Confirmed: Waraka wa Baraza la Maaskofu Wakatoliki(TEC) wasomwa hadharani kwa waumini wote kwa makanisa yote RC Tanzania nzima

Afu ikishasomwa ndo nini kitatokea?
Ni kazi kujuelimisha au ki argue na wewe sababu inaonyesha uelewa wako wa Mambo Ni mdogo.

Kama waraka unasomwa kwa mamilioni ya watu TZ nzima ukawaamsha hata ambao walikuwa hawajui Nini kinaendelea na bado huoni impact yake Basi ww una tatizo.

Impact siyo kwa huo mkataba tu Bali lazima ufikiri kwa mapana yake juu ya athari za kisiasa na kijamii kwa siku za mbeleni.

Nb: Dalili njema Ni Kwamba watu wameshachoka na Sasa wanahoji. Kwasababu Samia na genge lake wanafanya haya kwa sababu walishazoea Kwamba watz Ni watu wa upepo na kusahau.
 
Wakuu Natanguliza salamu , baada ya kuwasabahi naingia moja kwa moja kwenye hoja .

Jana iliagizwa kwamba ndani ya Makanisa yote na Parokia zote za kanisa Katoliki leo Jumapili , waumini wasomewe Waraka wa Maaskofu wa kupinga DP WORLD kupewa Bandari za Tanganyika .

Naweza kuthibitisha kwamba hawa watu ni Waaminifu sana ! WARAKA HUO UMESOMWA BILA HATA KUPUNGUZA NENO .

View attachment 2722618

Kuhusu faida za mkataba huo naweza kuwa na wasiwasi. Lakini kanisa la katoriki kutoa tamko kuhusu jambo lenye maslahi mapana ya taifa lina nipa wasiwasi zaidi. Vp ikiwa kundi lingine la kiimani na kidini likitoa tamko ambalo pengine likakinzana na tamko la kanisa katoriki, je nchi itakuwa katika hali gani?
Hebu tufikirie kwa mlengo huo. Tamko linalotoka kwa taasisi fulani ya kidini, ina maana ni tamko la wanataasisi hiyo, je ni lini kanisa la katoliki lilifanya white paper process ya kupata maoni ya wakatoliki wote mpaka wafikie hitimisho la kuwa mkataba huo haufai kwa niaba ya kanisa?
Nashauri, tukiwa kama nchi, tusioneshe mfano mbaya kwa kulinyamazia suala hili. Maana hili likifumbiwa macho, watakuja na mambo makubwa zaidi ambayo kama nchi yanaweza kutugawa wananchi kwa misingi ya imani zetu.

Binafsi nasema. "NAPINGA KITENDO CHA KANISA LA KATOLIKI KUTOA TAMKO LINALOPINGA MKATABA KATI YA TANZANIA NA DPW."
WAJUE CHOMBO CHAO NI KWA AJILI YA KUWALEA WAKATOLIKI KIIMANI. HIYO NI TAASISI YA KIROHO, SIYO TAASISI YA HARAKATI. KAMA WANATAKA IWE HIVYO WAENDE KWA KABIDHI WASIHI MKUU , KUBADILISHA USAJILI WAO.

NB: SIUNGI MKONO MIKATABA ISIYO NA TIJA KWA TAIFA.
 
Ni miezi sasa imepita , Swala la Bandari limekuwa kwenye headlines za medias na Kwa watanzania. Hii kampeni ya Kupinga mkataba imeenda mpaka vijijini, Yani imezidi hata ile ya "NYUMBA NI CHOO"

Sijui na nyie mnajiuliza kama mimi, Kwamba Swala ni Bandari TU?!
Au kuna yaliyo chini ya Kapeti?!

Hatari ni kwamba Siasa na Dini tayari limeingilia kati kwenye mgogoro huu. Hivi vitu vimeshasababisha Baadhi ya Nchi kuwa kwenye Vita kwa Karne sasa.

Kwa jicho la ndani , Dini na migogoro ya kisiasa inayoendelea litaipeleka Tanzania yetu tunayoipenda sehemu mbaya.

Tuombee sana Taifa Letu
 
Watanzania hatuitaki DPW na vipengere vyake vya unyonyaji full stop.
HIZI HAPA KESI 10 ZA DP WORLD KATIKA MAHAKAMA YA USULUHISHI WA KIMATAIFA

1) DP World dhidi ya Kenya (2022). Kituo cha Kimataifa cha Kutatua Mizozo ya Uwekezaji (ICSID) kwa sasa kinasikiliza kesi iliyofunguliwa na DP World dhidi ya Kenya. DP World inatafuta fidia kwa kukiukwa kwa mkataba uliofanywa na Kenya.

