Damas Ndumbaro: Marufuku kuvaa jezi ya Mamelodi au Al Ahly kwa Mkapa kwenye michezo ya Simba na Yanga
Dah mawaziri wengine viazi kweli,
Yeye kama hajui raha ya soka aache kuongea nonsense
Kama waziri hapo moja kwa moja ameongea kauli za kutaka serikali isipate mapato kutokana na viingilio vya mashabiki,
Fans wa simba wenye uzalendo wa kuishangilia yanga ni wachache na hata Fans wa yanga wenye uzalendo wa kuishangilia simba ni wachache..
 
Yaani wameshatupangia jinsi ya kuwa maskini na hata furaha kidogo tunayotaka kuipata kupitia mpira wanataka pia kutupangia jinsi ya kusherehekea. Hivi unawezaje kulazimisha watu wawe wazalendo?? uzalendo ni kuvaa au kutokuvaa jezi kweli??
 
Hilo bomu analolitengeneza atajuta

Kuvaa hizo jezi haitozuia Simba /Yanga kushinda,kufungwa au kusuluhu

Mchezo ni uwanjani, hizo jezi hazina cha kufanya na hata hiyo solidarity forever haipo basi tu

Kwa hiyo tuanze kukagua shabiki mmoja mmoja passport, like serious?

Waziri katoa boko, kama anataka kutumia hii platform kupanda chati kisiasa kafeli
Huyu Waziri huwa HAJUI kabisa kuzungumza Kuna siku nilimsikia UFM kuhusu lile sakata la Katibu wa Mpira wa Netball, dah nilimuona uwezo wake wa kupambanua mambo ni mdogo sana, hata hiyo PhD yake inafikirisha sana yaani 😂😂😂
 
Hapa ndio nimeamini media zetu zimejaa unafiki. Sijaona mtu aliye challenge zaidi ya kujifichia kwenye uzalendo. Haya yangezungumzwa na msemaji au kiongozi wa team ungeuona moto
 
Ukija uwanja wa Taifa ukiwa umevaa jezi ya Mamelodi Sundowns lazima utuoneshe passport ya Afrika Kusini na ukiwa na jezi ya Al Ahly utuoneshe passport ya Misri, nje na hapo Polisi watakuchukua ukapumzike” Damas Ndumbaro, Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Yapi maoni yako?

Tunashangilia timu kwa kulazimishana?

Waziri kavunja katiba halafu kavunja haki za binadamu.

Kwenye kubeti nako atalazimisha watu wabeti upande upi? 🤣🤣🤣
 
Tunashangilia timu kwa kulazimishana?

Waziri kavunja katiba halafu kavunja haki za binadamu.

Kwenye kubeti nako atalazimisha watu wabeti upande upi? 🤣🤣🤣
Kuna kipindi serikali inatakiwa iwe na ubabe ili usijisahau.
 
Back
Top Bottom