Dar: Mvua kubwa sana imenyesha usiku wa kuamkia leo 21/01/2024

Hata kwenye kipindi hiki cha maafa ya mafuriko tutarajie wajanja kupiga hela za maafa. Hii nchi ngumu sana.
 
Nchi imefunguka, mama anaupiga mwingi sana.
Asante serikali kwa kutuletea mvua. Wakulima wa mpunga walikuwa wameanza kulalamika kukosa maji. Pia wananchi wasiokuwa na huduma ya maji ya DAWASA leo wamepata maji ya bwerere.

Asante sana Rais Samia, unaupiga mwingi mama yetu. Mungu akubariki na kukutunza.
 
Wako bize wakiandaa pongezi kwa Samia na CCM.
 
Tuacheni utani bora makao makuu yabaki Dodoma sema wamechelewa kujenga ...Ukitumia akili Dar pale kati ni bondeni kabisa haswa jangwani hata ukiangalia barabara kwa huku magomeni unaona pale ni bondeni kabisa...

Dodoma huwezi kukuta huo ujinga wala mvua kubwa kiasi hiki..


Dar sehemu nyingi ni overrated haswa madalali eti wanauza viwanja bei juu huko Tegera na Madale ni hovyo kabisa
 
Hii la mvua litapita. Dar itabaki na unyama wake.
 
Kuna sehemu mtu umeishi miaka 6 maji hayajawhi kuingia,leo maji hadi yanafunika gari
Hii mvua kali tu kiukweli tusije kulaumu saaana serikali.

Na ukiongeza natural drainage ya dsm ilivyo mbovu, bado makazi yanaiingilia matokeo ndo haya.

Kwa wanaokaa mlandizi mvua kama hio ilipiga wiki moja imepita, upepo mkali hadi unasikia paa linanyanyuka, lkn maafa hayakuwa serious
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…