DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

Hivi huu usafiri au ni ujinga watu wamejazana hakuna gari mnasubiri hadi lisaa moja na hakuna taarifa mliotoa
 
View attachment 2625074
DART Tumeanzisha ukurasa huu rasmi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa lengo la kupata maoni, ushauri , mrejesho na hata malalamiko yanayohusu huduma zetu. Aidha tunawahakikishia watumiaji wa huduma zetu kuwa maoni, ushauri, malalamiko, Pamoja na hoja zenu juu ya huduma zetu yatafanyiwa kazi kwa uharaka na hatua stahiki zitachukuliwa ili kuboresha huduma.

Kwa kupata msaada wa haraka kuhusu huduma zetu unaweza kutupigia simu 0800110147 ni bure. Kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa tano na nusu usiku

Pia unaweza kutufuatilia katika tovuti ya www.dart.go.tz na mitandao yetu ya kijamii ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka ya FACEBOOK, INSTAGRAM, TWITTER, LINKEDIN, YOUTUBE.

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

Anuani
S.L.P 724, 16103
Ubungo Maji, Morogoro Road
Dar es Salaam, Tanzania

Barua pepe: info@dart.go.tz.

#usafiri wa umma nadhifu

#mwendokasi app
Naomba kujua ujenzi wa barabara ya mwendokasi mwenge hadi boko unaanza lini
 
Mkandarasi ameshakabidhiwa site tayari kuanza ujenzi na ikumbukwe kuwa mwezi wa saba mkataba ulisainiwa baina yake na serikali, anatarajiwa kukamilisha kazi hiyo ndani ya miezi 18 tangu siku aliposaini mkataba.
 
Mabasi mapya,tentative dates ni lini??
 
Kitu kimoja muhimu wekeni bench za kukalia kwenye vituo vyote, hii changamoto nimeishuhudia sio maramoja ,hasa DIT, MAGOMENI KAGERA ,MOROCCO, KANISANI, huku kote nimekutana na changamoto ya mabasi kuchelewa kufika kituoni ama kupitiliza yakiwa yame jaza.Kwahio watu wanasimama hadi saa nzima wakisubiri basi sasa sio wote wazima kuna wagonjwa ,wazee, wenye matatizo ya viungo,hii mnawapa watu tabu ya lazima.Shughulikieni hii tafadhali
 
Kuna mdau anasema kila kituo mpaka wachungulie
Hivi karne hii hata machinga ana 🔊 zake na amerekodi maneno na nyie mmeshindwa bus liwe na speaker za kutangaza kituo ilipo bus na kinachofuata

Hizo hela mnakusanya tumeni basi watu waje kujifunza kwa wenzenu system zinavyofanya
Poleni sana ila mmefeli sana ingawa siko huko
 
Mngeanzisha VIP trips,basi nzuri na hamna kusimama humo ndani full Ac na pia mtu anaibook akiwa home na pia iwe na kagharama flan kamechangamka hata buku tatu from feeder to destination trunk..

au basi me naota tu
 
Habari DART,
BINAFSI LEO NILIKUWA NATAKA KUANDIKA UJUMBE MKUBWA SANA JUU YENU.
Kabla sijafanya hivyo ndio nimekutana na account yenu hapa.

Binafsi ninayo yafatayo juu ya huduma zenu.

MIMI NAISHI MIKOANI ILA NIMEKUWA NIKIJA SANA DAR ES SALAAM MARA KWA MARA.
Kwa kipindi cha mwezi 7,8,9 mwaka 2023.

Niseme ndio kipindi nimetumia sana usafiri wetu.
Kabla ya hapo nilikuwa napenda kutumia bolt hata sehemu mna route zenu mfano Mbezi mpaka Kariakoo.

Mwaka 2020 nilitumia usafiri huu pia ila sikufurahishwa sana na utaratibu wa kipindi hicho ukilinganisha sasa.

Japo kipindi cha 2020 basi zenu zilikuwa mpya na kila kituo zilikuwa zinatangaza tofauti na sasa.

Kwa kilichofanya niandike kuhusu nyinyi siku ya leo ni yafatayo.

1. Niwapongeze kiukweli kwa sasa mimi binafsi naona mwendo kasi inaokoa muda sana na mmekuwa wabunifu sana, hasa route ya kutoka stendi ya mbezi kuja kimara. Pongezi nyingi kwa hilo.
2.Wahudumu wa mwendokasi kwa sasa sijui wamepewa nini ila huduma zao ndivyo inavyotakiwa kuwa, very professional kulingana na mazingira, wamekuwa wavumilivu sana na wanatoa msaada vyema kwa mtu asiliye mgeni hii ni tofauri kabisa na zamani, ambapovilipelekea binafsi kuacha kutumia huduma hiyo.
Wapewe Pongezi nyingi sana kwenye hili.na naomba waendeleze hili.

