Coming soon: New Kawe City (Uptown Kawe)

Coming soon: New Kawe City (Uptown Kawe)

hii miradi kwa tanzania ya sasa haiwezekani maana wateja wenyewe hakuna, ba ndio hao wameacha kuja bongo licha ya miaka 20 ya kuvutia wawekezaji, sasa hao makarani wa barclays ndio watakao kuwa wapangaji na wanunuzi wa hizo bidhaa hapo

Ni Mradi wa ubia na NHC, sitanii, fuatilieni
 
Shukrani kwa serikali ya awamu ya nne. Stay tuned! Mambo mazuri yanakuja na yataendelea kuja chini ya serikali ya CCM.

Kama hutaki maendeleo wewe utakuwa ni mchawi na ukatafute nchi ya kuishi.

Ni wazo zuri lakini nitaisifia serikali ya awamu ya nne pale tu itakapowatoa watoto wote wa shule ya msingi kutoka kukalia mawe na kuwaweka kukalia madawati wakati inamaliza muda wake. Haya ya miji mipya kwa baadhi yetu hayana maana yo yote wakati watoto bado wanakalia mawe darasani au akina mama wanatembea maili tatu na watoto migongoni kutafuta maji!

bongo hali ya madarasa mjengwablog 8-3-12.jpg

View attachment 89565
 
Haya maghorofa yakianguka atapona mtu hapo!! nilikuwa Hamburg Ujerumani hivi karibuni nikauliza mbona sijaona majengo marefu kama katika miji mingine ya Ulaya wakaniambia majengo marefu yanapoteza madhari ya mji, kukabiliana na majanga ya moto ni gharama na zaidi ya yote uokoaji dhidi ya maafa ni mgumu sana, Hao Ndio Wajerumani Unaowasikia!!!
 
Kama unajengwa kwa kodi za watanzania big nooooo.....yaani watu hatuna dawa, barabara za uhakika na madawati halafu nyie mnaendekeza anasa!!
 
Trust me hapo unafurahia picha tu, hiyo michoro ni mikakati ya kutuibia tu. Kama kweli wanapenda kuendeleza hii nchi, wamalize kwanza mradi wa Kigamboni. Kesho watakuja na mapichapicha mengine ya kupaendeleza Manzase, tutakusanyika hivi hivi kushangaa picha na kusifia. Mafisadi yameshajua sisi tunapenda mipicha, so wataiproduce sana kabla ya utawala huu kuisha ila hakuna mradi utasimama.

Mkuu kwani kuna tatizo gani miradi yote ikitekelezwa in parallel, mimi nafikili Investor wa Kigamboni na wa Kawe ni watu/makampuni mawili tofauti.
 
Haya maghorofa yakianguka atapona mtu hapo!! nilikuwa Hamburg Ujerumani hivi karibuni nikauliza mbona sijaona majengo marefu kama katika miji mingine ya Ulaya wakaniambia majengo marefu yanapoteza madhari ya mji, kukabiliana na majanga ya moto ni gharama na zaidi ya yote uokoaji dhidi ya maafa ni mgumu sana, Hao Ndio Wajerumani Unaowasikia!!!

Mkuu nafikili huu ni utamadumi wa nchi karibu zote za Ulaya - hawapendi kabisa ma SkyScrappers; Merikani ya Kasikazini na Nchi za Mashariki ya mbali specifically Uchina na Singapore ndio wako obsessed na Maghorofa marefu kupindukia.
 
Wadanganyika kwa kupenda kuangalia mapicha.

Picha zimependeza sana. Zimetumika bilioni ngapi kuchora picha hizi?

Sijui hii miradi itaonekana kihalisia tutakaposherehekea miaka 100 ya uhuru au bado tutatembea na mabango yenye picha ya miradi hii ili wananchi waone tunayokusudia kufanya?

Hapo hujataja Kigoma kuwa Califonia na Mtwara kuwa Dudai.

Mradi wa maisha bora kwa kila mdanganyika na kugawana umasikini umeshakamilika?
 
Shukrani kwa serikali ya awamu ya nne. Stay tuned! Mambo mazuri yanakuja na yataendelea kuja chini ya serikali ya CCM.

Kama hutaki maendeleo wewe utakuwa ni mchawi na ukatafute nchi ya kuishi.
Ni mtu mpumbavu tu anayeweza kushangalia maghorofa marefu akidhani ndiyo maendeleo. Ndiyo maana wengi wetu tumechoka na hiki chama kinacholeta maendeleo ya vitu badala ya watu.
 
Nni saawa na kununua lipstick ya 15000 wakati watoto hawana hata unga wa uji ndani.

Prioritisation!!!!!
 
Wacha ije maana mambo ya kawaida kama umeme, Maji hamna...
 
Nimependa, niseme tu kweli...
Tunaomba mradi sasa tuukague
LIKEWISE....I hope mradi utakuwa tayari kabla sijazeeka! According to Tanzanian Standard Kuzeeka si kunaanza 70 Years? Nitawahi aisee, more than 30 years ahead!
 
Nni saawa na kununua lipstick ya 15000 wakati watoto hawana hata unga wa uji ndani.

Prioritisation!!!!!
Ukiipatia vizuri matumizi yake, hiyo lipstick itazalisha mchele, nyama, soda, ma-juicy; nini unga wa uji !!
 
Mkuu nafikili huu ni utamadumi wa nchi karibu zote za Ulaya - hawapendi kabisa ma SkyScrappers; Merikani ya Kasikazini na Nchi za Mashariki ya mbali specifically Uchina na Singapore ndio wako obsessed na Maghorofa marefu kupindukia.
Umesahau south East Asian countries, hawa wako so addicted ingawaje wanaweza ku-justfy! Nchi zao, kama hiyo Singapore, Malaysia, Indonesia ni nchi ndogo sana but highly populated!
 
Duh, Tanzania tuna plan nyingi, la kigamboni hatujamaliza, tumekwenda kawe, nako tutaunda authority? Dodoma nako tumeacha, amakweli mshika mawili moja au yote humponyoka
 
Sio vibaya! Lakini kwa nini tusimalize kipande cha Barabara kuelekea Lindi/Mtwara kabla ya kuujiingiza kwenye hii miradi wizi?
 
hata kimweri naye aliwaota wazungu wa vuga na matumbo yao makubwa meupe! wacha tuendelee kuota!
 
..only when CHADEMA itakaposhika dola...
 
Wakuu nadhani tukubaliane kitu kimoja muhimu lazima tuwe na vision ili tuweze kufika tunapokwenda, ukiangalia hizo building designs na hiyo idea yote ya kawe project tunaelekea kwenye right direction, tunachoka kuona hivi vitu kwa wenzetu wakenya, kagame na wengine.
 
Back
Top Bottom