DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

Kwa mujibu wa design tunatakiwa tuwe na basi kila baada ya dakika tano ,kwa sasa kwakua tuna upungufu wa mabasi ndiomaana hali haiko kama inavyotakiwa kuwa , lakini juhudi zinafanyika usiku na mchana na serikali yenu sikivu ya awamu ya tano kuhakikisha mabasi ya kutosha yanapatikana kwa awamu ya kwanza na awamu ya pili kule Mbagala ambayo iko katika hatua za mwisho za umalishaji.
Jibu la kisiasa hili. Ungeeleza tatizo mtalimaliza lini au hadi sasa mnaupungufu wa mabasi kwa % ngapi na nini mkakati ya muda mfupi au mrefu wa kutatua tatizo.

Hili jibu lako hata mwaka 2050 tatizo likiendelea kuwepo ukatoa jibu la hivi itakuwa sawa ila haisadii wanaohitaji hiyo huduma yenu
 
Ushauri wangu ni kuwa tokeni hapo mlipo msafiri nje ya nchi. Mtembelee nchi kama Sweden na Uholanzi muone huduma za usafiri wa umma zinavyofanyika. Hata kama mazingira hayafanani ila mjikite kujifunza yale yanayoweza kufanyika nyumbani pia.

Mkifika Sweden ama Uholanzi, msiishie kukaa mahotelini wala maofsin bali mtumie kama mwezi mzima kila siku kwa kutumia usafiri wa umma. Week ya mwisho ya safari yenu nendeni sasa mkawatembelee wataalamu wenzenu maofsin wawape shule ya namna walivyofanikiwa kuendesha sekta ya usafiri wa umma.

Baada ya hapo mrudi nyumbani kutekeleza mtakayojifunza. Huu ndo ushauri wangu.
 
View attachment 2625074
DART Tumeanzisha ukurasa huu rasmi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa lengo la kupata maoni, ushauri , mrejesho na hata malalamiko yanayohusu huduma zetu. Aidha tunawahakikishia watumiaji wa huduma zetu kuwa maoni, ushauri, malalamiko, Pamoja na hoja zenu juu ya huduma zetu yatafanyiwa kazi kwa uharaka na hatua stahiki zitachukuliwa ili kuboresha huduma.

Kwa kupata msaada wa haraka kuhusu huduma zetu unaweza kutupigia simu 0800110147 ni bure. Kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa tano na nusu usiku

Pia unaweza kutufuatilia katika tovuti ya www.dart.go.tz na mitandao yetu ya kijamii ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka ya FACEBOOK, INSTAGRAM, TWITTER, LINKEDIN, YOUTUBE.

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

Anuani
S.L.P 724, 16103
Ubungo Maji, Morogoro Road
Dar es Salaam, Tanzania

Barua pepe: info@dart.go.tz.

#usafiri wa umma nadhifu

#mwendokasi app
1. Ushauri wangu wa kwanza ni kwamba si sahihi nyie kujiita ''Mabasi Yaendayo Haraka (DART)'' kwa sababu hamuendi haraka bali mnaendesha mabasi yenu kwenye barabara yenu maalum, so mnaweza kujiita Dar City Bus/Transport kwa sababu hamna tofauti yoyote na UDA, ukiondoa kutembea kwenye barabara yenu (hivi barabara ni yenu au ni ya Umma??)

2. Ushauri wa pili (hamtaupenda) hivyo zaidi zaidi nauelekeza kwa serikali: Kwa kuwa hizo barabara zilijengwa kwa fedha za umma (hata kama ni mkopo tunalipa watanzania wote mpaka walioko vijijini) kuwe na kampuni mbili au tatu, zenye uwezo na vigezo vyote ziruhusiwe kusafirisha abiria kwenye hizo barabara ili zishindane na nyie mnaojiita DART, kama ambavyo kwenye mawasiliano ya simu tuna Vodacom, Tigo, Airtel, Halotel etc.
Jambo hili litakuwa na faida nyingi, kwanza barabara hizi ambazo serikali imetumia bilions of money zitakuwa efficiently used; pili abiria hawatakuwa na muda mrefu wa kukaa kituoni kwa sababu kila after 5 - 10 minutes kutakuwa na Bus la kuwasafirisha waendako, tatu mapato ya serikali yataongezeka kwa sababu ya abiria wengi kusafirishwa kwa siku, nne abiria watakuwa wanasafiri more comfortably bila kujazwa kwenye bus moja kama nyanya kwenye tenga (hii itatokana na ushindani na uwingi wa mabasi; na pia ninajua kuna makampuni yanaweza hata kuanziasha express/VIP transport ambapo pale mtu akiona ana haraka sana au anaumwa hataki shida atalipia 1000 au 1500 per trip anakaa comfortably kwenda huko aendako; na Mwisho hata nyie DART mtabadilika maana kwa sasa mnafanya kazi kimazoea sanaa...
 
Suala hili linafanyiwa kazi

Kwa nini hujibu baadhi ya hoja na maswali?
Kuna maswali umeulizwa huko juu lakini unajifanya kama hujayaona!
Ushauri ukitolewa sawa unaweza kuuchukua tu bila kujibu, lakini maswali unapaswa kujibu bila kuacha chembe! Kama huna majibu sema huna!!!
 
Magari kuwa mengi au machache sio tatizo kuna muda kuna abiria wengi kuna muda abiria ni wachache au hamna kabisa ule muda abiria wapo wengi magari yawe mengi abiria waingie siti zijae then row mbili wasimame gari inachora asubuh zina supply chap chap hadi muda abiria washapunguwa nayo yanapumzika mpka jioni yanarudi mengi tena.