2) DP World dhidi ya Ethiopia (2022). ICSID pia inasikiliza kesi iliyofunguliwa na DP World dhidi ya Ethiopia. DP World inatafuta fidia kwa kukiukwa kwa mkataba uliodaiwa kufanywa na Ethiopia.

3) DP World dhidi ya Djibouti (2021). ICSID ilitupilia mbali kesi iliyofunguliwa na DP World dhidi ya Djibouti. DP World ilikuwa inatafuta fidia kwa kukiukwa kwa mkataba uliodaiwa kuvunjwa na Djibouti.

4) DP World dhidi ya Pakistan (2020). ICSID ilitupilia mbali kesi iliyofunguliwa na DP World dhidi ya Pakistan. DP World ilikuwa inatafuta fidia kwa kukiukwa kwa mkataba uliodaiwa kuvunjwa na Pakistan.

5) DP World dhidi ya India (2019). ICSID ilitupilia mbali kesi iliyofunguliwa na DP World dhidi ya India. DP World ilikuwa inatafuta fidia kwa kukiukwa kwa mkataba baina yake na India.

6) DP World dhidi ya Argentina (2018). ICSID ilikataa kesi iliyofunguliwa na DP World dhidi ya Argentina. DP World ilikuwa inatafuta fidia kwa kukiukwa kwa mkataba uliodaiwa kuvunjwa na Argentina.

7) DP World dhidi ya Chile (2017). ICSID ilikataa kesi iliyofunguliwa na DP World dhidi ya Chile. DP World ilikuwa inatafuta fidia kwa kukiukwa kwa mkataba baina yake na Chile.

8) DP World dhidi ya Uruguay (2016). ICSID ilikataa kesi iliyofunguliwa na DP World dhidi ya Uruguay. DP World ilikuwa inatafuta fidia kwa kukiukwa kwa mkataba baina yake na Uruguay.

9) DP World dhidi ya Peru (2015). ICSID ilikataa kesi iliyofunguliwa na DP World dhidi ya Peru. DP World ilikuwa inatafuta fidia kwa kukiukwa kwa mkataba na uporaji uliodaiwa kufanywa na Peru.

10) DP World dhidi ya Brazil (2014). ICSID ilikataa kesi iliyofunguliwa na DP World dhidi ya Brazil. DP World ilikuwa inatafuta fidia kwa kukiukwa kwa mkataba uliodaiwa kuvunjwa na Brazil.

Ni muhimu kuelewa kuwa hizi ni baadhi tu ya kesi nyingi ambazo DP World imehusika nazo. DP World ni gwiji mkubwa katika tasnia ya bandari duniani, na amehusika katika migogoro mingi na serikali ulimwenguni. Migogoro hii mara nyingi imekuwa migumu kutatuliwa.
 
Kumekucha, kumekucha Tamko la TEC lasomwa kwenye Makanisa yote ya Kikatoliki nchini Tanzania. Waraka huo umekataliwa pia na Waumini wa Kanisa la Katoliki. Sisi waumini wa Kikatoliki tutapeleka tamko hili kwenye Jumuiya ndogondogo ili tuwasomee na kutoka hapo tamko hili litapelekwa kwa kila familia na Mkuu wa familia kuwasomea familia yake na ikiwezekana kuwasomea majirani zake hata wale wasio Wakatoliki. Kama Mkataba ulikuwa na nia nzuri kwa nini hapakuwa na ushindani?. Sauti ya watu ni Sauti ya Mungu. Tumsifu Yesu Kristo.
 
Hii siku imekua kama Christmas ya ghafla tunaomba waraka usomwe ten wiki ijayo na Sissi wapagani tuje tusikilize

Leo sijaenda church Ila kwa hii taarifa naweza kuja wiki ijayo tuu kupokea waraka matakatifu

Cc:😛apa
Cc::askofu
Cc::maparoko
 
Leo nilichelewa misa ya kwanza ikabidi niwapeleke watoto misa yao.
Wakati nafuatilia kilichokuwa kinaendelea ndani Mara waraka ukasomwa baada ya hapo akaletwa mtaalam wa elimu ya urais na mtaalam wa sheria .
Watoto wakapewa elimu ya uraia na kutafsiriwa mkataba kwa lugha nyepesi, kifungu kwa kifungu Cha mkataba wote.
Watoto waliokuwa wakubwa kidogo wenye uelewa walitoka kanisani wakilia na kushangaa inawezekanaje Watanzania kuiuza nchi yao kiasi kile.
Wakuu tutulie tuone kinachofuata.
 
