Dereva fahamu HAKI na WAJIBU wako unapokutana na Traffic Barabarani kuepusha Migogoro

Mi nitajibu namba 11.

Traffic anaweza kukuandikia kwa kuweka namba yako ya gari na namba ya simu
 
Mi kuna aliyenikamata kwa kunisingizia kwamba ameruhusu gari ziende mimi nikaendelea kusimama,
Nilipombishia kulipa faini anipeleke mahakamani,akanipeleka kituoni,mkubwa wake alinipokea kwa kejeli kwamba
ninavyoona huyu polisi kalipenda gari langu kuliko mengine?
Na kuambiwa waniweke ndani wakati wanaandaa kesi yangu au niite ndugu zangu wanidhamini.
Kwa kuzingatia kauli ya mkubwa aliyonipokea nayo nikaona isiwe tabu,ngoja nilipe faini.

kuanzia siku hiyo wakinikamata iwe kwa haki au kwa kuonewa nafanya moja kati ya mawili au nalipa faini.
au natoa hela ya kubulashi viatu nawahi majukumu yangu.
 
Chukulia huna vyote.
Anatakiwa kuandika namba ya gari na kukupa maelekezo ya ni kituo gani umpelekee leseni ndani ya masaa 72
yakipita bila kumpelekea unahesabiwa makosa na utapatikana kwa usajili wa namba ya gari yako.
 
Atakupeleka kituo cha polisi, utaacha gari hadi utakapo peleka leseni
Haya ni mawazo sio sheria,sasa hayo masaa 72 ni ya nini?
inamaana gari ikikaa kituo cha polisi yakapita masaa 72 inapigwa mnada?
 
Je ni kwa mujibu wa sheria ? Unaweza taja kifungu gani?

Anatakiwa kuandika namba ya gari na kukupa maelekezo ya ni kituo gani umpelekee leseni ndani ya masaa 72
yakipita bila kumpelekea unahesabiwa makosa na utapatikana kwa usajili wa namba ya gari yako.
 
Mmmhhh.... Huoni hapa unafuga maovu? Unadhani kwa style hii si watanzania watazidi kuonewa?

 
You are right, I was trained this way by a certified instructor. Moreover wa kushoto kwako atadhania unaenda kushoto na wa kulia kwako atadhania unaenda kulia, mkanganyiko huu unaweza kuleta ajali
 
Nenda kasome NIT au veta, msiende kwenye vyuo umiza km zamani.

Hayo maswali yte utapata majibu yke huko.
 
Ni hazard tu wakuu..hakunaga double hazard coz hakuna single hazard...kwako mwalimu kashasha!!
 
Je ni kwa mujibu wa sheria ? Unaweza taja kifungu gani?
Kwa kweli kifungu sikijui,lakini nimejibu kwa kutumia mafunzo niliyojifunza chuo cha usafirishaji,wakati nafundishwa defensive driving.
kama wapo humu,wanaweza kupinga au kuthibitisha.
 
Mmmhhh.... Huoni hapa unafuga maovu? Unadhani kwa style hii si watanzania watazidi kuonewa?
Ili uonevu uishe kuna sheria nyingi inabidi zibadilishwe,kwa mfano ilitakiwa siku hiyo hiyo
nipandishwe kizimbani na kusomewa mashtaka,na siyo polisi anapewa mamlaka ya kuniweka ndani ili aandae mashtaka
au nipate wadhamini na wadhamini kumbuka lazima waende serikali za mitaa au wawe na barua za waajiri wao ndo waje
kunidhamini,kisa natetea haki ya kutolipa 30000/= kuchangia nchi kuingia uchumi wa kati.
Mengine lazima utumie kanuni ya funika kombe mwanaharamu apite.
 
Wewe kumbe huwajui polisi, akikuona unajua sana haki zako anakusingizia ulitaka kumgonga, ukienda kituoni unawekwa ndani halafu wanakuunganisha kwenye kesi ya mauaji ambayo hata hujawahi kuisikia, na hakuna dhamana. Ndio maana mimi nikipandishiana nao halafu nikiona wanadinda basi huwa nawapa grease kidogo maisha yanaendelea
 
You are absolutely right. Nadhani dawa ni kuwa muungwana na kumueleza changamoto nadhani kamanda ataelewa tu. Sheria inapaswa iendane na hekima katika kutafsiri.
 
hapo sawa
 
Si kweli. Labda wanawaonea maamuma. Mimi siandiki kizembe wewe.mwaka huu mpaka mwezi huu sijaandikiwa kosa wala kulipa rushwa na mon to sunday nipo barabarani. Labda kama wewe ni daladala...
Mnalea ubovu mjue haki zenu.
Ndugu gari yako ni aina gani?
Kama una suzuki carry au lori
jaribu kuliendesha siku moja uone tunachozungumza hapa.
Mimi nikiendesha gari nyingine kwa kweli nakumbuka nilisimamishwa nikiwa naenda mkoani tena
kwa mambo ya speed,basi lakini endesha suzuki carry liwe na kila kitu kimekamilika hata ile simamishwa simamishwa tu
inakufanya siku nyingine usiliendeshe maana uwe na uhakika utachelewa huko uendako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…