Embu tupe maana yako ya neno "maombi" maana naona hayo ndo yanakutoa povuUnajibu dhaifu mno
Kwanza mimi sijazungumzia kua hakutakua na maisha baada ya corona
Pili hayo magonjwa yaliyopita na kuua watu hadi ikafikia hatua dawa imepatikana ebu elezea ni kwa namna gani dawa ilipatikana? Ni Kwa njia ya maombi?
Tatu, hiyo dawa ya maleria ilipatikana kwa maombi na jitihada za waumini ndi zilifanya mpaka mseto ukashushwa kutoka juu?
Kama majibu ya hayo maswali yatakua ni negative basi huna haki ya kusema huoni sababu ya mimi kukashfu dini.
It's Scars
Uwe unawaza kidogo.
Serikali ndo imekataza hayo mambo.
kwanini kiongozi wa dini aje kupinga?
Wewe kama hauamini kwenye dini endelea kutokuamini.
USIANZE KASHFA KWA VIONGOZI WETU WA DINI...
watu wameachwa kuingia na kutoka alafu leo ugonjwa unaingia utawalaumu viongozi wa dini au MUNGU?
TUPAMBANE NA HALI ZETU.wachawi ni sisi wenyewe.
Sent using Jamii Forums mobile app
Poleni na majukumu ya hapa na pale sasa na kale yanayowafanya msilale, niende moja kwa moja kwenye mada husika.
Kama kweli maombi yanafanya kazi kwa namna ambayo tunaaminishwa, kwanini viongozi wa dini wameungana kutekeleza agizo la kuvunja mirundamano ikiwemo mijumuiko ya kiibada ili kuikwepa korona?
Kama walifanya maombi kwa lengo la kuizuia corona isiingie nchini, lakini tunaona corona imeingia, nini kinachokufanya uwaamini kua maombi ya sasa wanayojipanga kuyafanya yataitokomeza corona mazima?
Haya mambo probably si magumu ila ugumu tunauweka sisi kwa kuweka mizaha kwa kutumia kivuli cha dini.
Hivi mfano hawa madaktari wetu na sekta ya afya kiujumla wangejumuika kwenye maombi kwa kuamini kwamba maombi ni njia madhubuti ya kutatua matatizo kama haya katika kila janga la ugonjwa. Kama ambavyo watu wa dini wamekua wakituhimiza kufanya, je tungefanikisha kutibu gonjwa lipi kwa maombi?
Ngoma inaingia tanzania wabongo tulijitia wachamungu sana kua tumepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na n'ge hivyo ukimwi kwetu sio tishio.
Lakini tunachokiona mpaka saizi mapasta na masheikh wanachukua vidonge kwa siri sana. Lakini pamoja na hayo hatuwaoni wakijisalimisha kua wameshindwa kudhibiti ukimwi kwa maombi yao.
Mungu ambaye tunamtolea sadaka kila siku halafu katika matatizo kama haya kajichimbia tu wala hatuoni juhudi zake, huyu si mungu wakuabudiwa. Ni sawa na rafiki mnafki ambaye kwenye matanuzi mkiwa viwanja mnakua naye karibu sana halafu ikatokea siku umeishiwa anakukimbia.
Wahubiri wanahubiri huku wamevaa face mask at the same time wanasema damu ya yesu ni tiba ya kila kitu. What a joke but i ain't laughing?
Tunaambiwa ukiwa na imani waweza kuamisha hadi milima lakini sikutegemea kuona vatican, mekka ziwe kipaumbele kukataza watu wasiende kwao kwa hofu ya korona.
Mungu muweza wa yote yuko wapi mbona kawasusia msala madaktari wetu halafu yeye amesizi tu eti mpaka aamshwe kwa maombi?
Kwanini mungu mjuzi wa yote na muweza wa yote ahitaji maombi?
Mbona kwenye zile hadithi za gharika na sodoma na gomora huyu mungu ali-respond haraka sana kwanini asifanye hivyo kwenye janga hili linalomaliza ndugu zetu na kudhoofisha hali ya uchumi wetu?
Hivi kweli mungu huyu yupo kweli? Maana viongozi wetu wa dini nao wanaathirika mpaka inafikia hatua italy makanisa yameshehena maiti inamaana yeye haoni?