Niko hapa kuthibitisha hilo pasi na chembe ya shaka yoyote leo nimehudhuria ibada ya misa takatifu katika kanisa la St Joseph Cathedral Dar.

Waraka umesomwa kwa waumini wote, na kupitia reliable source ya Jesuits agent amenithibitishia makanisa yote na vigango vyote vya kanisa katoliki Tanzania nzima wamesomewa waraka huo leo.

Pascal Mayalla unajisikiaje kwa kuikana imani kwa sababu ya vipande 30 vya fedha?

Mama Samia anakwenda kuwaabisha wanafki na machawa wote, kesho asubuhi Rais anapewa brief na DG wa usalama wa Taifa
reaction ya Taifa baada ya waraka wa TEC na Rais anakwenda kulihutubia Taifa, watch n see, lisipotekea hili JF wanipige life ban.

Roma Locuta, Causa Finita Est.

Kwa kua Tanzania ni yaTEC peke yao.
 
Kuhusu faida za mkataba huo naweza kuwa na wasiwasi. Lakini kanisa la katoriki kutoa tamko kuhusu jambo lenye maslahi mapana ya taifa lina nipa wasiwasi zaidi. Vp ikiwa kundi lingine la kiimani na kidini likitoa tamko ambalo pengine likakinzana na tamko la kanisa katoriki, je nchi itakuwa katika hali gani?
Hebu tufikirie kwa mlengo huo. Tamko linalotoka kwa taasisi fulani ya kidini, ina maana ni tamko la wanataasisi hiyo, je ni lini kanisa la katoliki lilifanya white paper process ya kupata maoni ya wakatoliki wote mpaka wafikie hitimisho la kuwa mkataba huo haufai kwa niaba ya kanisa?
Nashauri, tukiwa kama nchi, tusioneshe mfano mbaya kwa kulinyamazia suala hili. Maana hili likifumbiwa macho, watakuja na mambo makubwa zaidi ambayo kama nchi yanaweza kutugawa wananchi kwa misingi ya imani zetu.

Binafsi nasema. "NAPINGA KITENDO CHA KANISA LA KATOLIKI KUTOA TAMKO LINALOPINGA MKATABA KATI YA TANZANIA NA DPW."
WAJUE CHOMBO CHAO NI KWA AJILI YA KUWALEA WAKATOLIKI KIIMANI. HIYO NI TAASISI YA KIROHO, SIYO TAASISI YA HARAKATI. KAMA WANATAKA IWE HIVYO WAENDE KWA KABIDHI WASIHI MKUU , KUBADILISHA USAJILI WAO.

NB: SIUNGI MKONO MIKATABA ISIYO NA TIJA KWA TAIFA.

Upo Tanzania wewe au Kenya Ulimiskia shehe Mwaipopo mbona alijipambanua yupo upande wa Dp world elewa Kanisa Katoliki ni mamlaka kamili je umesali leo je umesikiliza waraka huo mkataba ni Rubish kabisa na kanisa lipo sahihi.
 
Niko hapa kuthibitisha hilo pasi na chembe ya shaka yoyote leo nimehudhuria ibada ya misa takatifu katika kanisa la St Joseph Cathedral Dar.

Waraka umesomwa kwa waumini wote, na kupitia reliable source ya Jesuits agent amenithibitishia makanisa yote na vigango vyote vya kanisa katoliki Tanzania nzima wamesomewa waraka huo leo.

Pascal Mayalla unajisikiaje kwa kuikana imani kwa sababu ya vipande 30 vya fedha?

Mama Samia anakwenda kuwaabisha wanafki na machawa wote, kesho asubuhi Rais anapewa brief na DG wa usalama wa Taifa
reaction ya Taifa baada ya waraka wa TEC na Rais anakwenda kulihutubia Taifa, watch n see, lisipotekea hili JF wanipige life ban.

Roma Locuta, Causa Finita Est.
Then what? Acha wajifurahishe ili kuondoa stress i.e wanajipa psychological relief tu
 
Upo Tanzania wewe au Kenya Ulimiskia shehe Mwaipopo mbona alijipambanua yupo upande wa Dp world elewa Kanisa Katoliki ni mamlaka kamili je umesali leo je umesikiliza waraka huo mkataba ni Rubish kabisa na kanisa lipo sahihi.

Sikumsikia, lkn kwa huyo Shehe kutoa maoni yake ni haki yake. Lkn kikundi kidogo kutumia taasisi ya kidini kutoa maoni yao ni jambo lisilokubalika.
 
