DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Siasa za kiafrica zinachagua makapi na kuacha mchele, ukiwa mchele huteuliwi, wanataka makapi yanayosema ndiooo kwa kila kitu, ili wasiharibu ulaji wa wakubwa, huko Duniani wenzetu kiongozi ni yule ambaye ni bora zaidi kuliko walio Bora, wazungu kila wakiona viongozi wetu wanacheka sana, kwamba Kama Hawa ndio viongozi je wananchi wao wakoje,
 
Siasa za kiafrica zinachagua makapi na kuacha mchele, ukiwa mchele huteuliwi, wanataka makapi yanayosema ndiooo kwa kila kitu, ili wasiharibu ulaji wa wakubwa, huko Duniani wenzetu kiongozi ni yule ambaye ni bora zaidi kuliko walio Bora, wazungu kila wakiona viongozi wetu wanacheka sana, kwamba Kama Hawa ndio viongozi je wananchi wao wakoje,
Tatizo siyo chuya ama mchele...

Tatizo ni mfumo wa kisiasa na kiutawala wa nchi yetu ambao unalea chuya...

Kwa mfumo huu tulio nao sasa, hata wewe mwenyewe "uliye mchele original" ukibahatika kuingia ndani ya mfumo huu, ghafla tu mfumo unakubadilisha na kuwa chuya original zisizofaa kupikwa wala kuliwa kabisa...!

Tunataka mfumo wa kisheria na kikatiba ulio strong kiasi cha hata kama pumba zitaingia ndani mfumo wa kiutawala na kisiasa wa nchi, uzibadilishe pumba hizo mchele original ufaao kupikwa na kuliwa na VIP...
 

Kina cha maji Ziwa Victoria chazidi kuongezeka, wananchi watahadharishwa​

Mariam John 0302Hrs   Juni 05, 2021 Habari
  • Mei mwaka 2020 wastani wa kina cha maji ziwani ulikuwa mita 1134.27 lakini kwa mwaka huu wa 2021 kimefikia mita 1134.87.
  • kuongezeka kwa kina hicho kumesababisha nyumba, mashamba na miundombinu kuzingirwa na maji.
  • Serikali yawataka watu kuondoka maeneo hayo.

Mwanza. Kufuatia kuongezeko kwa kina cha maji cha Zwa Victoria, Serikali imetoa tahadhari kwa watu wanaoishi kando ya ziwa hilo na kuwataka kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kufanya usafi wa mazingira, kupanda miti na kuepuka shughuli za kibinadamu kando ya ziwa.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Bodi ya Bonde la Ziwa Victoria, Gerald Itembu, mwezi Mei mwaka 2020 wastani wa kina cha maji ziwani ulikuwa mita 1134.27 lakini kwa mwaka huu wa 2021 kiwango kimeongezeka kwa 0.60 na kufikia mita 1134.87 ambazo hazijawahi kufikiwa katika kipindi chote.

“Hiki ni kipimo kikubwa kuwahi kurekodiwa tangu Bodi ya Bonde la Ziwa Victoria kuanza kurekodi taarifa zake miaka 50 iliyopita” amesema Itembu wakati akizungumza na waandishi wa habari jana Juni 4 jijini Mwanza.


Kutokana na kipimo hicho ni dhahiri kuwa maji hayawezi kupungua kirahisi badala yake yanaendelea kuongeza kadiri mvua zinavyozidi kuongezeka.

Itembu amesema watu wasilaumu maji yamewavamia katika maeneo yake isipokuwa yanafuata asili yake.

Amewataka watu waliokuwa au wanaofanya shughuli karibu na ziwa hilo kuchukua hatua ya kuondoka maeneo hayo huku akiwataka kutunza mazingira ili kuhakikisha hawafanyi shughuli ambazo ni hatari kwenye vyanzo vya maji.

