Dereva fahamu HAKI na WAJIBU wako unapokutana na Traffic Barabarani kuepusha Migogoro

Dereva fahamu HAKI na WAJIBU wako unapokutana na Traffic Barabarani kuepusha Migogoro

Mi nitajibu namba 11.

Traffic anaweza kukuandikia kwa kuweka namba yako ya gari na namba ya simu
 
Mi kuna aliyenikamata kwa kunisingizia kwamba ameruhusu gari ziende mimi nikaendelea kusimama,
Nilipombishia kulipa faini anipeleke mahakamani,akanipeleka kituoni,mkubwa wake alinipokea kwa kejeli kwamba
ninavyoona huyu polisi kalipenda gari langu kuliko mengine?
Na kuambiwa waniweke ndani wakati wanaandaa kesi yangu au niite ndugu zangu wanidhamini.
Kwa kuzingatia kauli ya mkubwa aliyonipokea nayo nikaona isiwe tabu,ngoja nilipe faini.

kuanzia siku hiyo wakinikamata iwe kwa haki au kwa kuonewa nafanya moja kati ya mawili au nalipa faini.
au natoa hela ya kubulashi viatu nawahi majukumu yangu.
 
Chukulia huna vyote.
Anatakiwa kuandika namba ya gari na kukupa maelekezo ya ni kituo gani umpelekee leseni ndani ya masaa 72
yakipita bila kumpelekea unahesabiwa makosa na utapatikana kwa usajili wa namba ya gari yako.
 
Atakupeleka kituo cha polisi, utaacha gari hadi utakapo peleka leseni
Haya ni mawazo sio sheria,sasa hayo masaa 72 ni ya nini?
inamaana gari ikikaa kituo cha polisi yakapita masaa 72 inapigwa mnada?
 
Je ni kwa mujibu wa sheria ? Unaweza taja kifungu gani?

Anatakiwa kuandika namba ya gari na kukupa maelekezo ya ni kituo gani umpelekee leseni ndani ya masaa 72
yakipita bila kumpelekea unahesabiwa makosa na utapatikana kwa usajili wa namba ya gari yako.
 
Mmmhhh.... Huoni hapa unafuga maovu? Unadhani kwa style hii si watanzania watazidi kuonewa?

Mi kuna aliyenikamata kwa kunisingizia kwamba ameruhusu gari ziende mimi nikaendelea kusimama,
Nilipombishia kulipa faini anipeleke mahakamani,akanipeleka kituoni,mkubwa wake alinipokea kwa kejeli kwamba
ninavyoona huyu polisi kalipenda gari langu kuliko mengine?
Na kuambiwa waniweke ndani wakati wanaandaa kesi yangu au niite ndugu zangu wanidhamini.
Kwa kuzingatia kauli ya mkubwa aliyonipokea nayo nikaona isiwe tabu,ngoja nilipe faini.

kuanzia siku hiyo wakinikamata iwe kwa haki au kwa kuonewa nafanya moja kati ya mawili au nalipa faini.
au natoa hela ya kubulashi viatu nawahi majukumu yangu.
 
2. Je ni sahihi mtu kuwasha double hazard anaposimama kwenye zebra/alama ya pundamilia ili na wenzie nao wasimame?ni kwa mujibu wa sheria?

Si sahihi kuwasha double harzad unaposimama kwenye zebra, unapotaka kunyoosha njia panda au unapovuka reli.
Kuwasha double harzad unamaanisha umepata matatizo kwa hiyo una ruhusu gari zilizo nyuma yako zipite
You are right, I was trained this way by a certified instructor. Moreover wa kushoto kwako atadhania unaenda kushoto na wa kulia kwako atadhania unaenda kulia, mkanganyiko huu unaweza kuleta ajali
 
Nenda kasome NIT au veta, msiende kwenye vyuo umiza km zamani.

Hayo maswali yte utapata majibu yke huko.
 
2. Je ni sahihi mtu kuwasha double hazard anaposimama kwenye zebra/alama ya pundamilia ili na wenzie nao wasimame?ni kwa mujibu wa sheria?

Si sahihi kuwasha double harzad unaposimama kwenye zebra, unapotaka kunyoosha njia panda au unapovuka reli.
Kuwasha double harzad unamaanisha umepata matatizo kwa hiyo una ruhusu gari zilizo nyuma yako zipite
Ni hazard tu wakuu..hakunaga double hazard coz hakuna single hazard...kwako mwalimu kashasha!!
 
