Tetesi: CRDB wameibiwa zaidi ya bilion 3 za wateja kwenye hacking ndio maana wakaweka siku za kujihakiki kubadili mfumo

Tetesi: CRDB wameibiwa zaidi ya bilion 3 za wateja kwenye hacking ndio maana wakaweka siku za kujihakiki kubadili mfumo

3.2B unaweza kuta ni bajeti ya kufagia na kufuta vumbi CRDB. Sio hela ya kupotea kusababisha usumbufu wa zaidi ya wiki na lawama zote hizi.

Bilioni 3 ni hela inayoweza potea hata HR wao asijue, ni hela ndogo sana kwa taasisi kubwa kama CRDB. Na taasisi kubwa hazipotezi hela ndogo. Hiyo hela imeleta wasiwasi unaoweza sababisha hasara ya mabilioni ya kutosha, kupoteza reputation, kuhamisha wateja wengi.
 
Kuna rafiki yangu mmoja kaniambia alifanya SWIFT transaction kwenda nje tangia jumanne ilopita lakini fedha haijaingia kule nje na pale kwenye akaunti yake fedha yaonekana imetoka na tozo imekatwa.

Nikamuambia awasiliane nao kufahamu yachukua siku ngapi kwa CRDB kufanya SWIFT Transactions.
 
Nadhani jamaa hajajua namna books zinakua balanced, short moja inaharibi ecosystem nzima ya mahesabu.
Tupeleke elimu ya hili suara vijijini, ona sasa hadi wataalamu wa serikali wa kibush bush hawaelewi jinsi mfumo unafanya kazi...
 
Mkuu, Tanzania ni nchi ambayo Raia wake wanapenda kusikia habari mbaya mbaya na speculations tu bila kuziverfy.. hivi watu wahack benki halafu wachukue TZS Bilion 3 tu? Hao watu watakuwa stupid and not serious..

kuhack mifumo ya benk ambayo sometimes inaingiliana na mifumk ya BOT sio investment ya kitoto - ukihack ukaiba TZS 3 B basi hauna faida ya kufanya kazi hiyo..

Ninadhani kumigrate kwenda mfumo mpya kumeta disruptions kidogo na mismatch ya numbers. Kabla ya kutangaza watamigrate mbona huu wizi haukuwa speculated.. kama wangehama na mfumo ukakaa sawa hata kusingekuwa na hizi speculations...
Sio kwamba wanapenda kusikia habari mbaya tu! Raia wengi wa tanzania na hata majority waliopo hapa JF wenye degree za vyuoni za kukariri ni Maimuna. Yaani watu wanapelekeshwa na mitaarifa ya kuokota na wanakwenda nazo. Kizazi hiki cha aina ya watu ndio wanataka kuwa kama Wa Nepal??
 
Bilioni 3 za madafu? Ni fedha kidogo kwa benki kama CRDB. Labda tatizo sasa liko kwenye kutojua ziliibiwaje na wako salama kiasi gani. Ila kwa Bongo wala hili siyo jambo la kushangaza. Tuna culture ya ku-relax na kutokuwa makini kwa kila jambo.
Point ni kwamba hiyo figure ya bilioni tatu TZS ni ndogo sana.

Ikiwa mteja mmoja tu kapoteza zaidi ya shilingi milioni 250 na CRDB ina wateja maelfu, bilioni 3 ni figure ndogo sana.
 
Yes

Khasa pale ambapo watu wengi wanopenda vitu vya bure watumia VPN za bure.

VNP za kulipia zina strong Security.

Unapotumia VPN wawapatia data zako zote bila kufahamu.

VPN nzuri na za kulipia ni kama SurfShark, Nord VPN, na Express VPN.
🙆🥹Vipi kama nina security kwenye simu kama avast ya kulipia mkuu?
 
🙆🥹Vipi kama nina security kwenye simu kama avast ya kulipia mkuu?
Kama ni Avast hakikisha watumia Avast VPN au Avast SecureLine VPN za kulipia.

Hakikisha waipata kutoka kwenye website ya Avast wenyewe na ikiingia kwenye simu yako au laptop fanya usajili kwa ajili ya subscription na baada ya hapo twende kazi.
 
3.2B unaweza kuta ni bajeti ya kufagia na kufuta vumbi CRDB. Sio hela ya kupotea kusababisha usumbufu wa zaidi ya wiki na lawama zote hizi.