Anasema kinachofanyika kwa sasa ni kufanya kipimo pale maji yalipofikia kutoka usawa wa bahari ili kutoa tahadhari kwa wananchi.

“Hii itasaidia kupunguza athari za kimazingira zinazoweza kutokea,” amesema


Madhara yaliyotokea baada ya kina cha maji kuongezeka ni pamoja na makazi ya watu na mashamba kuzungukwa na maji hasa katika mikoa ya Kagera, Mwanza na Mara.
 
02 June 2021

Kina cha maji Ziwa Tanganyika chaongezeka hadi mita 774.6 za mraba.​


site%201_0.jpg

Kina cha maji ya Ziwa Tanganyika kimeongezeka hadi mita za mraba 776.4 kutoka usawa wa bahari na kusababisha athari za mazingira pamoja na miundombinu ya serikali ikiwemo soko la kibirizi na majengo ya chuo cha uvuvi FETA Kigoma.
site%203_0.jpg


Mjiolojia wa bonde la Ziwa Tanganyika Bw.Respicius Mshobozi amesema kiwango hicho kimetokea kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1974 na kwamba kujaa kwa maji hayo kumechangiwa na mvua zinazonyesha mfululizo kwa miaka miwili.
.
Kuongezeka kwa kina cha maji ya Ziwa Tanganyika, kumefanya bodi ya bonde la Ziwa Tanganyika kukutana na kujadili athari zinazosababishwa na ongezeko la maji hayo, ambapo wameitaka jamii kuendelea kuzingatia sheria ya mazingira ya kutofanya shughuli za binadamu ndani ya mita 60 kutoka kwenye chanzo cha maji.
site%204.jpg


Aidha, Kwa upande wao wananchi ambao wameathirika kutokana na kujaa maji wameiomba serikali kuboresha maeneo ya shughuli za uzalishaji

 
Kilichonishangaza zaidi ni maeneo ambayo chanzo cha maji yametoka ziwa victoria nako kunamgao wa maji.sijui ziwa victoria nalo limekauka?Nchi hii shida sana.tumejikita kuwekeza kwenye anasa za viongozi na siyo kutatua changamoto za umma
 
Ilikuwaje kipindi cha utawala wa Magufuli mvua zilinyesha kwa wingi hadi kimo cha ziwa Tanganyika na Victoria vikaongezeka? Nini kimetokea baada yake maana ni kama mvua zimeanza kukata kiaina? Je Magufuli alikuwa na kibali gani kwa Mungu ambacho huyu wa sasa hana!? Je nikwasababu jina la Mwenyezi Mungu halitajwi sana kama ilivyokuwa? Mniwie radhi najaribu kuwaza tu!
 
Tatizo siyo chuya ama mchele...

Tatizo ni mfumo wa kisiasa na kiutawala wa nchi yetu ambao unalea chuya...

Kwa mfumo huu tulio nao sasa, hata wewe mwenyewe "uliye mchele original" ukibahatika kuingia ndani ya mfumo huu, ghafla tu mfumo unakubadilisha na kuwa chuya original zisizofaa kupikwa wala kuliwa kabisa...!

Tunataka mfumo wa kisheria na kikatiba ulio strong kiasi cha hata kama pumba zitaingia ndani mfumo wa kiutawala na kisiasa wa nchi, uzibadilishe pumba hizo mchele original ufaao kupikwa na kuliwa na VIP...
Nilitaka kumjibu hivi, hata huo mchele pure ukiingizwa kwenye system soon unabadilika kuwa chuya na mawe.

Linchi limejaa upuuzi mwingi sana.
 
