Dar: Tozo za Daraja la Nyerere Kigamboni zimeshuka

Dar: Tozo za Daraja la Nyerere Kigamboni zimeshuka

Kinacho nifurahisha kwa hii serikali ya Ccm ni pale wanapo fanya maamuzi ya kuboronga na kuwaumiza raia halafu wakisha kosolewa wakirekebisha bado watajisifu badala ya kuomba radhi.. Funny Ccm.
Ndio dalili ya kukomaa kisiasa, CCM ni samaki mbichi, anarekebika kutokana na mahitaji ya jamii.

Hata katiba mpya mnayodhani itawabeba, CCM itaji camouflage na ita fit kuliko hata wanaoipigania.

If you can't change, the change will change you.

Hata vyama vingi vya siasa, CCM iliona isivutane navyo, ikaweka strategy ya kuvikaribisha, halafu Ika inflitrate vyama hivyo na kuviendesha kutoka back door.

Wafalme wa vyama hivyo wote Sasa wamelegeza nati na kurudi kwa muajiri wao CCM...Mrema, Lipumba, Nyaucho and the likes
 
Rais Samia Suluhu na Mbunge Faustine Ndugulile wamevunja kikwazo kigumu kabisa Cha maendeleo ya kigamboni.

Sasa tozo zimeshuka na zitalipwa kwa siku badala Kila mtu anapovuka

Hiki kilikuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya kigamboni. Kigamboni ikianza kujengwa itakuwa mji mzuri sana na utaibadilisha Dsm.

Habari zaidi ukurasa wa Instagram wa mbunge..

Ni miaka michache tu iliyopita, wananchi masikini na wanyonge waliambiwa waogelee, lakini mama kaonyesha kwamba yeye kwa hakika ndiye Rais wa wanyonge na masikini

Pia soma;

1). Watu wa Kigamboni tudai haki yetu ya kutumia daraja bila tozo sasa muda ndio huu
View attachment 2235011View attachment 2235012View attachment 2235013
kwenye daladala za abiria 15-40 hapana bado pesa kubwa elfu20 kwa siku hapana hapana bora wangefanya elfu2 kwa kila trip
 
Hivi karibuni Serikali ya Rais Samia Suluhu imefanya jambo kubwa sana lakini kama vile watu hawaoni, wanasubiri tu pale mambo yanapotindinganya waje kutupa lawama. Ni hivi, Serikali ya Rais Samia hatimaye imesikia vilio vya muda mrefu vya wakaazi wa Kigamboni, na wamiliki wa vyombo mbalimbali vya moto juu ya gharama za kuvuka katika daraja la Nyerere.

Daladala, magari binafsi na vyombo vingine vya usafiri kama pikipiki na bajaji, walikerwa sana na gharama kubwa katika kuvuka darajani hapo. Daladala zilikuwa zinalipa Sh. 5000 ili kuvuka, kwa hiyo kama atavuka kwenda na kurudi basi atalipa Sh. 1000. Dereva mmoja wa daladala alikiri kwamba hapo awali siku nzima walilipa Sh. 100,000 hadi 120,000, hiyo iliwaumiza sana ukizingatia kwamba hapo bado pesa ya bosi, mafuta na matengenezo madogo madogo.

Hivi sasa kubwa nzima madereva wa daladala wanasema walipia 40,000 kwa kutwa. Jamani, kwa hili hatuna budi kuipongeza sana na kuishukuru serikali ya Rais Samia Suluhu. Bajaji hupakiza watu watu watatu kisheri. Hapo awali mtu mmoja alitozwa 500 kama nauli na kutoka Kigamboni darajani hadi Chuo Cha Uhasibu. Kama mtu mmoja atalipa 500/-, na darajani bajaji ilitozwa 1500/- hivyo watu wa bajaji ilikuwa hawapati faida hata kidogo. Hivi sasa bajaji zinatozwa Sh. 500/- tu, vipi hapo wadau kuna kelele tena?

Watu wa pikipiki wametoka kulipia 600/- hadi 300/-. punguza la 50%. Nimetembelea eneo la Kigamboni nimeongea na watu wale, hakika sura zao zinafuraha sana, na wameridhika sana na maamuzi ya Serikali ya Rais Samia.

Tozo daraja copy.jpg
 
Kwani hilo daraja limejengwa kwa hela kutoka mfukoni mwa mtu? Kuna sababu gani ya kuwatoza wananchi wapitapo kwenye hilo daraja? Mbona kwenye madaraja mengine hakuna tozo?
Swali zuri sana. Daraja la Kigamboni lazima watu walipie kufidia gharama za mfuko wa NSSF ambao fedha zake ndio zilitumika katika ujenzi wa daraja hilo.
 
Swali zuri sana. Daraja la Kigamboni lazima watu walipie kufidia gharama za mfuko wa NSSF ambao fedha zake ndio zilitumika katika ujenzi wa daraja hilo.
Sasa si suala tu la serikali kuwafidia hao NSSF ili wananchi wapite pasipo kutozwa malipo! Mbona kuna madaraja mengi tu nchini wananchi wanapita bila kulipishwa chochote!

