'Dawa 178 na Vifaa Tiba 15 vilivyoondolewa kwenye Kitita kipya cha NHIF'

Kuna lile shangingi la kisiasa litakuja ns ngonjela zake likidifu mama kaupiga mwingi! Ulevi?
 
Kama utakuwa na uwezo kidogo Bora kujiunga na bima za makampuni binafsi za AAR ama nyingine tu, hizi bima zetu za kinyonge za NHIF tutajikuta tunafia hospitali Kwa kukosa dawa πŸ™ŒπŸ˜­

Nchi imegeuka ya Matajiri hii saivi
Sawa kabisa, si unajua wao hawaugui malaria na hata wakiiugua wanamudu tiba yake. Ndiyo maana dawa za magonjwa ya matajiri wamezibakiza, halafu eti bima ya afya kwa wote. Waseme bima ya afya kwa matajiri, maskini hana bima.
 
Lakini Bima ni ajiri ya dharula, unaweza ugua na hauna kitu! Sasa ukiambiwa kununua tena dawa na vifaa maana yake nini?
Bima maana yke unalipia in advance ili utakapougua utibiwe, sasa wanapoanza kulazimisha eti unapougua uwe na hela,JE KUNA MTU ANAJUA ATAUGUA LINI NA UGONJWA GANI?
Halafu Bunge linapitisha?
 
Ukiaachana na Mambo Mengine naichukia sana NHIF, ukiongeza hili swala la kifurushi kipya ndo kabisaa ...
 
Bima zao wazihuisha hazina mpaka ingawa utaona kama kadi zinafanana na yako ila yy ni V.I.P akifika hospital hiz stori hawezi kuambiwa eti kuna dawa zimetolewa.
 
 
Sawa kabisa, si unajua wao hawaugui malaria na hata wakiiugua wanamudu tiba yake. Ndiyo maana dawa za magonjwa ya matajiri wamezibakiza, halafu eti bima ya afya kwa wote. Waseme bima ya afya kwa matajiri, maskini hana bima.
Viongozi hawana huruma na Wananchi wao πŸ₯²
 
Kuna wakati watu waache ujinga qa kushabikia vitu ambavyo n sensitive sana ona kinachofanywa na NHIF knagharimu wananchi mno

Mfano Leo kila dawa tunazoandika kwa bima zinagoma Ina mana inabdi kumwambia mgonjwa aanze kununua dawa nje hko ya maduka ya madawa tunawaumiza mno Hawa wananchi
 

Inawezekana leo tukaona hawa wanaharakati wanaopiga mbinja kana kwamba wanasaka umaarufu. Lakini tupime haya mambo yanayozungumzwa with facts. Na tumeona namna ambavyo Waziri wa Afya akitoa fafanuzi mbalimbali wakati wa tangazo la Mgomo wa watoa huduma za afya binafsi dhidi ya ujio wa Kitita kipya cha Bima ya Afya NHIF.

Serikali, inapaswa kuwajali wananchi wake linapokuja suala la msingi kama afya. Lakini endapo serikali inafanya jambo lenye muelekeo wa kutumia hitaji muhimu la Afya za watu kama mtaji wa kuvuna kutoka kwa wananchi ni wazi serikali hiyo itakuwa haijali na hailindi maslahi ya wananchi ambao ndiyo nchi yenyewe.

Mpaka sasa, hakuna aliyewajibika kwenye uchotwaji wa mabilioni ya fedha kutoka mfuko wa Bima ya Afya (NHIF). Na wale wale wanaonyooshewa vidole kuhusu ubadhirifu huo ndiyo wamekuja na hii scheme ambapo kwa wataalam wa intelejensia jamii tunaona ni kama kuhaha kutaka kufidia upotevu ulioripotiwa na CAG.

Kuondoa dawa 178 na vifaatiba 15 kwenye kitita kipya cha NHIF haimaanishi kwamba watakaoathirika ni watoa huduma za afya binafsi, bali ni sisi wananchi ambao tunawajibishwa (LAZIMA) kisheria kulipia Bima ya Afya.

NI LINI WATANZANIA TUTAKUWA SERIOUS KWENYE MAMBO YA MSINGI?
Tubadilike. Waziri wa Afya siyo mwenzetu kwenye hili. Hana huruma kwa Watanzania na hili linaloendelea ni jibu tosha la namna watawala wetu wasivyoishi na Tanzania mioyoni mwao.
 
Kinachofanyika huko NHIF hakina tofauti na kilichotokea katika mifuko ya PSSSF na NSSF. Issue ya kikotoo imekuja baada ya mifuko kuwa dhoofu hali kutokana na madeni makubwa ya serikali na pengine hata ubadhilifu. Uzembe wa watendaji mzigo anakuja kubebeshwa mwananchi. Hili bomu ipo siku litawalipukia!
 
Halafu wanakuja vimbwenelehi kutujaza ujinga kwamba nchi inakwenda vizuri. Tukianza kuhoji tunatishiwa kwamba tunahatarisha usalama wa nchi.

Kimya chetu ndo umauti wetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…