Niko hapa kuthibitisha hilo pasi na chembe ya shaka yoyote leo nimehudhuria ibada ya misa takatifu katika kanisa la St Joseph Cathedral Dar.

Waraka umesomwa kwa waumini wote, na kupitia reliable source ya Jesuits agent amenithibitishia makanisa yote na vigango vyote vya kanisa katoliki Tanzania nzima wamesomewa waraka huo leo.

Pascal Mayalla unajisikiaje kwa kuikana imani kwa sababu ya vipande 30 vya fedha?

Mama Samia anakwenda kuwaabisha wanafki na machawa wote, kesho asubuhi Rais anapewa brief na DG wa usalama wa Taifa
reaction ya Taifa baada ya waraka wa TEC na Rais anakwenda kulihutubia Taifa, watch n see, lisipotekea hili JF wanipige life ban.

Roma Locuta, Causa Finita Est.
waraka huu waendelee kuusoma hati uchaguzi wa mwakani serikali za mitaa na uchaguzi wa 2025 kwenye urais. pia, wawakumbushe waumini wao kwamba wabunge waliowachagua wameshindwa kuwakilisha mawazo yao bungeni wakawakilisha ya kwao binafsi, hivyo 2025 wawe makini wachague watu watakaowasemea wao, sio wale wanaoenda kusemea familia zao na matumbo yao.
 
Niko hapa kuthibitisha hilo pasi na chembe ya shaka yoyote leo nimehudhuria ibada ya misa takatifu katika kanisa la St Joseph Cathedral Dar.

Waraka umesomwa kwa waumini wote, na kupitia reliable source ya Jesuits agent amenithibitishia makanisa yote na vigango vyote vya kanisa katoliki Tanzania nzima wamesomewa waraka huo leo.

Pascal Mayalla unajisikiaje kwa kuikana imani kwa sababu ya vipande 30 vya fedha?

Mama Samia anakwenda kuwaabisha wanafki na machawa wote, kesho asubuhi Rais anapewa brief na DG wa usalama wa Taifa
reaction ya Taifa baada ya waraka wa TEC na Rais anakwenda kulihutubia Taifa, watch n see, lisipotekea hili JF wanipige life ban.

Roma Locuta, Causa Finita Est.
walishajipanga, waliambiwa kuhusu hili na watu wao, kwani hukusikia kikao cha baraza la mawaziri sambamba na hii. Ndio sababu ya kuachiwa akina Slaa na wenzake. Kifuatacho sijui walikubaliana nn tusubiri ( ila nahisi ni kukomaa shingo kimya kimya)
 
Niko hapa kuthibitisha hilo pasi na chembe ya shaka yoyote leo nimehudhuria ibada ya misa takatifu katika kanisa la St Joseph Cathedral Dar.

Waraka umesomwa kwa waumini wote, na kupitia reliable source ya Jesuits agent amenithibitishia makanisa yote na vigango vyote vya kanisa katoliki Tanzania nzima wamesomewa waraka huo leo.

Pascal Mayalla unajisikiaje kwa kuikana imani kwa sababu ya vipande 30 vya fedha?

Mama Samia anakwenda kuwaabisha wanafki na machawa wote, kesho asubuhi Rais anapewa brief na DG wa usalama wa Taifa
reaction ya Taifa baada ya waraka wa TEC na Rais anakwenda kulihutubia Taifa, watch n see, lisipotekea hili JF wanipige life ban.

Roma Locuta, Causa Finita Est.
Ukisoma kitabu cha Dkt Slaa kiltwacho Nyuma ya Pazia, utagundua mauchafu na madudu mengi sana ya ndani ya baraza la maaskofu.

➡️Ukurusa wa 26 ibara ya 4 ya kitabu hicho, Dkt Sláa anaeleza kwa kina kwanini alimua kuachana na Upadre
1991. Kikubwa ikiwa ni wizi uliotamalaki ndani ya TEC.

➡️Kupitia Dkt Slaa mwenyewe, inatufanya tusiwaamini
TEC hata kidogo, TEC ni wezi na wala rushwa, Slaa mwenyewe kwenye kitabu chake ameeleza.

➡️Kwenye hili la waraka wao walioutoa jana, tutawezaje kuamini kwamba nyuma yao hakuna mashinikizo ya rushwa na ulaghai? Historia haiwabebi, wana uchafu mwingi sana ndani yake. Na haya sio maneno yangu, ni maneno ya Dkt Slaa Mwenyewe ndani ya kitabu chake.
 
Back
Top Bottom