View attachment 2934578
Inawezekana leo tukaona hawa wanaharakati wanaopiga mbinja kana kwamba wanasaka umaarufu. Lakini tupime haya mambo yanayozungumzwa with facts. Na tumeona namna ambavyo Waziri wa Afya akitoa fafanuzi mbalimbali wakati wa tangazo la Mgomo wa watoa huduma za afya binafsi dhidi ya ujio wa Kitita kipya cha Bima ya Afya NHIF.
Serikali, inapaswa kuwajali wananchi wake linapokuja suala la msingi kama afya. Lakini endapo serikali inafanya jambo lenye muelekeo wa kutumia hitaji muhimu la Afya za watu kama mtaji wa kuvuna kutoka kwa wananchi ni wazi serikali hiyo itakuwa haijali na hailindi maslahi ya wananchi ambao ndiyo nchi yenyewe.
Mpaka sasa, hakuna aliyewajibika kwenye uchotwaji wa mabilioni ya fedha kutoka mfuko wa Bima ya Afya (NHIF). Na wale wale wanaonyooshewa vidole kuhusu ubadhirifu huo ndiyo wamekuja na hii scheme ambapo kwa wataalam wa intelejensia jamii tunaona ni kama kuhaha kutaka kufidia upotevu ulioripotiwa na CAG.
Kuondoa dawa 178 na vifaatiba 15 kwenye kitita kipya cha NHIF haimaanishi kwamba watakaoathirika ni watoa huduma za afya binafsi, bali ni sisi wananchi ambao tunawajibishwa (LAZIMA) kisheria kulipia Bima ya Afya.
NI LINI WATANZANIA TUTAKUWA SERIOUS KWENYE MAMBO YA MSINGI?
Tubadilike. Waziri wa Afya siyo mwenzetu kwenye hili. Hana huruma kwa Watanzania na hili linaloendelea ni jibu tosha la namna watawala wetu wasivyoishi na Tanzania mioyoni mwao.