Tetesi: CRDB wameibiwa zaidi ya bilion 3 za wateja kwenye hacking ndio maana wakaweka siku za kujihakiki kubadili mfumo

Tetesi: CRDB wameibiwa zaidi ya bilion 3 za wateja kwenye hacking ndio maana wakaweka siku za kujihakiki kubadili mfumo

Mkuu mimi naamini kuna wizi umekuwa unaendelea kimya kimya. Nina account ya miaka mingi CRDB ambayo naweka tu kutoa ni nadra sana, tangu mwaka juzi pesa zimekuwa zikipungua bila kuwa na sababu.
Mlipuko wa sasa naona umeanza na Lipa mtandaoni ya hivi karibuni ambayo naamini hackers au wafanyakazi wa CRDB watakuwa wanahusika.
Ni ushirikiano kati ya hackers na Insider threat (wafanyakai wa benki).

Natayarisha mada hapa ya bank security na ni jinsi gani cyber security ni hatari khasa akitumiwa insider threat.
 
Kuna mtu aliniambia kilichofanya wapigwe ni baada ya watanzania wengi kutumia VPN siku za karibuni huku wanatumia app ya CRDB kwenye simu,wahuni wakatumia mwanya huo kuhack..

Nafikiri sasa hivi wafanye ukiwasha VPN usiweze kufungua Apps za Bank ,kama ilivyo Rooted phones
Is it possible?
 
Kijana hayo manamba ndo makalatasi yenyewe, kiufupi huwa wanapeleka manamba benki kuu wanapewa makalatasi mapya kutoka Uswizi then wanatuletea sisi, sasa ukiibiwa hayo manamba ni sawa na kupoteza neno siri la akaunt ya M-Pesa...
Nadhani jamaa hajajua namna books zinakua balanced, short moja inaharibi ecosystem nzima ya mahesabu.
 
Mkuu, Tanzania ni nchi ambayo Raia wake wanapenda kusikia habari mbaya mbaya na speculations tu bila kuziverfy.. hivi watu wahack benki halafu wachukue TZS Bilion 3 tu? Hao watu watakuwa stupid and not serious..

kuhack mifumo ya benk ambayo sometimes inaingiliana na mifumk ya BOT sio investment ya kitoto - ukihack ukaiba TZS 3 B basi hauna faida ya kufanya kazi hiyo..

Ninadhani kumigrate kwenda mfumo mpya kumeta disruptions kidogo na mismatch ya numbers. Kabla ya kutangaza watamigrate mbona huu wizi haukuwa speculated.. kama wangehama na mfumo ukakaa sawa hata kusingekuwa na hizi speculations...
Sure...alafu hacking ni kama emergency action....tungeona tu mtandao upo down...
Kuhack ni investment...lazma utumie pesa na watu wazito hapo bank ndio ufanikishe...sasa utoke na 3b kweli
 
Zimechotwa na mtu sio kwamba wamehakiwa kuna mtu kaingia kachota kiasi anachotaka na hawana cha kumfanya kesho anaenda kununua Gari lingine la mabillion awalingishie masikini wanaolipa kodi na wanaoweka pesa zao wanazodunduliza kwenye vibubu bank
Mifumo ya bank sio rahisi kiasi hicho...hata mkurugenzi hawez fanya kitu hiki
 
Is it possible?
VPN hili ifanye kazi lazima ichukue data zako zote, logs, browsing history, DNS queries,Data trafficking,logging details,IP addresses,location,device information, content traffic,..kibaya sasa free VPN 100% ambazo zipo Playstore or App store zinatengeneza hela kwa kuuza data za watumiaji,wanao nunua ndio watajua watatumiaje data hizo...

kamwe usifungue bank app VPN ikiwa ON,ni kosa kubwa..

Usitumie free VPN,za kulipia zipo na bei rahisi,.
 
System upgrade wamezifanya bila tahadhari hayo ndiyo matokea yake, hata TRA ishawahi kuwakuta...


Cc: Mahondaw
 
Is it possible?
Yes

Khasa pale ambapo watu wengi wanopenda vitu vya bure watumia VPN za bure.

VNP za kulipia zina strong Security.

Unapotumia VPN wawapatia data zako zote bila kufahamu.

