Jinsi ya kufanya astral travel
Kwanza, lazima tudhibiti mawazo yetu, lazima tudhibiti mawazo yasiyo na maana ambayo hupita kwenye akili zetu kila wakati. Keti mahali ambapo unastarehe, ambapo unaweza kupumzika kabisa, na ambapo hakuna mtu anayeweza kukusumbua. Ukitaka, zima taa kwa sababu mwanga unaweza kuwa kikwazo wakati kama huu. Kaa kimya kwa muda kidogo ukifikiria mawazo yako, tazama mawazo yako, angalia jinsi yanavyozidi kutambaa kwenye fahamu zako, kila moja likijaribu kuengua wazo jingine. ugomvi ule na mtu ofisini, bili ambazo hazijalipwa, gharama ya maisha, hali ya ulimwengu, yale ambayo ungependa kumwambia mwajiri wako—yafagie yote kando!
Fikiria kuwa umeketi kwenye chumba giza kabisa juu ya skyscraper; mbele yako kuna dirisha kubwa lililofunikwa na screen nyeusi, screen ambayo haina 0atterns, hakuna kitu ambacho kinaweza kuleta distraction. Itazame ole screen. Awali ya yote hakikisha kwamba hakuna mawazo yanayovuka ufahamu wako (ambayo ni ole screen nyeusi), na ikiwa mawazo yanaelekea kuingilia, yarudishe nyuma juu ya ukingo. Unaweza kufanya hivyo, ni suala la mazoezi tu. Kwa muda fulani mawazo yatajaribu kupepesa kwenye ukingo wa screen hiyo nyeusi, yarudishe nyuma, kwa nguvu na kuyataka yaondoke, kisha zingatia tena screen, halafu iinue ile sceeen ,katika fikra zako,iinue ile screen uone nini kipo nyuma ya pazia .
Unapo8tazama ile screen nyeusi utagundua kwamba kila aina ya mawazo ya ajabu yanataka kuingia. Yarudishe nyuma, yarudishe kwa jitihada , usiruhusu mawazo hayo kuingia (ndiyo, tunajua kwamba tumesema hili kabla, lakini tunajaribu kuhakikisha kuwa inaeleweka). Unapoweza kushikilia hisia ya boank kabisa kwa muda mfupi, utagundua kuwa kuna 'snap' kama kipande cha ngozi kinapasuka, basi utaweza kuona mbali na ulimwengu wetu huu wa kawaida, na kuingia katika ulimwengu beyond time and space. Kwa kufanya mazoezi haya, kwa kufanya hivi, utagundua kuwa unaweza kudhibiti mawazo yako kama wanavyofanya Adepts na Masters.
Jaribu, jizoeze, kwani ukitaka kuendelea ni lazima ujizoeze na ujizoeze hadi uweze kushinda mawazo yasiyo na maana.