Mtihani kwa serikali ya mkoa wa Dar es Salaam kuwa na viongozi wabunifu, badala ya kuwaza kuzuia maandamano ya tarehe 24 January 2024
View attachment 2878042
Picha : RC Albert Chalamila mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam
Kingo za mito na vijito vinaweza kabisa kuimarishwa na kuzuia majumba ya wakaazi wa Dar es Salaam kuanguka kutokana na maporomoko ya kingo za mito
Picha ikionesha kingo za mifereji, vijito ilivyoliwa jijini Dar es Salaam na kupelekea makalavati, madaraja kujaa mchanga
View attachment 2878040
Wanafunzi wa kitivo cha uhandisi chuo kikuu tajwa kongwe UDSM kwa kushirikiana na halmashauri ya Ubungo TAMISEMI wangeweza kutumia kodi za wananchi vizuri na wanafunzi wa UDSM kujifunza kwa vitendo kujenga kuimarisha kingo za mifereji, vijito na mito ya maji hatimaye majina yao kuingia ktk rekodi kumbukizi tukuka kuwa elimu imewezesha kutatua changamoto katika jamii .
Picha chini toka maktaba ikionesha changamoto endelevu zinazolikabili jiji na pia mkoa wa Dar es Salaam
View attachment 2878039