Bilioni 3 ni hela inayoweza potea hata HR wao asijue, ni hela ndogo sana kwa taasisi kubwa kama CRDB. Na taasisi kubwa hazipotezi hela ndogo. Hiyo hela imeleta wasiwasi unaoweza sababisha hasara ya mabilioni ya kutosha, kupoteza reputation, kuhamisha wateja wengi.
Suala sio pesa iliyopigwa ni ndogo issue hapo ni mfumo wao uko hatarini.

Kama leo wadukuzi wamewapiga bilioni 3, vipi kesho?

Na financial report ya 2023/2024 inaonyesha CRDB walipata faida ya bilioni 551 after tax

Je, wadukuzi wakitumia hiyo loophole kuja kuchota tena watachota kiasi gani kama mifumo haiko salama?

Hilo ndilo jambo ambalo linawahangaisha kwa sasa CRDB.
​
 
Ole wao nikiwa tz nikute hata sh moja kwenye account yangu imepungua watajua hawajui, next week I will be back
 
Tunateseka kwa legacy yake, mpaka leo wewe anglia aina ya uchanguI nchini unafikiri nanai kaweka katiba ya mwaka 1977 ambao inatutesa.
Unamlaumu Nyerere bure tu. Kaweka katiba 1977, kaondoka 1985. Miaka arubaini toka mzee atoke madarakani hakuna reform yoyote ya katiba na bado unamlaumu? Kapita Mwinyi, Mkapa, Kikwete hadi Magufuli na hakuna aliyeigusa katiba, lawama unamtupia Nyerere..kweli?
 
Suala sio pesa iliyopigwa ni ndogo issue hapo ni mfumo wao uko hatarini.

Kama leo wadukuzi wamewapiga bilioni 3, vipi kesho?

Na financial report ya 2023/2024 inaonyesha CRDB walipata faida ya bilioni 551 after tax

Je, wadukuzi wakitumia hiyo loophole kuja kuchota tena watachota kiasi gani kama mifumo haiko salama?

Hilo ndilo jambo ambalo linawahangaisha kwa sasa CRDB.
​
OP ameandika wameibiwa 3.2B na ndio chanzo cha matatizo ya kuhakiki mifumo.

Suala la mifumo kuingiliwa basi wangezuia huduma au kufunga, sio kuanza kukosea mihamala au mtu kuanza kupungukiwa kiasi kwenye akaunti yake au mtu kutuma hela na isiende. Uhakiki gani huu unapoteza hela za watu. Hasara inayotokana na uko unakoita kuhakiki mifumo ni kubwa zaidi ya 3.2B mleta mada anazodai zinahakikiwa.

Mabenki yote haya NMB, NBC na nani yanaibiwa au kupoteza zaidi ya hiyo 3B kwa mwaka kwa njia ya kutatanisha, bado hujaongeza bad investments zinazopoteza mabilioni, bado hujaongeza bad loans, fraudsters na waliofirisika. Kila mwaka mabenki yanapoteza mabilioni na haizuii huduma kuendelea wala haifanyi ukitoa hela isije.

3.2B ni peanuts. Equity Kenya mwaka huu wametimua wafanyakazi 1,200 kwa siku moja kisa ujanjaujanja. Umesikia mtu akilipa hela inakatwa akaunti kisha haiendi?
 
Faida ya CRDB baada ya makato ya kodi kwa mwaka 2023 ni bilioni 422 na mwaka 2024 ni bilioni 550. Robo ya faida kwa quarter moja ni bilioni 105 (2023) na bilioni 136.2 (2024).

Walikuwa wapi siku zote kwa kweli ni swali subjective, sijui wewe ulitaka wabadili lini? Ni subjective kwa kuwa huo muda utakaoona walipaswa wawe wamebadili mfumo mwingine anaweza kuona kwamba walichelewa pia.
Hakuna benki za maana wanabadili mifumo kipumbavu kama walivyofanya hawa
 
Suala la mifumo kuingiliwa basi wangezuia huduma au kufunga, sio kuanza kukosea mihamala au mtu kuanza kupungukiwa kiasi kwenye akaunti yake au mtu kutuma hela na isiende. Uhakiki gani huu unapoteza hela za watu. Hasara inayotokana na uko unakoita kuhakiki mifumo ni kubwa zaidi ya 3.2B mleta mada anazodai zinahakikiwa.
Unafikiri ni kwa nini hizo changamoto zinajitokeza?​
 
Back
Top Bottom