Dar: Amchoma mpenzi wake na Petroli kisa wivu wa mapenzi

Dar: Amchoma mpenzi wake na Petroli kisa wivu wa mapenzi

Siku zote huwa nawaambia watu maneno haya ila wanaona kama utani. Asante mshana umeliona kwa jicho lingine. Kifupi majeruhi wa moyo sio wa kucheza nae. Kama unaigiza bora usepe mapemaaa
Yanatokea kama hayo ndio unasikia povu la lawama.
Kuwa mtulivu na ndoa yako.Ulioa kutafuta nini kama unafahamu huwezi kujizuia.

Uzinzi hauna huruma na mapigo yake huwa makali mno,ukiona tu umechepuka jiandae na lolote siku umemaliza kula mzigo.Weka akilini kuwa mambo moto moto yanakuja mbeleni kukumaliza.Tuache kabisa unafiki wa mambo mepesi ya mchana.

Hakuna na haitotokea usaliti wa ndoa ukawa mwepesi.

Ukila cha mwenzio unaliwa cha kwako,na mkienda mbali ni zaidi ya haya tunayo yaona leo.
 
Sometimes tuzitafakari kwa makini hizi scenarios

Unakutana na binti ya watu.. Ana ndoto zake .. Mnayajenga na kuingia kwenye ulimwengu wa mahusiano mpaka ndoa
Anakusaidia kwa mengi mno unamtumia mpaka kusikofaa kutumika kiutu.

Unamharibu na kumharibia mengi.. Ila kwakuwa wewe ni wake anaridhia kiroho safi kabisa na bila kinyongo

HALAFU unakuja kumletea zinazomchoma moyo na kumuumiza hisia...! Muogope sana mwanamke aliyejeruhiwa
Siku zote Ubongo unatakiwa kuongoza mihemko, the vice versa is always disaster,
Hakuna kitakachojustify hiyo mihemko ya huyo mwanamama, ametumia mihemko pasi ya kushirikisha ubongo and they both lost.
Tupende kwa moyo huku tukishirikisha ubongo wakati wote .
 
Mental case huyu sio wa kupeleka jela.. ni psychopath. Tuwape upendo wale tuwapendao unapoumiza hisia za mtu mwenye psychopath traits ndio hiki kinachotokea.

Mpatie upendo yoyote aliyekaribu yako, upendo ndio tiba pekee kwa psychopaths. Ukichunguza maisha ya huyo mdada akiwa udogoni lazima ukute alipitia mateso kwa alokua anaishi nao
 
Japo amekosea ila tujiulize.....

Imekuwaje hadi amefikia kumchoma mumewe aliyemchagua mwenyewe moto.

Wanaume "baadhi" epukeni kuwaumiza wanawake na Kisha kupuuza kumaliza migogoro, kwa kudhani huo ndio uanaume.

Mnawajaza hasira na hawana kwa kutemea nyongo. Mwisho wa siku wanafanya maamuzi ya kustaajabisha.

Wanandoa na nyie mkiona vurugu ni nyingi kuliko amani achaneni kila mtu aendelee na maisha yake. Acheni kuvumilia mnavyoona hamuwezi kuhimili.

Hakuna kaburi linaloandikwa "Aliolewa" au "Alioa" ni alizaliwa tarehe.... Na kafariki tarehe.....

Acheni upuuzi wa kuwaza jamii itauonaje tukiachana anzeni kuwaza tukiendelea kuishi kwa kuumizana mwisho wake nini!?

Ona sasa watoto wanakosa malezi ya baba na mama.

Wakati wangeachana watoto wangeweza kuendelea kuwaona wazazi wao hata kama ni kwa utaratibu maalum.
Ninachowapendeaga wanawake wao wapo sawa muda wote, yule jamaa wa kigamboni aliyemuua mke wake na kumchoma alilaumiwa sana na sasa huyu mwanamke aliyemuua mume wake bado wanalaumiwa wanaume. Strange World!!
 
Pole yake marehemu. Lakini alishindwa nini kung'amua hatari iliyopo mbele yake iwapo alishakoswa koswa na petrol mara ya kwanza kama mwanajamvi mmoja alivyoeleza kwenye huu uzi? Pia marehemu alishindwa nini kujua mapema kama ana "date" na kichaa kabisa? Huyo mwanamke kwangu mimi ni kichaa kabisa ni wale machizi fresh ambao wapo wengi wa kike na kiume huku mitaani. Mpaka kufikia kuchoma nyumba ni lazima huyu mwanamke alishafika levo za kuongea mwenyewe kwa sauti na lazima alikuwa anataja jina la merehemu na kujiapiza mara nyingi tena kwa ubaya. Kama marehemu na watu waliokuuwa karibu naye walichukulia poa basi matokeo ndiyo hayo.

Kwa binadamu mwenye akili timamu hawezi choma nyumba ambayo ina wapangaji wengine ndani tena tunaambiwa hapa mama na mtoto walikuwa ndani chumba kingine wakatoka salama, kuna fremu ya fundi piki piki na duka la dagaa achilia mbali hasara aliyompa mmiliki wa nyumba. Mtu ambaye amewapa hasara zisizo na fidia wenzake waliodunduliza kupata mitaji kisa huyo Mario wake aliyekuwa anampa bia za bure huyo sio mzima wa akili na ni mbinafsi kwa kiwango cha juu.

Angalizo kwenye mahusiano; ukiwa mme au mke ukiona mbele hakuna mwanga basi chukua maamuzi magumu ya kuondoka au kuachana bila kujali mali, vitega uchumi na muda uliowekeza kwani uhai ni mali zaidi ya hivyo vyote. Ukipuuza na kuona ngoja nivumilie au watu watasemaje basi ndiyo hayo ya petroli na gunia za mbili za mkaa yatakukuta.
 
Back
Top Bottom