DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

Mwendokasi wa mbagara gerezani utaanza lini? Mana taarifa mliyotoa ulitarajiwa uanze mwezi huu wa 10,sasa tuna siku 6 tu tumalize mwezi.
Hakuna taarifa iliyoeleza kuwa usafiri utaanza mwezi huu wa kumi isipokuwa kulikuwa na taarifa za mradi kukabidhiwa serikalini baada ya mkandarasi kumaliza ujenzi.
 
Mfumo huu ulikuwepo awali lakini ilitokea changamoto ukaharibika ndiomaana hata utaratibu wa kutangaza vituo haupo, kwa sasa tuko kwenye hatua za kununua mfumo wa ITS inteligent transport system ambao utakuwa ukitumika kuongoza magari, kupanga ruti, sambamba na masuala yote yanayohusu vituo, muda ambao abiria atatumia kutoka sehemu moja hadi nyingine n.k.
 
Hakuna ukweli katika jambo hilo, kwanza daladala uwezo wake ni mdogo katika kubeba abiria wengi, pili miundombinu ya vituo hairuhusu kushusha na kupakia abiria kwani daladala ni fupi na hazijatengenezwa kwa ajili ya BRT.
Hamna mfumo mzuri wa kupeana taarifa ndani ya taasisi. Sasa mimi nakwambia daladala zipo zimeanza kazi zinatoka Makumbusho kupitia, Mwananyamala, Studio, Magomeni, Manzese, Ubungo hadi Mbezi na mimi nipo nimepanda muda huu.
 
Ni mnatumia njia ya BRT au vituo vya pembeni ya barabara?.

That's why jamaa anakwambia daldala ni fupi haziwezi kutumia vituo vya Mwendokasi!.
 
Ni mnatumia njia ya BRT au vituo vya pembeni ya barabara?.

That's why jamaa anakwambia daldala ni fupi haziwezi kutumia vituo vya Mwendokasi!.
Zinatumia nji ya kawaida ila madereva wajanja. Mfano yakitoka Mbezi wanaita abiria wa Ubungo Manzese Magomeni ambapo nauli ni 600. Wakifika Magomeni wanashusha abiria wote wanaanza kupakia wa makumbusho. Ya asubuhi nilipandia studio nikashukia Manzese nilikuwa na shida zangu.
 
Upo nje ya mada kabisa, nadhani utakuwa uelewi issue ya kuongeza mabasi 15!.
 
kuna siku nimekaa pale mbezi kwenye foleni lisaa hakuna basi inayokuja kupakia abiria
 
Baada ya magari kuongezeka yanapungua.. just imagine gari ya kwanza inaharibika kimya la pili linaharibika kimya 3 4 5 6 7 8 9 10 mpaka 70 kimya hapa kuna watu au genge la wahuni..

Watu wanashindwa na kampuni binafsi ni nani anaweza kukubali gari zake zote ziwe juu ya mawe awa watu wafunguliwe kesi za uhujumu uchumi tu
 
Pia zinaweza enda Ilemela, pasiansi had airport itasaidia sana kupunguza adha ya usafiri kwa mkoa wa mwanza
 
Hamna mfumo mzuri wa kupeana taarifa ndani ya taasisi. Sasa mimi nakwambia daladala zipo zimeanza kazi zinatoka Makumbusho kupitia, Mwananyamala, Studio, Magomeni, Manzese, Ubungo hadi Mbezi na mimi nipo nimepanda muda huu.
kinachozungumziwa hapa ni daladala kupita kwenye njia maalum za BRT sio route za kawaida za njia za mitaani ambazo zimeainishwa na Mamlaka ya LATRA. habari hii ilisema daladala kuanza kutumia njia za mwendokasi ili kusaidia mabasi jambo ambalo sio sahihi. Umewahi kuona wapi daladala inapita kwenye barabara za kasi? magari binafsi yenyewe na ya serikali na vyombo vya ulinzi unaona jinsi yanavyozuiliwa. tuache kuleta taharuki, niletee picha humu ya daladala inayosaidia Mabasi kazi kama ipo.
 
Serikali iko kazini na kama ulifuatilia juzi ziara ya Waziri Mchengerwa alitoa maagizo ya kuongeza watoa huduma zaidi ya mmoja ili kuleta ushindani huo ndio mwelekeo tuvute subra mambo mazuri yanakuja, hakuna mtu yeyote anayefurahia watanzania kuteseka kwa adha ya usafiri ni suala la muda tu.
 
Yani kati ya usafiri unaokera ni huu wa mwendokasi.
Kukaa kituoni kwa nusu saa na zaidi huku mabasi yakiwa yanaunguruma na kupaki bila sababu huku watu wamefurika na hakuna mtu anaechukua hatua. Mfano ni hapo kivukoni
 
Afsa Usafirishaji

Humo niliko-bold hivi umemuelewa kweli huyo uliyem-quote au ulimsoma ili umjibu?currently kuna gari 70 zipo juu ya mawe na mliosababisha haya bado mpo ofisini hata wakija washindani bado hizo chache za serikali zilizobaki mtaziuwa tutarudi huku huku kwenye tabu sasa kwanini hao waliozembea gari 70 zikafa wasichukuliwe hatua ili wawe mfano kwa wengine?

Hizo siasa za serikali ipo kazini usizilete hapa hata huyo mcherengwa hana cha kubadilisha ktk huu mradi kama nyie mliopo huko hamjawajibishwa kwa uzembe wenu,huu mradi unaenda na upepo wa siasa coz week tatu nyuma pale Mbezi terminal alikuja mkuu wenu wa idara na mkuu wa mkoa au wa wilaya (sikumbuki vizuri maana sikufuatilia) hii siku bus zote mlizihamishia ruti ya Mbezi ili kuonekane hakuna tatizo kesho yake abiria tukakaa pale 47minutes bila kuja gari yoyote.

Bado sijazungumzia leo kukaa dk zaidi ya ishirini stand kisa magari hamna,hizo gari kuna shida gani zisitengenezwe?hela mnazokusanya mnapekeka wapi ujue mnatia hasira sana nyie jamaa.
 
Yani kati ya usafiri unaokera ni huu wa mwendokasi.
Kukaa kituoni kwa nusu saa na zaidi huku mabasi yakiwa yanaunguruma na kupaki bila sababu huku watu wamefurika na hakuna mtu anaechukua hatua. Mfano ni hapo kivukoni
Wanakera sana hawa halafu mtu anakuja hapa anajibu tu simple simple kwamba eti serikali iko kazini.

Ipo kazini kuwatia watu shida au kazini kufanya nini!
 
Kuna ushauri upi kati ya uliotolewa hapa mmeufata?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…