Yakiwa mengi bila mpangilio inaweza sababisha foleni tu
 
Hongereni sana kwa kujiunga JF,

Maoni yangu/Malalamiko:-

Kuna tabia ambazo madereva wenu wanakera sana mpaka wanapoteza maana ya mwendokasi ,navyojua serikali haifanyi biashara zaidi ya kutoa huduma ,sasa kuna baadhi ya madereva wakishafika kwenye vituo vikuu(eg gerezani/morrocco/Ubungo) basi wanapaki magari wanaenda kukaa kupiga story wakati kuna abiria kibao wanasubiri magari.....Sijajua why wanafanya hivyo au utakuta wanaondoka tupu bila kubeba abiria.
 
Zilikuwepo ila wafanyakazi wao wasio waaminifu walizihamishia kwenye majumba yao
Dust bins zipo lakini katika baadhi ya mabasi zimeondolewa ama kwa kuibiwa ama kwa kuharibiwa , tunajitahidi mara kwa mara kuhakikisha zinakuwepo na zinatumika ipasavyo, suala la ulinzi wa mali za umma ni la kila mmoja wetu hivyo tujitahidi kuwa walinzi na wa mali za umma, nimesema hivyo kwasababu kuna watu wanadiriki hata kukata handle za kujishika ndani ya mabasi wakati abiria amesimama. Tuwaombe wananchi kuwa walinzi wa mali za umma na kuimarisha usafi kwa ujumla katika mradi wa DART.
 
Tuko active na tunamaanisha na katika hili hatuna masharti kama wengine
Dart mwendokasi ni nani amewaroga?
Ni faida Gani mnapata mkichagua maoni ya watu wachache na kuamua kuyajibu wakati wengi wametoa malalamiko kero au maoni.
Ni hasara Gani mnapata mkijibu maoni na malalamiko ya watu wote?
Naomba unijibu nikicho kuandikia maana sisi hatukuomba tuwape maoni ila nyie wenyewe maana tulikaa kimya na hasira zetu mkaja kututibua nyongo zetu.
 
Dart mwendokasi ni nani amewaroga?
Ni faida Gani mnapata mkichagua maoni ya watu wachache na kuamua kuyajibu wakati wengi wametoa malalamiko kero au maoni.
Ni hasara Gani mnapata mkijibu maoni na malalamiko ya watu wote?
Naomba unijibu nikicho kuandikia maana sisi hatukuomba tuwape maoni ila nyie wenyewe maana tulikaa kimya na hasira zetu mkaja kututibua nyingi zetu.

Jamaa anaboa sana!!!!
vile vitu rahisi ndio anaona vya kujibu!
Zile kero konki anapotezea! Maybe huyu ni mtu kaamua kutengeneza id ya Dart tu, na wala pengine hausiki kabisa na Dart!
 
DART Mwendokasi Hamuwezi kuwa na utaratibu wa gari kuwepo kituoni kila baada ya say robo saa? Wakati mwingine watu wanasubiri gari haziji na zikija zimejaa. Hamuwezi ondoa hiyo kero kwa kuhakikisha kila baada ya dk fulani gari inapita kituoni?
Mfumo wa rotation ni mbovu na sio system ni mtu anapanga ratiba manually.Kunge kuwa na software yenye magari yote ndio iongoze rotation.Pia wanaopswa kupumzika ni madereva sio magari.Kuwe na madereva wengi wanaogawana.Hii style ya dereva kumpuzika na gari kupumzikka sio kabisa.
 
Mimi napenda kujua usanifu mnaotumia katika upanuzi WA hizi barabara, Mfano chang'ombe veta kwenda chang'ombe Kilwa road, hapa mixes traffic, barabara ya Magari mchanganyikomeweka njia Moja hii Sio sawa, Najua mnaangalia sana miundo mbinu yenu ila kwenye mixed traffic inabidi pia mfanye maboresho na muweke njia mbili kila upande!!
Hili tatizo nimeliangalia Kwenye michoro ila litasumbua sana Bora mlifanyie kazi mapema!! Barabara ya Tabata kwenda kinyerezi phase 5, shida ni hiyo hiyo, barabara ya Mikocheni kwenda kawe kutoka Morocco tatizo ni hilo Hilo Single lane mixed traffic hii haikubaliki!! Lifanyieni kazi ni shida kubwa mtasababisha mbeleni
 
2. Kuna madereva wanajiona Miungu watu wanapita na "Out of Service" yaani.
Kuna dereva ana kauli chafu sana, aliwahi kumbana mtu mlangoni badala ya kumpa pole akamwambia umezoea daladala hii siyo daladala
 
DART Tumeanzisha ukurasa huu rasmi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa lengo la kupata maoni, ushauri , mrejesho na hata malalamiko yanayohusu huduma zetu. Aidha tunawahakikishia watumiaji wa huduma zetu kuwa maoni, ushauri, malalamiko, Pamoja na hoja zenu juu ya huduma zetu yatafanyiwa kazi kwa uharaka na hatua stahiki zitachukuliwa ili kuboresha huduma.
Mtaweza kujibu maswali kwa kasi? Au mtakuwa kama Tanesco kila kitu "mtasema tuwaambie tulipo na namba zetu za simu" ndipo mtujibu au kama TTCL mtatuambia "subiri staff wetu aliyekwenda China kwenye mafunzo aje"
 
Back
Top Bottom