Uchaguzi 2020 Dar: Jeshi la Polisi lasitisha wito wake kwa Tundu Lissu, lamtaka aendelee na Kampeni zake

Kwani RPC wa Kilimanjaro alimuandikia Lisu barua? IGP Siro na hao wa Kanda maalum ndiyo walijitia kimbelembele.
 
Kura kwa Lissu!
 
Hii ni picha halisi ya jinsi ambavyo taasisi hii muhimu ya kimabavu (polisi) kuwa wana mapungufu mkubwa ya kisheria katika kushughulikia issues zinazohitaji weledi wa kisheria...

Hii ni ishara kuwa watu wengi wameonewa na polisi kwa kuwa tu polisi wao wenyewe hawazijui sheria zinazoongoza utendaji kazi wao....!!

Hii ni crisis inayohitaji kushughulikiwa haraka ili kufikia maendeleo ya haraka na ustawi wa jamii ya watanzania...
 
kama nime elewa vizuri wito bado uko pale pale ila anatakiwa kuripoti mkoa wa kipolisi Kilimanjaro, na hii ni Zaidi ya ngonjera ya policcm

Huo wito wa Kilimanjaro kuna barua?
 
Sasa asingeipokea haya madubwasha tungeyaona wapi?
Imagine barua muhimu kama hii anaandika secretary halafu hakuna mtu mwingine anaeipitia kuangalia kama ina makosa!Yaani barua anaandika msaidizi wa ofisi halafu anapelekewa boss kusaini halafu boss anasaini tu bila hata ya kuisoma yaani!Jeshi la polisi linatakiwa likaguliwe vyeti
 
Jeshi la polisi hapo nawapongeza sana kwa kuweka busara mbele. IGP Sirro acha kumtetea Magufuli anayevunja sheria ovyo kwa kutukana na kutishia wananchi kuwa hatawaletea maendeleo wakimchagua mtu asiye wa CCM. Hivi NEC hamuoni hili kama ni kosa???? NALIPONGEZA JESHI LA POLISI KWA BUSARA MLIYOONYESHA. Bado huyo DPP anayefungwa watu wasio na makosa kwa sababu ya chuki aliyonayo juu ya CHADEMA.
 
jeshi ambalo wanachi waliishalichukulia ni la hovyo halijali hizi filimbi.

wewe ndio utaona unaliabisha,wakati wenyewe hata habari hawana.
Linazidi kukosa thamani na heshima mbele ya watanzania!
Yaani mpaka watu wakiwaona polisi wanajua ni watu wa mabavu wasio na akili!
 
Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana. Warumi 12:19

Naamini kwa moyo wangu wote kwamba Mungu anaenda kukupa nafasi ya kuongoza nchi yetu ya Tanzania. Hakuna aliyejua kuwa Daudi angeweza kumwangusha shujaa Goliathi, ila Mungu alimsaidia Daudi.

Kati ya mambo makubwa aliyofanya Daudi ni kutokulipa kisasi kwa watesi wake. NAKUPA ONYO KALI, Usije kulipa kisasi kwa watesi wako, Jitahidi utakapoingia madarakani umweshimu mzee Magufuli wala usiwaze kumtendea baya lolote. Hata ikiwezekana mwachie ndege moja ili awe anaenda nayo kwenye uwanja wa Chato. Usimnyanyase wala kumtenda vibaya.

Hata hao jesi la polisi usiwafanyie chochote kibaya, kwa ghadhabu, wewe tengeneza mfumo mzuri wa jeshi la polisi la kisasa ambalo halijihusishi na siasa wala ukandamizaji wa raia.

Maendeleo yana chama kwa mujibu wa JPM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…