Dar: Amchoma mpenzi wake na Petroli kisa wivu wa mapenzi

Dar: Amchoma mpenzi wake na Petroli kisa wivu wa mapenzi

Watoto watateseka sana. Baba hayupo na mama hayupo. Who gonna take care of them? Inaumiza sana.
...Watateseka Sana. Kwa tunavyowsjua ndugu watakaowachukua na kukaa nao, mtoto akikosea kidogo tu utasikia..."usinisumbue! Mama na mama yako wameuana huko unataka kuniletea Shida mimi!"

Ndugu wa kiafrika waone hivi hivi...
 
Muda mwingine akili ituongoze kuliko hisia.

Imagine, umemchoma moto mwenzako na kumuua, wewe utaozea jela kwa maumivu makali.

Umefaidika nini sasa? Kwenda kufia jela ndiyo faida?

Aisee!.

Nimewaandikieni ninyi mtaokaosoma hapa.
Kuna mwanamke alimuua mchepuko wake kwa visu. Kapelekwa mahabusu ndani ya wiki tu anaanza kujuta.
Ni miaka mitano iliyopita. Bado yupo huko lupango ,,natumai sasa kazoea hayo maisha.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Noma sana mkuu reaction ya mwanamke mpumbavu ni disaster!

Alichoma nyumba ndani mna mpangaji kalala na mwanae,nje duka la spare za pikipiki ndani mna jamaa hiyo jana aliingiza pikipiki mpya na mlikuwa na store ya mtu kajaza mzigo wa dagaa vyote vimeteketea Mungu saidia huyu dada mpangaji alitoka salama ila huyu dogo akawa muhanga,mpaka sasa hivi panafuka moshi yote ni mal@ya mmoja kasababisha.
Mama suraiiya
 
Siku zote huwa nawaambia watu maneno haya ila wanaona kama utani. Asante Mshana umeliona kwa jicho lingine. Kifupi majeruhi wa moyo sio wa kucheza nae. Kama unaigiza bora usepe mapemaaa
Nadhani ni Sawa na yule aliyechomwa na mkaa.. au sio??

Ila binafsi naona wote wamekosea sana maana baada ya hapo atajuta na atamkumbuka alie muua kwa mateso sababu yapo mazuri walivyofanya pamoja pia mpaka wakachaguana yani
 
Mkuu ni makabe eneo gani hilo?? Maana asbh nimepita hapo sijaona wala kusikia. Nakuja kuona status tu wanazengo wanapost
Makabe ukipita barabara ya Madukani jirani na zilipo office za serikali ya mtaa maarufu wanapaita kwa Washa.

Nyumba ipo barabarani kabisa.
 
Back
Top Bottom