Dawa ya Mpenzi anayekujibu dharau au ambaye hana muda na wewe ni hii hapa

Dawa ya Mpenzi anayekujibu dharau au ambaye hana muda na wewe ni hii hapa

Mkuu hapo kwenye ukimnya ungeongezea na KUJIPENDA mwenyewe hakika sasa hivi ungeitwa baba kijacho ili asikupoteze.

Hawa wapuuzi ukijifanya upo available, mara unaumia mara unampenda, kumsahihisha na kumjali sana utajikuta una nyonyoka hadi nywele..


Nb. Sisi wenzako sasa hivi tuna KAA KIMNYA, TUNAJIPENDA WENYEWE WALA HATUWATAFUTI NA IKITOKEA KATUFUMA TUNAJIBU "SAWA" KWENYE KILA KITU ALAFU TUNAKULA BUYU
New tricky......kwasasa sitaki kusikia nyee wala nyaa ni kula buyu tu
 
Watu na hisia zenu.

Huwa natoa notice mapema, nina zero tolerance na drama, malingo ma dharau.
Akileta hizi pigo, anakula persona non grata chap.
Hapo kwenye Personal non granta hahhahaha inampa emotional damage kwa miezi 2 full
 
Aisee mahusiano yanachangamoto nyingi sana, hii ya kutotafutwa ni kidogo muno. Niseme tu kama ilikusaidia wew inatosha ILA SIO NJIA YAKUAMINIKA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA MAPENZI MPKA UTOE MAELEKEZO YA SISI WAJOMBA TUZITUMIE.
Mimi nimepigwa nazo nyingi sana ila njia nyingi zilifeli sana ila chache ndio nimeandika ndg Mjomba
 
Wajomba na Mamshangazi habari zenu.

Mahusiano yanachangamoto nyingi sana, ukiona mahusiano yako yamesimama imara na hujawahi pitia changamoto kama hizi siku ikikukuta utatamani kuzimia.

Baadhi ya mahusiano yanapitia changamoto hizi.
1. Kunyamaziwa kimya kwa siku 2 hadi 3

2. Kujibiwa majibu short kama "SIJUI, SINA,UTAJUA MWENYEWE"

3. Mpenzi wako kutokukuaga kwa lolote yaan anakuwa anajiamulia mwenyewe tu hadi ukimpigia simu ndio akuambie yupo sehemu fulani.

4. Kutokukutafuta asubuhi na usiku akitala kulala,muda wote anajifanya yupo BUSY

5. KUKUJIBU KWA HASIRA

6. Hajali kuhusu hisia zako pindi unapomueleza

7. Unampigia simu hadi mara 3 na kutuma sms zaidi ya 3 na hajibu lolote hadi masaa 3 au 6 pengine ndio imeisha hivyo.

8. Kumrekebisha makosa kila siku na bado anayarudia.

BINAFSI NILIPITIA CHANGAMOTO HIZI ILA NILIJIFUNZA KITU....!!!
Kwa mahusiano niliyokuwa nayo hapo awali niliteseka sana na nilipatwa na msongo wa mawazo, Binafsi sio mtu wa kuwa na wanawake wengi na sio mtu wa kutengeza mahusiano kila leo....ninapenda sana kuwa na husiano langu 1 muhimu sana.

NILIFANYA NINI?
Binafsi nilianza kujifunza haya na ilinisaidia kwa kiasi kikubwa kurejesha FURAHA BINAFSI
1. Nilijiweka chini nikajishauri kwa masaa 3 then nikaamua kukaa KIMYA.

2. Sikumtafuta tena, baada ya siku 3 alinitafuta kwa simu na sms na sikupokea simu yoyote na sikujibu lolote.

3. Nilijiweka Busy for nothing, yaani kazi zangu zikiisha najipa overtime ya kazi hata za wengine ili nisikae chini kuwaza ushenzi, nilijipa mzigo mkubwa sana.

4. Nilianza kuzingatia Afya zaidi na kutafuta amani yangu

5. Sikutafuta rafiki yake yeyote wala sikuongea na yeyote kuhusu mpenzi wangu, kifupi nilikata mzizi na kuondoka ma shina.

Hayo juu ni baadhi tu ya vitu nilivyofanya, kiukweli inaumiza kujitenga na mtu uliyempenda kwa dhati na kumjali kwa kila aombacho.

KUMBUKA.
Sikumuacha ila nilijipa muda kupona kwenye mateso na vifungo vya ajabu.

MAJIBU
Baada ya kugundua ukimya wangu ambao yeye aliona ni kero alianza kunitafuta kila saa na kuniuliza wapi nilipo ili aje tuongee, sikuwa najibu lolote zaidi ya ku bluetick huko whatsap tu hii ilimfanya akasogea zaidi na kumiss muda wangu kwake, haikuwa rahisi ila kwasasa tangu qjue kuwa ninaweza kuishi bila yeye amekuwa karibu na adabu imerudi.

FUNZO KWA WAJOMBA NA MAMSHANGAZI

JIFUNZENI KUITAFUTA AMANI YA MOYO WAKO MAANA ULIYENAYE ANAWEZA KUITUMIA KUKUUMIZA KWA KUKUONA WEWE MSUMBUFU.

INAUMA ILA INABIDI UZOEE.
NAOMBA KUWASILISHA
OOh kwa age hii mwanamke akiniletea dharau zinamrudia yeye kwani nimampenda anayethamini mapenzi yangu na asiyethsmini huwa simpi thsmani hata chembe, hata akija uchi sina mpango naye
 
Yes, hebu tupe kanunui mbili tatu.....maana sisi wengine kuna watu tumewapenda na hatujui sababu za kuwapenda!🤔
Mimi sio mwandishi mzuri kaka.
Woooi mimi mwenyewe huyu kaka nikimuangalia anavyonipenda namuomba Mungu anipe hekima na busara niwe mtiifu kwake daima.
 
OOh kwa age hii mwanamke akiniletea dharau zinamrudia yeye kwani nimampenda anayethamini mapenzi yangu na asiyethsmini huwa simpi thsmani hata chembe, hata akija uchi sina mpango naye
Sasa akija uchi siunapita naye tu halafu unamuacha aende
 
Back
Top Bottom