Kwanini Mungu ahitaji maombi yetu ili aweze ku-solve matatizo yetu, ilihali anaelewa hitaji la moyo wetu hata kabla hatujasema?
====
Chukua tahadhari kwa kufuata angalizo lililotolewa na mamlaka ya afya Corona haidhibitiwi kwa maombi bali kwa kuepuka makatazo ambayo yameainishwa na shirika la afya
Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasiyoonekana.Ukiambiwa dawa ya corona imepatikana na ili ukubali kua inafanya kazi kweli inabidi uamini
Halafu ukaletewa cyanide hapo kua inabidi uamini kwanza kabla haujanywa utakubali?
Je kuamini kwako kutabadilisha chochote kwenye cyanide kua kinga ya corona?
It's Scars
Mungu hawezi kudhihakiwa kwa kuuliza maswali magumuWewe Unamchukulia Mungu Kama wakuu wa mikoa au wilaya?MUNGU hadhiakiwi apandacho mtu ndicho atachovuna, dhambi zote zinazoendelea unataka Mungu ajibu unavotaka? MUNGU ni MUNGU hata asipojibu kile umwombacho
Sent using Jamii Forums mobile app
Unavyosema "sisi tunaamini" kwani hiyo siyo dhana?Kumbe ww unaona kwamba uwepo wa Mungu ni "dhana"????
Sisi tunaamin kwamba yeye ndo aliyeiumba dunia na principle zake
Sent using Jamii Forums mobile app
Kama hili linajulikana kiujumla inamaana unataka kutuaminisha kua watu wadini ni wanafki?
Kama mungu yeye ndio ameamua watu wafe kwa korona na jambo hilo linatambulika kidini kwanini watu wadini wanafanya maombi ili wasalimike?
Halafu kama point ya mungu ni kuwadhuru watu kwa corona kwanini vatican na mekka wakataze watu wasiende kuhiji makwao kwa kuogopa kudhurika na ugonjwa?
Huoni kwa kuwazuia watu wasiende huko maana yake ni kuzuia watu wasidhurike jambo ambalo wanakua wanaenda kinyume na matakwa ya mungu?
Unaelewa kwa mujibu wako hao waliozuia nyinyi msiende huko wamefanya dhambi maana wanawanyima haki ya kusambaza ugonjwa ili watu wadhurike kama alivyokusudia mungu wenu??
Wote walioumwa corona wamekula popo na nyoka?Janga mulitafute wenyewe,halafu,lawama mpeleke kwa Mungu.
Mugu alishaleta maelekezo ya jinsi ya kuishi,kupitia vitabu,Mitume,Manabii.Vitabu vyake,vina maelekezo yote ya maisha,kipi ufanye,na kipi uwache.Kipi ule na kipi usile.Mnakula popo,nyoka,majongoo,konokono nk.Halafu mkiumwa mwalamika kwa aliyewapa tahadhari.
Ni sawa na kumlaumu,aliyetengeneza gari au machine,wakati ameshakupa maelekezo kupitia vitabu na mafundi,jinsi kuitunza machine,kwa kuifanyia service,kila ukifika mda fulani,wewe huifanyii service,halafu wamlaumu mtengeneza magari.Au gari la petrol,unakwenda weka diesel,halafu unamlamu aliyetengeneza gari,likikataa kufanyakazi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Dini yako ndo imekataza ya kwake huenda imeruhusu, sasa unataka watu wote waishi kwa kufata sheria za dini yako? We mbona hauli pop kwasababu dini zingine zimeruhusu
Na nyie wadigo imekuaje imewapata?
Kutokua sahihi wakati nikizungumzia mungu ambaye si sahihi ni sahihi pia
Halafu siku ikatokea wanasayansi wamegundua dawa utamskia "si nilikuambia kua mungu atafanya muujiza basi ule muda ambao mungu aliupanga kujibu maombi yangu ndio huu"
Katika watu wajinga na mazwa zwa hapa duniani sijaona wa kuwazidi watu wa aina ya mtoa mada.Kama Mungu angekuwa anafanya kazi kama mleta mada anavyotaka then there is no point of having a brain to the human at all.