Je ni kwa mujibu wa sheria ? Unaweza taja kifungu gani?
Kwa kweli kifungu sikijui,lakini nimejibu kwa kutumia mafunzo niliyojifunza chuo cha usafirishaji,wakati nafundishwa defensive driving.
kama wapo humu,wanaweza kupinga au kuthibitisha.
 
Mmmhhh.... Huoni hapa unafuga maovu? Unadhani kwa style hii si watanzania watazidi kuonewa?
Ili uonevu uishe kuna sheria nyingi inabidi zibadilishwe,kwa mfano ilitakiwa siku hiyo hiyo
nipandishwe kizimbani na kusomewa mashtaka,na siyo polisi anapewa mamlaka ya kuniweka ndani ili aandae mashtaka
au nipate wadhamini na wadhamini kumbuka lazima waende serikali za mitaa au wawe na barua za waajiri wao ndo waje
kunidhamini,kisa natetea haki ya kutolipa 30000/= kuchangia nchi kuingia uchumi wa kati.
Mengine lazima utumie kanuni ya funika kombe mwanaharamu apite.
 
Wewe kumbe huwajui polisi, akikuona unajua sana haki zako anakusingizia ulitaka kumgonga, ukienda kituoni unawekwa ndani halafu wanakuunganisha kwenye kesi ya mauaji ambayo hata hujawahi kuisikia, na hakuna dhamana. Ndio maana mimi nikipandishiana nao halafu nikiona wanadinda basi huwa nawapa grease kidogo maisha yanaendelea
 
Na mimi naomba kuchangia. Mko njia kuu nje ya mji kwa mfano nje ya 50; mbele kuna milori kadhaa imetangulia mwendo mdogo sana. Unayafuata taratibu ukisubiria upate sehemu inayokuruhusu ku-overtake.

Mungu si Athumani, unaruhusiwa ku-overtake bila hiana mbele kweupe unaingia kulia. Lol! kumbe msafara mrefu kiasi, hamad, dotted line imefikia mwisho huwezi kurudi kushoto kwa sababu kuna gari; unakanyagia ili ulimalizie lile lori then unarudi kushoto tayari ulishavuka dotted line.

Duh! Balaa, kumbe walikuwa wamejificha mahali, ghafla wanaibuka barabarani unawekwa pembeni. Michezo hii ipo sana Kibaha - Mlandizi na Dumila - Gairo. Jamani, tukienda kiuhalisia hapo kosa langu ni lipi?

Kumbuka mstari wa kuniruhusu ku-overtake unapoanzia sijavaa darubini ili nijue unaishia wapi; ni hadi mita chache kabla ya unapoishia ndipo napoweza kugundua unaishia pale; siwezi kurudi kwa sababu kushoto kuna gari.

This is a very stupid regulation; nilishapigwa sana mabao ya aina hii. Sheria (I think rule) hii ilitakiwa izingatie zaidi ulipotokea/ingilia na sio pale dereva alipomalizia kutokana na changamoto niliyoileza hapo juu. Wahusika waliangalie hili.
You are absolutely right. Nadhani dawa ni kuwa muungwana na kumueleza changamoto nadhani kamanda ataelewa tu. Sheria inapaswa iendane na hekima katika kutafsiri.
 
Double hazard kwenye junction kuonesha unanyoosha ni kuiokosea sheria ya usalama barabarani, matumizi yake ni parking ya dharula tu.

Kwenye junction yenye makutano ya njia nne na wewe uelekeo wako ni mbele, hauwashi chochote, bali kabla ya kuingia kwenye hiyo junction, pepesa macho kulia kuona kama kuna mtu ashaingia usubiri, baada ya hapo kanyaga wese kunyooka mwanawane.
hapo sawa
 
Si kweli. Labda wanawaonea maamuma. Mimi siandiki kizembe wewe.mwaka huu mpaka mwezi huu sijaandikiwa kosa wala kulipa rushwa na mon to sunday nipo barabarani. Labda kama wewe ni daladala...
Mnalea ubovu mjue haki zenu.
Ndugu gari yako ni aina gani?
Kama una suzuki carry au lori
jaribu kuliendesha siku moja uone tunachozungumza hapa.
Mimi nikiendesha gari nyingine kwa kweli nakumbuka nilisimamishwa nikiwa naenda mkoani tena
kwa mambo ya speed,basi lakini endesha suzuki carry liwe na kila kitu kimekamilika hata ile simamishwa simamishwa tu
inakufanya siku nyingine usiliendeshe maana uwe na uhakika utachelewa huko uendako.
 
Back
Top Bottom