Dar inaongoza vijana watu wazima kuishi kwa wazazi wao

Tatizo nililoliona mimi vijana wengi wa dar wanasumbuliwa na uoga uliopitiliza anajua akienda kupanga ipo siku kodi itamshinda, mimi mwenyewe nilikuwa naishi home ila nilithubutu kwenda mbali na nyumbani ila ni maeneo ya hapo hapo dar nilikuwa sichagui kazi maisha yalienda flesh tu.
 
Mm naamini vijana wengi wanaotoka nyumbani kwao ni kutokana na kadhia za wazaz na wengine wanataka uhuru wa kuwa na mademu zao..Mm naamini kitu kimoja! Hakuna mzazi anaependa kumuona mtoto wake anapata tabu kama eneo la kuishi linakuwepo! Ila kinachofanyika ni kwamba ww kama mtoto unatakiwa ujipange kuanzia hapo, tafuta kazi ya maana ata ambayo inakuingizia elfu 5 kwa siku..mm naamini as long as huna gharama ya kulipa kodi kwa mwezi..hakikisha unajipanga vzr sana.ili ukitoka apo kwa wazaz unanyumba yako nzuri tu
 
Halafu MAZA anasema hatutaki kuoa
 
we ndio mshamba wapo kibao wanaotoka dar na kuja mikoani..tena ni matajiri ref;Hamza msomali alitoka dar akaenda chimba madini chunya.....nenda mashambani iringa na mbea igunga kwenye mpunga wapo wengi wasomi wanatoka na kuja kuzifuata fursa mikoani...wajinga jinga na maskini ndio wanakomaa hapo na kuishi kisanii...
 
Ahya poa.
 
unaishi kwenu na mume wako?
 
unaishi kwenu na mume wako?
πŸ™„πŸ™„πŸ™„πŸ™„πŸ™„ Bro mimi kidume bhana nimeoa naishi na mkewangu.
Hapo ni typing error nina mke sio ni mke.
Mimi ni mtoto pekee wa kiume katika familia yetu yenye watoto watatu.
 
Kukaa Bure huwezi pata akili
 
ila hiyo ya kuzalia nyumbani duh

kwa kijana wa kike kukaa nyumbani akiwa kwenye 30s huko ni vibaya?
Kwa kijana wa kike kama ramani hazijasoma vizuri, hakuna ubaya wowote wa yeye kuwa nyumbani hata kama atakuwa na 30+ years.

Ikiwa life sio zuri sana nyumbani anaweza akajipambania akiwa anatokea nyumbani, badala ya kujifanya shupavu kujitegemea kwa njia za udangaji.
 
Unajua bro inategemea unajiwekaje hapo nyumbani.
Ukiwa kijana wa hovyo,dira hauna,direction ya maisha hauna hata mawazo chanya ya kimaisha hauna pia hata kupambana haupambani wazee wakifungua mlango wanaweza ona beberu kalala kitandani kumbe kijana wao Moses.
Ila ukiwa una malengo yako na unayatimiza na pia unai handle familia pale inapohitajika kwa familia zetu hizi waonekana mtu wa umuhimu ni ngumu wao kukuruhusu utoke home.
Mimi mpaka naoa nimeoa niko nyumbani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…