VPN nzuri na za kulipia ni kama SurfShark, Nord VPN, na Express VPN.
 
Hii si utani ni kwamba utaratibu wa Afrika hatutaki kuaibika wakati ukweli unajulikana

CRDB wamehakiwa na kila mtanzania pesa zimeonekana kupungua kwenye account yake
Na hawajui lini itarejea ni kwamba wahuni wamepita nazo
View attachment 3471585
Britanicca
Usikute ni wale hackers waliohack mtandao wa X, walionja asali, sasa wamechonga mzinga kabisa
 
Hata kama wameiba au kuhack lakini kilichoibwa ni Namba Cash si imebaki?

Sioni tatizo labda wataalam mtueleweshe
Swali lako umeliuliza kivingine kwa kukosea maneno fulani (hizo namba ndio pesa yenyewe) ingawa upo sawa kwenye premise...; Kwamba kwenye hii mifumo lazima iache money trail kwamba lazima uki follow the money ufike sehemu ujue nani alichukua (ingawa hapo unaweza ukakuta yule aliyechukua kabebeshwa mzigo hakujua au akaunti ilifunguliwa kimagushi na huyo hayupo au aliyekwenda kutoa ni mtu ambaye identity yake imeibiwa au alishakufa) lakini all in all lazima atapatikana mbuzi wa kafara wa either kubebeshwa mzigo sio wake au kwa uzembe wake aliruhusu mwanya wa kufanyika ambayo hayakutakiwa kufanyika... Na huko tunapoelekea mfumo wa Block Chain itakuwa vigumu sana hata kuweza kubadilisha records zikishafanyika (yaani lazima utaacha tell, tell signs

Sasa tukija kwenye swali la msingi siku hizi hizo namba ndio pesa; pili kwenye FIAT currency ikifanya kazi vizuri mabenki ndio yanatengeneza pesa kwa kuweza kukopesha pesa ambazo hawana au zaidi ya zile walizonazo; hivyo wewe ukienda kukopa wanakupa pesa ambazo hawana (manamba) wewe ukienda kuzungusha kitaa na kuwarudishia unakuwa umetengeneza zile ambazo zilikuwa hazipo na wao kuwapa faida;

Pia kumbuka Banki kubwa ni too big to fail kwahio hapo ni kwamba CRDB ikitaka kufirisika Kodi zetu ndio zitatumika kuwainua...; in short huu mchoro chini unaelezea vizuri sana hii so called capitalism ya sasa ambayo ni Utapeli
1757835399988.png

Cha maana kama CRDB imechafuka sana waiuze au wajiuzie wenyewe kwa kubadilisha jina na kujifanya ni wengine wakati ni walewale ili kurudisha Imani sababu ikitokea PANIC Benki hazina pesa at any given time ya kumpa kila anayedai na Serikali lazima itaingilia kati au Uchumi huu utakufa kifo cha Mende.

NB: Hayo manamba ndio pesa zenyewe kwahio kama kuna manamba fulani yametoka sehemu fulani kwa kuwekwa kwenye akaunti feki au ya mtu aliyeshakufa na kutolewa wale ambapo manamba yalikuwa transfered kutoka kwake akija kudai itabidi Benki itafute hayo manamba kufidia na ikiwa haina hayo manamba itabidi kodi zako zifidie (Bail out) au Benki ife na ikifa nadhani sheria unaweza kulipwa kutoka Benki Kuu percent fulani tu na sio pesa zote; lakini ili kuepusha panic serikali itatumia kodi zako kuyamaliza; Ingawa hii figure sio kubwa kwahio Benki inaweza kuyamaliza na watu kufukuzwa kazi na wengine kutolewa mbuzi wa kafara...
 
CRDB ni wapuuzi mno...

Kuna ile idara ya mikopo ni tatizo na wanapenda rushwa balaa...

Unaweza kuwa umekamilisha taratibu zote za kupata hela yako tena hela yenyewe ni ya mkopo...

Lakini jamaa huwa wazito kweli kuachilia mzigo kuingia kwenye akaunti mpaka mpelekeshani na kufokeana...

Yaani hawa CRDB ni wajinga kweli kweli, huvunja Ts & Cs walizoziweka wao wenyewe..!
 
Back
Top Bottom