Dar es Salaam ili uende kazini na kurudi lazima uandae elfu 10 ya usafiri pamoja na chakula. Maskini hana chake hapa nchini

Tupige hesabu za mtu anayetumia gari ndogo tu inayokula wese la kawaida tu, say 1.3L engine. Mtu huyu anaendesha 50km kwenda kazini na kurudi kila siku. Gari inakula walau 1L kwa 10-12km/hr kwa wastani. Huyu mtu anahitaji kila siku kuweka wese angalau 5L x 3150 = 16,000 ≈ 20,000...hapo ameenda na kurudi, hajapata mishe yoyote ya kuongeza km.

Mwanzo tuliona wanaomiliki pikipiki hawajielewi, leo hii naona wao ndio wanafurahia maisha. Nasikia 1L inaweza kutembea hadi 60km sijui kama kuna ukweli hapo.
 
Naandika hii mada nikiwa na uchungu moyoni.

Sasa hivi nina miezi kama 4 hivi natumia Daladala kwenda na kurudi kazini na mara chache, tena chache sana huwa natumia bodaboda kazini mpaka home, home mpaka kazini.

Kutoka Nyumbani mpaka kazini nikipanda bodaboda direct ni elfu 15. Go and return inalala 30000 sh
Nikipanda bodaboda 1500 sh. mpaka kituo cha Daladala na nikipanda Daladala moja mpaka kazini awali nilikuwa natumia 1000 sh. Jumla 2500 sh, kwenda na kurudi natumia sh. 5000 kamili, nikipanda gari mbili nilikuwa natumia kama elfu 6 hivi. Pesa ambayo himilivu kwangu.

Ila sasa nikipanda Daladala itanilazimu nitumie takribani 7000 kwenda na kurudi.

Hapo ukiweka na chakula na maji around 5000.

Kwahiyo Mimi tu inabidi nitumie angalau elfu 12 kwaajili ya kazini. Familia kwa sasa hali ilivyo kwa siku ni sh. 10 -20 hapo mahitaji yote muhimu kama gas, mkaa, chumvi , Michele na unga viko ndani. Kama havipo lazima uangushe 20.

Kwahiyo inanilazimu kwa siku nitumie kuanzia elfu 30.

Vipi kwa anayelipwa laki 2.5 au laki tatu kwa Wahindi?

Vipi anayelipwa elfu 7 kiwandani kwa siku?

Kipato changu kidogo nahisi kupata msongo wa mawazo.

Serikali ipunguze nauli, watu wanashindia mihogo makazini Ili kubana nauli za kurudia nyumbani jioni.

Hakuna mtumishi wa umma au mwajiriwa wa sekta binafsi Dar es Salaam anaweza kununua kiwanja center labda awe fisadi. Wengi tunajuchanga tunapata viwanja Chanika, Bagamoyo, Kisarawe, Pugu n.k.

Kwa nauli hizi Ili ugeuke na gari upate seat lazima ujipange. Unakuta kila ukipiga hesabu 20 imeenda kwa usafiri na misosi.

Umaskini utaendelea kutupiga maana hatuna mtetezi.
Maajabu eti Tegeta Nyuki Kariakoo imeongezeka Tsh 200, na Mbezi nyuki pia, na Dar morogoro now tsh. 15000 kutoka elfu kumi
 
Naandika hii mada nikiwa na uchungu moyoni.

Sasa hivi nina miezi kama 4 hivi natumia Daladala kwenda na kurudi kazini na mara chache, tena chache sana huwa natumia bodaboda kazini mpaka home, home mpaka kazini.

Kutoka Nyumbani mpaka kazini nikipanda bodaboda direct ni elfu 15. Go and return inalala 30000 sh
Nikipanda bodaboda 1500 sh. mpaka kituo cha Daladala na nikipanda Daladala moja mpaka kazini awali nilikuwa natumia 1000 sh. Jumla 2500 sh, kwenda na kurudi natumia sh. 5000 kamili, nikipanda gari mbili nilikuwa natumia kama elfu 6 hivi. Pesa ambayo himilivu kwangu.

Ila sasa nikipanda Daladala itanilazimu nitumie takribani 7000 kwenda na kurudi.

Hapo ukiweka na chakula na maji around 5000.

Kwahiyo Mimi tu inabidi nitumie angalau elfu 12 kwaajili ya kazini. Familia kwa sasa hali ilivyo kwa siku ni sh. 10 -20 hapo mahitaji yote muhimu kama gas, mkaa, chumvi, Michele na unga viko ndani. Kama havipo lazima uangushe 20.

Kwahiyo inanilazimu kwa siku nitumie kuanzia elfu 30.

Vipi kwa anayelipwa laki 2.5 au laki tatu kwa Wahindi?

Vipi anayelipwa elfu 7 kiwandani kwa siku?

Kipato changu kidogo nahisi kupata msongo wa mawazo.

Serikali ipunguze nauli, watu wanashindia mihogo makazini Ili kubana nauli za kurudia nyumbani jioni.

Hakuna mtumishi wa umma au mwajiriwa wa sekta binafsi Dar es Salaam anaweza kununua kiwanja center labda awe fisadi. Wengi tunajuchanga tunapata viwanja Chanika, Bagamoyo, Kisarawe, Pugu n.k.

Kwa nauli hizi Ili ugeuke na gari upate seat lazima ujipange. Unakuta kila ukipiga hesabu 20 imeenda kwa usafiri na misosi.

Umaskini utaendelea kutupiga maana hatuna mtetezi.
Ukiona watu wanaamka saa tisa za usiku kutembea kwenda kazini, hawajapenda, wanaokula mihogo ya kuchoma ya jero mchana na Maji ya Mia hawajapenda, Lakini Viongozi wetu wana posho za kutosha kuwalisha watu wote wa Tanzania, Mlo wa mchana na usiku lakini wameamua kuchumia matumbo yao kwanza na hata milele.
 
Sema na kuishi mbali sana jau,
Hapo mkuu kama hio ratiba ni kweli nakuonea huruma,

Sometimes tunakimbilia viwanja vya bei rahisi ila mara mia ulipe pesa kubwa upate sehemu nzuri sio kujificha huko porin
Kabisa Mkuu kukaa mbali jau, sema kuna sababu nyingi mtu kukaa mbali. Ila yote kwa yote kwa foleni za Dar na miundombinu ya hovyo ukikaa mbali kuna cost implications nyingi.

Mimi natumia wastani wa 30 to 40min niko city centre.. pamoja na kuwa natumia gari kubwa above 3000cc ila sioni gharama sana maana nime balance kati ya muda wa kusafiri, gharama ya makazi na gharama ya kuendesha gari.

Kupanga ni kuchagua!
 
Maisha ni kuchagua. Kuna ambaye anang'ang'ania kukaa mjini huku akipambania mlo tu hana uwezo wa kufanya savings yoyote, na kuna anayekaa bushi ambaye mlo kwake ni wa uhakika na ana savings ya kufanya maendeleo.

Endeleeni kung'ang'ania mjini tu. Mtakumbuka shuka kukiwa tiyari kumeshakucha
 
Kweli mkuu mfano watumishi wa umma wanaoishi mikoani haswa miji midogo huwa wana nafasi ya kufanya maendeleo kuliko walio mjini kutokana na gharama za maisha
 
Back
Top Bottom