Bahati nzuri umeweka wazi kabisa "Maombi". Maombi yana majibu mawili "NDIO" au "HAPANA".
Yani uchukue tahadhari kwa lengo lipi?Unafiki ni nini na unaingiaje katika hili ? Sijajua kwanini umewaita Wanafiki.
Ulitakiwa uwaulize watu wa dini hiyo husika. Ila kwa kukusaidia tu kwa mujibu wa dini yangu Uislamu, tuna ambiwa yafuatayo :
"Kuchukua tahadhari katika juu ya jambo fulani ni kuitendea kazi dini yaani kuyafanyia kazi mafundisho ya dini, na kutochukua tahadhari na kufanya sababu ni kuitia dosari DINI (Yaani kuitia dosari Tawheed, ile hali ya kumpwekesha Mola katika uwezo wake)"
Watu wa dini wanachukua tahadhari sababu yote yanatoka kwake na hakuna anae jua amepangiwa nini juu ya janga hili.
Mathalani katika hadithi iliyopokelewa na Imaam Muslim, inayosimuliwa na swahaba Uthmani bin Affan, inaweka wazi muongozo juu ya magonjwa ya mlipuko yakiingia katika mji. Mtume wetu alifundisha ya kuwa "Panapo ingia magonjwa ya mlipuko (Tauni) basi watu waliopo katika mji husika wasitoke katika mji huo na wale ambao wako nje ya mji huo wasiingie katika mji huo"
Kwahiyo hii yote ni tahadhari na utaratibu huu umetoka kwa yule ambaye ameuleta ugonjwa huo, Mola anatautaka tuzifanyie kazi akili zetu na tuyafanyie kazi mafundisho yake. Mifano iko mingi juu ya hili, ila kwa sasa tosheka na maelezo haya mafupi.
Hakuna aliye sema lengo la Mola ni kuwadhuru, bali nilisema ametaka ugonjwa utudhuru. Sababu kubwa ya ugonjwa au kudhihiri kwa majanga ni kutukumbusha waja wapi tukipo kosea na kurudi katika njia ya sawa. Kwahiyo kudhurika ni matokeo na si lengo.
Lakini, Allah ameweka utaratibu wake wa kuwa akileta janga sehemj halichagui yupi mkosaji na yupi si mkosaji, wote mnaingia na siku ya hesabu tutahesabiwa kwa haki.
Mathalani watu wa Makka (Nazungumzia dini hangu, na watu wa Vatican watazungumzia dini yao) hao wamefanyis kazi mafundisho ya mtume na hilo limetoka kwa Allah kwahiyo, hatutakiwi kubweta kubweteka si katika maagizo ya Allah, na kuchukua tahadhari na kutafuta sababu ndio amri ya Allah aliye juu.
Allah aliye juu akitaka jambo likufike popote ulipo linakufika, ila ukichukua tahadhari ni njia ya kutii amri yake, na kwa kutii amri yake hukuepusha na jambo hilo.
Kwahiyo huko hawajaenda kinyume a matakwa bali wametii maagizo ya Allah aliye juu.
Hili umeliona wapi toka kwangu mpaka useme kwa mujibi wangu ?
Kisha soma kwa umakini nilichokiandika ili ujue ya kuwa unae mzungumzia (Allah) hukuwahi kumjua na wala hukuwahi kupatia katika kumzungumzia.
Ahsante.
Hili swali lina ni disturb mwezi mzima sasa..Hivi kweli mungu huyu yupo kweli?
Siungi mkono hoja ,,,hapo kwenye ujinga andika "upumbaavuu"Infact ni kwamba hakuna sector yeyote ambayo muafrika anafanya kwa weledi bila kukosea kama sector ya ujinga
Muafrika kwenye ujinga ndo anaplay part vizuri kuliko sector yeyote unayoijua wewe
Kama Mungu angekuwa anafanya kazi kama mleta mada anavyotaka then there is no point of having a brain to the human at all.
Bahati nzuri umeweka wazi kabisa "Maombi". Maombi yana majibu mawili "NDIO" au "HAPANA".
Ndio ujue HAKUNA MUNGU hapo! Ni fix tu za kale tulizolishwa na mapadri.