3. Moja ya kitu kilichonishangaza sana kwasasa kuona watanzania kwa sasa tunapanga foleni kuingia ndani ya basi. Aisee aiyeweka utaratibu huu na kwasasa unafwatwa Pongezi kubwa sana.naomba liendelee kusisitizwa.

Maboresho nayoyaomba myafanye kama itawezekana
1.Kwenye vituo sijui kama ipo chati na ramani ya mwendo kasi, hii itasaidia sana hasa wageni wasio ishi dar kusoma na kuelewa.

2. Kutangaza ndani ya basi kituo kinachofata, hii muhimu sanasana kwa wageni.

3.WAZO KWA UONGOZI WA DART HIVI kwanini ndani ya barabara zenu msiweke Namna ya kulipia magari binafsi.
Mdano mtu anamgonjwa, anawahi Airport, Anaswala la lazima kuwahi, muweke utaratibu wa BOOKING SYSTEM yani kila saa moja mnaweza ruhusu tiketi 11 yaanu magari 11 yanalipia huduma ya kutumia barabara kama express hivyo linapewa kibari maalumu kupita na kutumia barabara hiyo. Vigezo na masharti yazingatiwe. Nafikili hii inaweza ongeza mapato sana na kuokoa maisha ya wanannchi. Mnaweza nipigia simu 0757728630 kwenye hili kujadiliana zaidi. Inawezekana likawa jipya lakini mkilifikilia kuna kitu mtakipata.

4.Kama inawezekana kiyoyozi kifungwe kwenye gari zenu kama inawezekana.

5.kuepusha muingiliano wa magari na watu kuvuka hovyo ni bora ukawepo mkakati wa kuweka fensi barabara yote ya mwendo kasi.

Zaidi ya haya asanteni sana kwa kuwahudumia watanzania na kuifanya nnchi yetu kuwa bora.
 
Niliona kule China ambako ndiko zinakotoka hizi gari za brt usafiri wa umma wote una full ac hamna kufungua madirisha na nauli ni sawa na hii tunayolipa sisi huku yaani yuan 2 kwanini haya ya kwetu yasiwe na huduma hiyo ya full ac muda wote wakati nauli ni kubwa sana.

La pili kule China mabus yao karibu yote yanatumia umeme muda wote wa kazi ambapo kuna yale yenye mkonga nyuma juu kama treni za umeme na kuna yale ya kucharge, hoja yangu ni kwanini haya mabus yasiletwe yale ya mkonga juu maana tayari yana barabara zake hivyo ni rahisi kutandaza waya za umeme kwaajili yake badala ya kung'ang'ania haya ya mafuta. Ninaamini inawezekana kabisa, hata tukiamua ya kucharge pia inawezekana station za kujazia charge ziwekwe kwenye vituo vikubwa yanakogeuzia kuliko kubaki nyuma tuu bila sababu za msingi.
 
Haya hapa, si kitu cha kushindwa hiki
Screenshot_20230912-021405.jpg
View attachment 2746414
 
Tunakushukuru sana kwa maoni yako ya kuboresha huduma zetu, mawazo yako ni mazuri sana na baadhi yake tumeshaanza kuyafanyia kazi ikiwemo utaratibu wa kuwa na Mabasi mahsusi yenye viyoyozi lakini pia kuwa na VIP buses, aidha tunaendelea na mchakato wa kuwa na sheria yetu ambayo itaturuhusu kusimamia ipasavyo miundombinu yetu ikiwemo ya udhibiti wa wavamizi wa magari binafsi na yale ya taasisi za umma kuingilia barabara za Mabasi Yaendayo Haraka. Kuhusu suala la barabara hizo kutumika kwa malipo huo sio utaratibu na lengo kuu ni wananchi waache magari yao binafsi ili watumie usafiri wa umma ambao ni wa rahisi na nafuu zaidi, mtandao wa BRT kwa awamu zote sita katika mkoa wa Dar es Salaam ukikamilika kutakuwa hakuna haja ya watu binafsi kutumia njia hizo mahsusi kwa Mabasi kwani mtandao wa njia hizo utakuruhusu kwenda popote pale kwa urahisi na kwa gharama nafuu ilimradi tu uwe ndani ya mtandao wa BRT.
 
Niliona kule China ambako ndiko zinakotoka hizi gari za brt usafiri wa umma wote una full ac hamna kufungua madirisha na nauli ni sawa na hii tunayolipa sisi huku yaani yuan 2 kwanini haya ya kwetu yasiwe na huduma hiyo ya full ac muda wote wakati nauli ni kubwa sana.

