Usiombe ukutane na mwanaume anakudharau halafu wewe umempenda unategemea mvuke hatua ya ndoa.
Kuna jamaa alifikia sehemu akaanza verbal abuse mara "we ni mzuri na una mguu mzuri sana ila ungekuwa mwembamba zaidi ya hapa, na pia sipendi maji ya kunde napenda mdada mweupe", eeh, you mean unataka nijichubue, and I was just 62kg kwa height ya 168m, kweli jamani?. Nikaona hii ni ile wanayosema wahenga "akufukuzae hakuambii toka"
Tukapotezeana hivyo kimya kimya. Ikapita kama wiki 2 akanipigia simu nakutakia mitihani mema", nilikiwa chuo, nikasema "asante baba".. hatukuwasiliana tena. Penzi likaishia hivyo. Before alikuwa ananiambia mi ni wife material nikawa namwambia ngoja nimalize shule kwanza, nakupenda kwa dhati kabisa.
Mwaka mmoja niko zangu kazini (niliajiriwa immediately) nakutana na coworker ambaye ni mutual friend yetu. Nam-add Facebook jamaa ana-pop up up kwemye friend list ya coworker. Nikashtuka unamfahamu fulani akasema ndiyo, kanipa story fulani nikabaki nacheka tu.
Ingawa naye alipata kazi haraka ali-mess up na mdada wa watu akamtia mimba, mzazi wa mdada akakomaa hapa unaoa, silei mabinti waliozalishwa akafungishwa ndoa mithiri ya ndoa mkeka ya kanisani, you can tell hakukuwa na maandalizi yoyote just ndoa ifungwe tu.
Kilichonichekesha mdada ni mweusi kama mkaa (Sina tatizo na rangi ya mtu, all skins are beautiful, ila si alininyali mimi maji ya kunde anataka mwanamke mweupe?, kwanini nisicheke?) Kama haitoshi, mdada alivyozaa alishift kutoka model hadi jimama libonge, yaani obese kabisa. Sasa kwenye picha yao ya harusi jamaa yuko kama ananing'inia walivyo-hug maana mdada kamzudi size, nikasema dawa yako, malipo hapa hapa duniani.
Few year later tukaonana, sijui kwanini Mungu anafanyaga hivi. Analalamika eti sikufight enough, anahoji kama kweli nilikuwa nampenda, nikamwambia baba, kwenye mapenzi nafight na mtu ninayempenda against dunia, siyo mimi ni-fight na dunia peke yangu wewe ukiwa upande wa dunia. Akashauri ooh, kuna option, naweza kumwacha mke wangu tuoane ndoa ya kanisani ila kwa walokole, wale wanafungisha tu ndoa talaka ikikamilika, and he was so serious, nikamwambia baba siingilii ndoa za watu kwa namna yoyote ile, na huyo ni mpaka lifo kiwatenganishe. Kuna mjinga mmoja akampa namba yangu nikamblock.
Penzi hakika halilazimishwi, kama mnalazimika kununiana na kuchuniana kudemand attention hilo siyo penzi, nna masha na long term implications.