Siasa za kiafrica zinachagua makapi na kuacha mchele, ukiwa mchele huteuliwi, wanataka makapi yanayosema ndiooo kwa kila kitu, ili wasiharibu ulaji wa wakubwa, huko Duniani wenzetu kiongozi ni yule ambaye ni bora zaidi kuliko walio Bora, wazungu kila wakiona viongozi wetu wanacheka sana, kwamba Kama Hawa ndio viongozi je wananchi wao wakoje,
Mkuu wa nchi ni kilaza,na yeye anateua vilaza,hata akiteua mwenye akili,hataweza kutumia akili zake,maana lengo na kipaumbele cha ccm,ni kubaki Madarakani kwa mbinu zote,
 
Tuna dharura ya ukosefu wa maji. Watawala hawaoni haja ya kuchukua hatua za haraka kupunguza makali ya upungufu huu. Kwao muhimu ni fursa ya kuonekana kwenye vyombo vya habari. Na hapo pesa nyingi zitaliwa.
Fikiria ni visima vingapi vingeweza kuchimbwa kwa pesa zilizotumika kwa uzinduzi wa matokeo ya sensa.
Sifahamu hata nini maana ya uzinduzi wa matokeo.
 
Safi sana, unaona faida za mitandao ya kijamii habari kama hii mungeiweka TBC au gazeti la uhuru mimi nisingeiona, lakini kupitia JF nimeiona, hongera sana.

Sasa, muwe mna toa ushuhuda kwa viongozi wa kisiasa kuwa mitandao ya kijamii na hasa JF inasaidia sana kufikisha ujumbe kwa wananchi wengi
Wana sikiliza basi hawa ahhh we lipa kodi tu
 
Mgao wa maji, kama maji yamepungua mto ruvu, hakuna uwezekano wa kuyazuiya hayo madogo yanayokwenda baharini? Ni kwa nini binadamu akose maji na huko yanapotelea baharini?
 
Ombi kwa DAWASA, please avail/give us water bill kama kawaidi pamoja ya kwamba kuna mgao. Isije kuwa meter inaendelea kusoma hata kama hamna maji.
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu yaliyo Jijini Dar es salaam , miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani pwani. DAWASCO inapokea maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Ndugu wana jukwaa, DAWASCO inajipambanua kwa kusimamia maadili ,kutoa huduma iliyotukuka pamoja na kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana kwa kila mwananchi.

Kama kutatokea kuharibika kwa bomba, wizi wa Maji, umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: DAWASCO - Welcome to new site
2. Kupitia mitandao yetu ya kijamii ikiwa ni pamoja na Twitter|DawascoOfficial..Facebook|DawascoOfficial ...Instagram|DawascoOfficial
3. Kwa mwananchiposta ; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu
DAWASCO
P. O. Box 5340
Sokoine Drive
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu huduma kwa wateja dawasco
0800110064 /022 2164800 ( Kupiga namba hizi ni Bure)

DAWASCO HUDUMA KWA WATEJA 0800110064
DAWASCO ILALA 0743 451879
DAWASCO KAWE 0743 451861
DAWASCO KIBAHA 0743 451875
DAWASCO KIMARA 0743 451865
DAWASCO KINONDONI 0743 451863
DAWASCO BAGAMOYO 0743 451877
DAWASCO MAGOMENI 0743 451862
DAWASCO TEGETA 0743 451881
DAWASCO TABATA 0743 451867
DAWASCO TEMEKE 0743 451866

Tunashukuru sana Dawasco kutuwekea huduma hii, nimejaribu kuangalia watu wote wliotoa maoni lakini sijaona majibu yenu. Nami natoa maoni yangu kama ifuatavyo, mmetrutangazia mgao wa maji lakini kuna sehemu hapa kimara mwisho, Kata ya Saranga King'ongo kuanzia Mengeni Msikitini mpaka Samaki Samaki tangu mgao umeanza hatujapa maji. Lakini wenzetu walio tuzunguka wanapata maji. Tafadhalini tunawaomba sana maji tunanua sh 40000 kwa lita 1000 na hatujui usalama wake. Tunaomba (japo ni haki yetu) mtupatie maji kama ratiba inavyosema.
Asanteni sana.
 
Back
Top Bottom