La pili kule China mabus yao karibu yote yanatumia umeme muda wote wa kazi ambapo kuna yale yenye mkonga nyuma juu kama treni za umeme na kuna yale ya kucharge, hoja yangu ni kwanini haya mabus yasiletwe yale ya mkonga juu maana tayari yana barabara zake hivyo ni rahisi kutandaza waya za umeme kwaajili yake badala ya kung'ang'ania haya ya mafuta. Ninaamini inawezekana kabisa, hata tukiamua ya kucharge pia inawezekana station za kujazia charge ziwekwe kwenye vituo vikubwa yanakogeuzia kuliko kubaki nyuma tuu bila sababu za msingi.
Tunakoelekea ni kuzuri tutaanza na matumizi ya Gesi asilia na hatimaye kwenye matumizi ya magari ya kuchaji kwa umeme na hata solar, lengo ni kuelekea katika matumizi ya nishati ambazo hazichafui na kuharibu mazingira kama vile matumizi ya umeme.
 
Wekeni hayo mabasi yenu AIC maana madirisha Huwa madogo na watu wanakuwa wengi sana jambo ambalo ni hatari.
Hafu kingine kwanini mabasi yenu mengine hupita vituoni matupu bila kusimama au kuchukua abiria hamuoni mnafanya biashara kichaa
Duh, AIC tena?
I hope unamaanisha AC.
Kwenye usafiri na majengo ya umma mfano madarasa, nyumba za ibada nk hii kitu haifai kabisa! May usafi ufanyike mara zote kuondo vumbi na waweke carpet ya kufutia miguu tope/vumbi (je itawezekana?)

Wao DART Mwendokasi wajitahidi kupunguza muda wa kusubiri gari! magari ya sehemu zenye abiria wengi mfn Gerezani -kimara terminal, yaongezwe. Lilitoka hili linaingia jingine hapohapo bila kusubiri dk15...
Abiria wakae level seat! Mbona mwanzoni wakati yamekuja ilikuwa hazijazi sana! Na ilikuwa ni usafiri wa luxury tofauti na sasa imekuwa kero!
 
DART kwanini mnalipisha abiria nauli mara mbili kwa kisingizio cha TIKETI kuexpire?

Hivi manadhani abiria wanaamua ndio wanaosababisha au ninyi kwa huduma yenu mbovu? Leo hapo Kimara nimewamezea mate hatari, mnafanya mambo ya kipumbavu kweli kweli...

Mtu una nunua tiketi ya moja kwa moja hadi Mbezi ukiwa Kivukoni au Gerezani, halafu unaenda kusubiri gari kwa zaidi ha nusu saa nzima then unapata gari ya kimara unaruhusiwa kuipanda ukiwa na tiketi yako itakayokuwezesha kuendelea na safari ya Mbezi, njiani gari lazima isimame vituo mbalimbali kushusha na kupakia abiria. Ukifika Kimara unataka kuunganisha na ukaonesha tiketi ghafla unaambiwa imeisha muda wa matumizi, ukijieleza husikilizwi badala yake unalazimishwa kwenda kununua nyingine, yaani unalipia nauli ya kutoka Kimara hadi Mbezi mara mbili(wizi mtupu).

Leo nililazimika kusimama pale ili nione ukubwa wa jambo hili, nikaona watu wengi wanakuja na tiketi walizokatia mjini wakifika pale wanaambiwa zimeisha muda wa matumizi na kuendelea kulazimishwa kununua zingine. Hivi kwa namna hii wanavyotuibia ndio utoaji wa huduma huu, uwezeshaji wa kutuibia?

Kwa nini ukiwa unaenda mjini unaweza kubadili magari/vituo bila shida lakini iwe shida ukiwa Kimara kwenda Mbezi?
 
Hamisi Kigwsngwala amesema mmeshindwa kuendesha hayo mabasi na kukusanya nauli ilhali makonda darasa la saba wa daladala ziendazo vijijini wanaweza, ninyi Ni wasomi mliobobea kwenye fani zenu mnashindwa mpaka mnataka mwekezaji aje akusanye nauli. Hamuoni kwamba mna vyeti feki au degree za michongo?
Mnashindwa nini ambacho makonda wa daladala za Mbagala wanaweza?
 
Asante kwa kuja.
Ni lini hayo mabasi mtayapeleka Mwanza pia ili wananchi wapate huduma ya usafiri..??
Sababu jiji la Mwanza limekua na tayari limechangamka na mkituletea hizo Bus zikaanzia route ya Kisesa, Igoma, Neshno, Buzuruga, Mabatini, Nata, Pepsi, Mkuyuni, Nyegezi, Buhongwa, Nyashishi hadi Usagara and Return.
Mwanza kupata mwendokasi pengine miaka 30 ijayo vingine ni matumizi mabaya ya fedha.
 
Vipi mikoani hamleti miendo ya kasi
Mbona hipo tu ya kutosha, km 40 kwa dk 15 au 20 ukiwa na town hiace, sasa hapo unataka mwendo kasi ipi? Km 80 kwa saa 1 unataka mwendo kasi ya namna gani?
 
Back
Top Bottom