Dawa ya Mpenzi anayekujibu dharau au ambaye hana muda na wewe ni hii hapa

Dawa ya Mpenzi anayekujibu dharau au ambaye hana muda na wewe ni hii hapa

Haya mambo ya kupigiana simu kila muda na messages ndo yanavunja mahusiano. Kila saa kupigiana na kuchat ni uwendawazimu. Mimi kiukweli ni jambo ambalo siwezi. Ukipokea salamu asbh ni hadi jioni baada ya kazi. Kama mchana nitakumbuka basi nitasalimia. Video calls marufuku.
 
Principle ni moja kama sio mbili
1.Hakuna kuongeza simu juu ya simu ambayo haijapokelewa.
2. Hakuna kuongeza sms juu ya sms ambayo haijajibiwa.

Kumpa mtu umuhimu sana kwenye maisha yako ni ukichaa.
100% correct, hivi umempigia mtu simu hajapokea kwa kutosikia au kusudi vyovyote vile unapiga tena sasa kama ya kwanza hajapokea au kujibu ya pili faida yake ni nini? hakupokea ya kwanza ndio atapokea ya pili? Kama hakusikia akiona atapiga lakini unapiga hapokei unapiga ya pili ndio anapokea basi jitafakari haraka kabla hujachelewa.
 
Wajomba na Mamshangazi habari zenu.

Mahusiano yanachangamoto nyingi sana, ukiona mahusiano yako yamesimama imara na hujawahi pitia changamoto kama hizi siku ikikukuta utatamani kuzimia.

Baadhi ya mahusiano yanapitia changamoto hizi.
1. Kunyamaziwa kimya kwa siku 2 hadi 3

2. Kujibiwa majibu short kama "SIJUI, SINA,UTAJUA MWENYEWE"

3. Mpenzi wako kutokukuaga kwa lolote yaan anakuwa anajiamulia mwenyewe tu hadi ukimpigia simu ndio akuambie yupo sehemu fulani.

4. Kutokukutafuta asubuhi na usiku akitala kulala,muda wote anajifanya yupo BUSY

5. KUKUJIBU KWA HASIRA

6. Hajali kuhusu hisia zako pindi unapomueleza

7. Unampigia simu hadi mara 3 na kutuma sms zaidi ya 3 na hajibu lolote hadi masaa 3 au 6 pengine ndio imeisha hivyo.

8. Kumrekebisha makosa kila siku na bado anayarudia.

BINAFSI NILIPITIA CHANGAMOTO HIZI ILA NILIJIFUNZA KITU....!!!
Kwa mahusiano niliyokuwa nayo hapo awali niliteseka sana na nilipatwa na msongo wa mawazo, Binafsi sio mtu wa kuwa na wanawake wengi na sio mtu wa kutengeza mahusiano kila leo....ninapenda sana kuwa na husiano langu 1 muhimu sana.

NILIFANYA NINI?
Binafsi nilianza kujifunza haya na ilinisaidia kwa kiasi kikubwa kurejesha FURAHA BINAFSI
1. Nilijiweka chini nikajishauri kwa masaa 3 then nikaamua kukaa KIMYA.

2. Sikumtafuta tena, baada ya siku 3 alinitafuta kwa simu na sms na sikupokea simu yoyote na sikujibu lolote.

3. Nilijiweka Busy for nothing, yaani kazi zangu zikiisha najipa overtime ya kazi hata za wengine ili nisikae chini kuwaza ushenzi, nilijipa mzigo mkubwa sana.

4. Nilianza kuzingatia Afya zaidi na kutafuta amani yangu

5. Sikutafuta rafiki yake yeyote wala sikuongea na yeyote kuhusu mpenzi wangu, kifupi nilikata mzizi na kuondoka ma shina.

Hayo juu ni baadhi tu ya vitu nilivyofanya, kiukweli inaumiza kujitenga na mtu uliyempenda kwa dhati na kumjali kwa kila aombacho.

KUMBUKA.
Sikumuacha ila nilijipa muda kupona kwenye mateso na vifungo vya ajabu.

MAJIBU
Baada ya kugundua ukimya wangu ambao yeye aliona ni kero alianza kunitafuta kila saa na kuniuliza wapi nilipo ili aje tuongee, sikuwa najibu lolote zaidi ya ku bluetick huko whatsap tu hii ilimfanya akasogea zaidi na kumiss muda wangu kwake, haikuwa rahisi ila kwasasa tangu qjue kuwa ninaweza kuishi bila yeye amekuwa karibu na adabu imerudi.

FUNZO KWA WAJOMBA NA MAMSHANGAZI

JIFUNZENI KUITAFUTA AMANI YA MOYO WAKO MAANA ULIYENAYE ANAWEZA KUITUMIA KUKUUMIZA KWA KUKUONA WEWE MSUMBUFU.

INAUMA ILA INABIDI UZOEE.
NAOMBA KUWASILISHA
Kung'ang'aniza mapenzi sehemu ambayo hayapo ni jambo baya sana.

Ni ubinafsi mkubwa sana.

Yani hujitendei haki wewe unayeng'ang'aniza na huyo unayemg'ang'aniza naye humtendei haki.
 
Hii ni njia pekeee
Niliyoitumia baada ya njia zote kufeli
Mume wangu alikua ananiona kero na nilishafikia hatua ya kukata tamaa kabisa
Maana atakosea yeye mimi ndo nitaomba msamaha
Na kadhalika na kadhalika
Ila nilikuja kuwa busy nilijipa kazi nzito na ratiba ngumu
Then i stay like 3 weeks sitajmtafuta
Alishakua ameondoka (kikazi) ila mimi ndo nilikua bado nabembeleza
Hizo week 3
Kwa mara ya kwanza katika mahusiano yetu na ndoa miaka (10) ndio aliomba msamaha na kuomba tuanze upya

So now nina amani tele na sote kwa pamoja tuna amani

Ila niliamua tu kufocus na mimi,my self and i so nadhibitisha hii njia ina majibu
Uliposema una mume roho imeniuma sana nimeshindwa hata kuendelea kusoma ulichoandika.
 
Kwamba hii ni Kama Equation ?; Yaani... Tatizo A = Suluhisho B (wala hakuna variable zozote) ?

Maisha yangekuwa hivyo basi ingekuwa mteremko lakini variables ni nyingi na kila Case ni Tofauti. Lakini mwisho wa siku wewe kama muhusika ndio utatambua kama ni upepo na utapita au ndio hivyo anayekufukuza hakwambii Toka, na kama hii reaction ni reversible au ndio hivyo ishatoka hata ukiweka catalyst kiasi gani ni kupoteza muda
 
Una move on tu bablai
 
Back
Top Bottom