hapo akitolea mfano, wahitimu wa mwaka huu,"ni karibu 50/50 kwani asilimia 50.2 ya wahitimu ni wanaume na asilimia 49.7 ni wanawake. Naweza kuona jinsi tunavyopiga hatua kwa vitendo."


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima katika Uongozi ya Chuo Kikuu Mzumbe na Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kwenye Mahafali ya 23 ya Chuo Kikuu Mzumbe Mkoani Morogoroyaliyofanyika katika eneo la Maekani, Kampasi Kuu Morogoro tarehe 24 Novemba, 2024. Shahada hiyo ni ya kwanza katika ngazi hiyo ya Uongozi kutolewa na Chuo hicho tangu kuanzishwa kwake


Shahada nyingine za Udaktari wa Heshima soma viunganishi hapa chini

Rais Samia atunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu ya Usimamizi ya Utalii na Masoko ya Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA), leo Desemba 28, 2023
Rais Samia Atunukiwa Udaktari wa Uchumi (Doctorate of Economics Degree) Uturuki
Rais Samia atunukiwa Udaktari wa Heshima kutoka Chuo Kikuu cha Ankara, Uturuki, leo Aprili 18, 2024
Rais Samia atunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa, Korea, Juni 3, 2024

My Take
Hata hili Chadema watapinga ila Sasa data za takwimu zinawakataa.

Mfano mzuri ni mradi huu wa kupanua Elimu ya Juu Nchini ambapo taasisi 23 za Elimu ya Juu zinaendelea na kazi ya Ujenzi wa Miundombinu ya Kujifunzia.

Aidha Mikoa 15 ambayo hakikuwahi kuwa na Vyuo Vikuu au Matawi ujenzi unaendelea.Hii ni kazi ya Kutukuka ya Rais Samia. Haya yote yanatokea Chini ya Samia 👇👇

View: https://www.instagram.com/reel/DCr7oyLOtS4/?igsh=MWF5NWIzNHVhcm1mOQ==

Kumbe Urais mtamu hivi, mama kanawili kama katoka kuzaliwa Leo, hongera mama kipenzi cha wengi (sio kwa wote) na Mimi nitagombea Urais wa vijana wa hovyo please msiniangushe vijana wote wa hovyo, natanguliza shukrani 🙏
 
JPM akirudi Leo, hataamini PhD alizonazo Delila,kwa muda wa miaka 3 TU.
 
1. Kwakuwa mwaka 1983 alisoma hapo (pale) hivyo nae ni Alumnae?

2. Kwakuwa Mkuu wa Chuo cha Kutoa PhD Kiholela holela ni Poti wa Kwao Mwambaoni?

3. Kwakuwa Mpambe wake nae ni Alumnae wa Chuo cha Kutoa PhD Kiholela holela?

4. Kwakuwa tunataka nae sasa aanze Kutukumbuka katika Teuzi zake kama afanyavyo kwa Mlimani Chuo?

GENTAMYCINE sasa nipo tayari kabisa kusoma Comments zenu ili nami pia nitafute Chuo cha kunipa PhD nyepesi.

Cc: Lucas Mwashambwa
 
1. Kwakuwa mwaka 1983 alisoma hapo (pale) hivyo nae ni Alumnae?

2. Kwakuwa Mkuu wa Chuo cha Kutoa PhD Kiholela holela ni Poti wa Kwao Mwambaoni?

3. Kwakuwa Mpambe wake nae ni Alumnae wa Chuo cha Kutoa PhD Kiholela holela?

4. Kwakuwa tunataka nae sasa aanze Kutukumbuka katika Teuzi zake kama afanyavyo kwa Mlimani Chuo?

GENTAMYCINE sasa nipo tayari kabisa kusoma Comments zenu ili nami pia nitafute Chuo cha kunipa PhD nyepesi.
Achana na mavitu ya ajabu ndugu utapoteza uwezo wako acha majinga yapeane
 
1. Kwakuwa mwaka 1983 alisoma hapo (pale) hivyo nae ni Alumnae?

2. Kwakuwa Mkuu wa Chuo cha Kutoa PhD Kiholela holela ni Poti wa Kwao Mwambaoni?

3. Kwakuwa Mpambe wake nae ni Alumnae wa Chuo cha Kutoa PhD Kiholela holela?

4. Kwakuwa tunataka nae sasa aanze Kutukumbuka katika Teuzi zake kama afanyavyo kwa Mlimani Chuo?

GENTAMYCINE sasa nipo tayari kabisa kusoma Comments zenu ili nami pia nitafute Chuo cha kunipa PhD nyepesi.
Luka Mwashamba ujee hukuuu
 
Back
Top Bottom