Mimi naona hao watu wa Kigamboni hawatendewi haki hata kidogo.
 
Hivi karibuni Serikali ya Rais Samia Suluhu imefanya jambo kubwa sana lakini kama vile watu hawaoni, wanasubiri tu pale mambo yanapotindinganya waje kutupa lawama. Ni hivi, Serikali ya Rais Samia hatimaye imesikia vilio vya muda mrefu vya wakaazi wa Kigamboni, na wamiliki wa vyombo mbalimbali vya moto juu ya gharama za kuvuka katika daraja la Nyerere.

Daladala, magari binafsi na vyombo vingine vya usafiri kama pikipiki na bajaji, walikerwa sana na gharama kubwa katika kuvuka darajani hapo. Daladala zilikuwa zinalipa Sh. 5000 ili kuvuka, kwa hiyo kama atavuka kwenda na kurudi basi atalipa Sh. 1000. Dereva mmoja wa daladala alikiri kwamba hapo awali siku nzima walilipa Sh. 100,000 hadi 120,000, hiyo iliwaumiza sana ukizingatia kwamba hapo bado pesa ya bosi, mafuta na matengenezo madogo madogo.

Hivi sasa kubwa nzima madereva wa daladala wanasema walipia 40,000 kwa kutwa. Jamani, kwa hili hatuna budi kuipongeza sana na kuishukuru serikali ya Rais Samia Suluhu. Bajaji hupakiza watu watu watatu kisheri. Hapo awali mtu mmoja alitozwa 500 kama nauli na kutoka Kigamboni darajani hadi Chuo Cha Uhasibu. Kama mtu mmoja atalipa 500/-, na darajani bajaji ilitozwa 1500/- hivyo watu wa bajaji ilikuwa hawapati faida hata kidogo. Hivi sasa bajaji zinatozwa Sh. 500/- tu, vipi hapo wadau kuna kelele tena?

Watu wa pikipiki wametoka kulipia 600/- hadi 300/-. punguza la 50%. Nimetembelea eneo la Kigamboni nimeongea na watu wale, hakika sura zao zinafuraha sana, na wameridhika sana na maamuzi ya Serikali ya Rais Samia.

View attachment 2235810
Kama ni kweli basi naungana na wenzangu wa kigamboni kuifurahia huduma hii
 
Swali zuri sana. Daraja la Kigamboni lazima watu walipie kufidia gharama za mfuko wa NSSF ambao fedha zake ndio zilitumika katika ujenzi wa daraja hilo.
Lakini hata huo mfuko wa NSSF mbona ni Sisi ndio tunaotozwa fedha zetu halafu tunalipwa huo mkupuo kiduchu hatulalamiki. Sasa iweje wao watutoze tena tozo kwenye fedha yetu?
 
Swali zuri sana. Daraja la Kigamboni lazima watu walipie kufidia gharama za mfuko wa NSSF ambao fedha zake ndio zilitumika katika ujenzi wa daraja hilo.
Pongezi Kwa Rais.

NSSF walikuwa wanatunyonya sana bora tozo imeshushwa
 
Wananchi wa Kigamboni walikuwa wanataka wapite hapo darajani bure kwa kuwa madaraja yote hapa Tanzania kupita ni bure.
Sasa kusema tozo ya kupita darajani imepunguzwa hivyo watu wafurahi, huo utakuwa ni ujinga na upuuzi. Hiyo ni sawa na Mwanaume mwenye njaa anataka ugali, halafu wewe unampa pipi kama mbadala wa Ugali, kisa pipi ina ladha tamu!

Sisi wakazi wa Kigamboni tunataka tozo ya kuvuka daraja itolewe kabisa, hatuitaki.
 
Unamshukuru mtu kwenye vitu vya msingi ambavyo anapaswa kukufanyia? Kwani hii nchi ni mali ya CCM? Haki zako ni zipi? Unajitambua?
 
Ningelikuwa na mamlaka nchi hii hilo daraja wa kazi wa kigamboni wangelipita free, Hakuna haja ya kuwa na tozo za kuvuka hapo, Serikali ni wajibu wake kutengeneza miundo mbinu bora kwa wananchi wake ili wawe salama pia kuchochea maendeleo na unafuu wa maisha, Hayo mambo ya tozo naona yangelibaki kwenye Panton tu. Au wana jamvi nakosea?

Likiwa Free ina maana kwenye Pantoni kivukoni mapato yatapungua.
 
Hii ni danganya toto, magari yaliyo mengi yalikuwa yanalipa 1,500/=, na sasa yataendelea kulipa 1,500/=, pia kwanini mnalazimisha watumiaji wawakooeshe pesa mkae nayo wiki au mwezi ndio aitumie?
 
Zitaisha lini???inamaana hadi leo hilo deni halijaisha tu naona mpaka tufe watakaokuja ndio wataenjoy kupita bure!
 
Back
Top Bottom